Ukichunguza kwa umakini ndoa ni Shimo la mateso matupu

Hajaoana na mtu wanaowezana watu wanatucheka siye kwanini tupo na umri zetu single .

Sio kwamba hatujawahi pata wanaume wafuatao

Mwenye hela , mzuri anaafya zake tumekutana ila shida nitabia huwezi ishi na mtu anadharau heshima Hana kero tu .

Halafu watu wanashangaa huyu kwanini haoelewi watu wanaangalia rafiki wakupendezana naye , kuchukuana , na maelewano Sasa .

Kwa matusi ya humu yakutosha finally kapatikana rafiki kipenzi , maelewano yapo hata ukiwa naye sio mapenzi tu ndio mnafanya hapana hata kufurahiana mwaweza lala Kwa kiss tu ni enough.

Nyie mnaoana kisa mnachekeana humjui undani wake .

Na mtaoanaje na mwanamke ambaye hamuendani mmoja anasali mwingine mwanga .😁😁😁 Mwingine kazoea disco mwingine amezoea tamasha za maombi na kusifu oa wakufanana naye
 
Partnership yeyote sio ndoa tu inaweza kupitia hayo yote kutokana na tofauti binafsi.
 
Ninachoweza kusema, Ndoa ni mateso sana sana. Mimi nina miaka 6 kwenye ndoa sijakaa na mke wangu kwa takribani miaka miwili mpaka alipohamishwa kuja mkoa ninalofanyia kazi, Dah niliwish sana aje walau niondokane na upweke niliokuwa nao. Ninampenda sana kiasi kwamba kuchepuka imekuwa kama alarm, kila ninapotaka kufanya hivyo nikimkumbuka najikuta naacha. Sasa baada ya kuhamia yaani amekaa tu miezi miwili tabia yake ikaanza kubadilika tumebahatika kupata watoto wawili, cha ajabu. Sometimes ananiambia waogeshe hao wanao..Mimi nikiendelea kupika jikoni. Offcourse si mbaya kwangu kuogesha wanangu lakini lugha anayoitumia utafikiri mimi ni mdogo wake. Kibaya zaidi unakuta nimewahi kurudi nyumbani walau nikashinde naye, nikiiingia chumbani namkuta amelala, ile nafungua tu mlango analalamika kusema ahaa umerudi ahaa huchelewi kidog walau nilale, hapo ni saa moja jioni , hajaanza hata kupika chakula. Offcourse tunaweza kukaa hata siku nne bila kuongea kisa kitu kidogo sana mpaka mimi nianze kumwongelesha. zamani tulikuwa tunakula wote chakula kwenye sahani moja, siku hizi hataki kabisa yaani...Unajiuliza hivi si bora angeendelea na kazi yake huko singida? maana radha ya ndoa imekuwa chungu kweli. Naweza rudi usiku sana toka kazini kutokana na changamoto za kazi, nikamjulisha kuwa leo nitachelewa kurudi, yaani inaweza fika hata saa tano usiku hajakupigia simu, ni mtu asiyejali kabisa, mbaya zaidi ukifika akikufungulia mliango hakuna kukupokea wala cha pole, yeye ni ndani huku hapo nimebeba vyakula, zawadi yake na vitu vyangu vya kazini. Achana na lile la kitandani, huwa najitahidi sana kumpa haki yake ipasavyo, mpaka nihakikishe ameridhika na nimelowana, ndipo sa naamini tupo pamoja, Matumizi pamoja na kwamba ana mshahara wake sijawahi mwomba hela, bali kila mwisho wa mwezi nampa hela ya matumizi.

Sasa pamoja na yote haya unajiuliza shida ninini? yaani ndoa imekuwa chungu mno aisee...natamani nirudi kuishi mwenyewe, kwanza speed ya maendeleo ilikuwa kubwa zaidi, Nilifungua ofisi mbili na zilikuwa zinaendelea vyema, lakini huwezi amini toka nifungue hajawahi kaa dukani hata weekend moja tu toka subuhi mpaka jioni, na hata nikiomba nimpe hela akajumue vitu siku ya weekend anasema, hawezi, hiyo kazi ni ngumu mno...yani imekuwa shida juu ya shida.
 
Umemaliza yote mkuu[emoji4][emoji119][emoji1431]
 

hatari sana ndoa ndoano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…