Ukichunguza kwa umakini ndoa ni Shimo la mateso matupu

Ili ndoa iwe tamu basi mmoja awe bwege. Wanaume wengi ndoa zinakua shubiri kwao pale mke anakataa kuwa bwege

Wanawake ndoa zinakua chungu

1. mume akikosa pesa
2.akiwa karibu sana na ndugu zake
3 etc
 
Vitabu vyote vya kiimani vimekemea uzinz, uzinz ni source ya hali ngumu ya kimaisha na ndo mana wengi wetu maisha yetu hohehae kwsbb ya uzinz, NDOA ni muhim
 
Matatizo uliyoyataja yapo hata kama haupo kwenye ndoa,
Kama unaingia kwenye ndoa kuepuka stress,utqkuwa unachemka,
Zipo stress za pesa,za ajira,boss mkali,
Stress za magonjwa.stress za familia l,ndugu,
Tatizo kubwa watu wanaingia kwenye ndoa bila kujua lengo la ndoa,kwenye ndoa hautafuti mtu mkamilifu,unatafuta mwenza mkamilishane mapungufu yenu,
Usiingie kwenye ndoa bila kujua tofauti ya kuwa mme,mke,baba,mama,
Unaoa harafu Bado unataka uishi kama boyfriend,girlfriend,au uendelee kuishi kama msela wa gheto,
 
Kosa kubwa lingine ni mtu kukubali ndoa ni mateso na akakubali kuishi hivyo kwa kuamini hivyo atateseka mara 2 zaidi ya awali
 
Kumbe hapa napo pana darasa, komment hii imenifunza usiruhusu hisia/nyege ziongoze maamuzi yako.
 
Mara nyingi nyinyi mnaoandika hivi ni watoto wa mitaani. Ndoa zenye amani zipo nyingi tu. Msiwe mnaandika ushuzi ushuzi bila takwimu.
 
Ndoa inaundwa na watu wawili na lazma muwe mmejuana inside out.

Hakikisha mwanamke wako anayajua madhaifu yako na wewe unayajua yake kisha ndio mfanye maamuzi sasa ya kuoana. Ikiwa hutayajua madhaifu ya mwenza wako basi ujue ndoa yenu ikimaliza miezi 6 bila mgogoro Mungu anawapigania.

Shida nayoiona wengi huwa tunagubikwa na fantasies na kusahau kuwa ndoa ni uhalisia. Ndoa sio maigizo hivyo kila mtu lazma awe real na mwenzake.
 
Kosa kubwa lingine ni mtu kukubali ndoa ni mateso na akakubali kuishi hivyo kwa kuamini hivyo atateseka mara 2 zaidi ya awali
Nakubaliana nawe, mtu akiweza kuiset akili na ufahamu wake hata kama yupo jela ataona kawaida tu maadamu anaishi.
Ila siku zote juwa mwanadamu na pengine viumbe vyote vinapigania uhai na uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…