Ukienda kutafuta maisha kwenye mikoa hii ni ngumu sana kutoboa

Ukienda kutafuta maisha kwenye mikoa hii ni ngumu sana kutoboa

Wewe kweli hujaelewa mada. Sasa wewe hapo kama kijana wa kitanzania unaweza kutoka Dar ukaja kutafuta maisha Izimbya??

Achana na wakazi, mikoa yote ukiangalia wakazi unakutaga wana maisha mabovu kuliko wanaokuja kutafuta. Hilo ni jambo la kawaida.

Hapa tunaongelea uwezekano wa huyo wa kuja kutumia fursa zilizopo kutoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani kazungumzia kagera ya mtukula tu au yote kwa ujumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kazungumzia kagera ya mtukula tu au yote kwa ujumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani kwenye mada hakuna Kagera kuna Bukoba.

Ila hata kama ni Kagera na vijiji vyote jambo unalotakiwa kujua ni kwa sehem yoyote wewe unapoingia katika jamii ya watu wa kijijini siku zote utawakuta wao hawapigi hatua kwa kuona hakuna fursa. Sasa wewe ukiingia ukataka kufanya yale yale wanayofanya wao ukategemea kutoboa ni ndoto!

Usiseme mtu akienda vijiji vya Kagera kwa ku refer shughuli za wakazi wa pale. Ukumbuke shughuli hizo ndo zinazowafanya wasitoboe. We ukiamua kwenda lazima uangalie fursa zilizopo ambazo either hawazioni au wanaziona wanazitumia kimazoea we unaziboresha na kuzifanya kibiashara.

Mfano nimekuja huku huku vijiji vya Kagera nikakuta watu wanafuga mbuzi kama ambavyo na wewe unajua. Mtu unakuta anafuga eti mbuzi wawili hadi mbuzi 7! Sasa hapo mtu anafuga mbuzi au anaishi na mbuzi?? Mimi nimeanza kufuga mbuzi hao hao seriously sasa hivi nimeshafikisha mbuzi 32 na target yangu ni kumaliza mwaka na mbuzi 100!

Sasa hapo ukiniuliza mimi unategemea nikwambia hakuna fursa za kutoboa?? Ila kwa kuwa wewe tukizungumzia kutoboa unakimbilia kumuangalia mwenyeji huwezi kuona kama tatizo liko kwa wenyeji.

Kwanza dada yangu tukubaliane sis wahaya ni wavivu wa kutupwa. Kagera yetu karibia mazao yote unayoyajua yanastawi vizuru tu na tuna mvua za kutosha. Ndugu zako hawatoboi huko vijijini kwa ajili ya uvivu wao wa kulima eka moja ya migomba na mazao wanachanganya humo humo msimu kwa msimu na kutopenda kufanya kazi alafu na wewe unawatetea kwa kusingizia eneo walipo. Sio kweli.

Kwa mtu anayejua kutafuta na ambaye yuko Smart kutoboa ni rahisi sana kama utakuja kufanya tofauti na wenyeji ila ukija ukachukua akili ya wenyeji WAFWAAA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ieleweke ni ngumu sana kufanikiwa kimaisha SIO haiwezekani kufanikiwa:-

- Arusha
- Kilimanjaro
- Tabora
- Simiyu
- Geita
- Kigoma
- Lindi
- Mtwara
- Ruvuma
- Bukoba
- Mara
- zanzibar yote

Hiyo mikoa kama ndio unataka kuanza kutafuta maisha sikushauri uende.
We unaishi mkoa gani ambapo umefanikiwa kwa kiasi gani, tuanzie hapo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ieleweke ni ngumu sana kufanikiwa kimaisha SIO haiwezekani kufanikiwa:-

- Arusha
- Kilimanjaro
- Tabora
- Simiyu
- Geita
- Kigoma
- Lindi
- Mtwara
- Ruvuma
- Bukoba
- Mara
- zanzibar yote

Hiyo mikoa kama ndio unataka kuanza kutafuta maisha sikushauri uende.
Geita,nimekuelewa sana,hili halina ubishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimanjaro na Bukoba sawa.ila Arusha big no.Geita usikae mjini ukitaka kufanikiwa na Tabora siku hizi pamechangamka ukijituma pesa inapatikana
 
Arusha, Kilimanjaro watu wamekaba kila kona hata majani yanauzwa Kigoma imejitenga sana mpaka umalize wilaya zote ndio ukute mkoa mwishoni kwa Zanzibar hasa Pemba chenchi ya elfu kumi mpaka uende bank

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...Wenzako wamekuja huku Zanzibar wakiwa dhaifu wakaondoka mashujaa ...wamekuja masikini sa ivi alhamdulillah wanajiweza kimaisha ...wengine walikuja kulelewa tu huku sa ivi wanatamba tu mjini wengine wamechukua mpaka mazari ya uongozi wa nchi hii ...Ali Hassan Mwinyi kaletwa kulelewa tu hatimae kawa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ...nadhani huijui Zanzibar wewe!!
 
Kama mtu atashindwa kufanikiwa Zanzibar basi hata fanikiwa popote Zanzibar kutoka ni rahisi Sana.
Write your reply...Wenzako wamekuja huku Zanzibar wakiwa dhaifu wakaondoka mashujaa ...wamekuja masikini sa ivi alhamdulillah wanajiweza kimaisha ...wengine walikuja kulelewa tu huku sa ivi wanatamba tu mjini wengine wamechukua mpaka mazari ya uongozi wa nchi hii ...Ali Hassan Mwinyi kaletwa kulelewa tu hatimae kawa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ...nadhani huijui Zanzibar wewe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo umeongea kweli lakini huenda hiyo idadi kubwa ya hilo kabila ni kutokana na wenyeji wa maeneo hayo ndio wao kwa hiyo lazima watakua wengi tu ukilinganisha na makabila mengine ambayo ni wachache mkoani hapo sababu sio wenyeji wa huo mkoa, au sio?

Nimefanya kazi kwenye maeneo mengi Tanzania hilo nimeliona kila eneo wenyeji lazima wazidi wageni kwenye kila idara ila utofauti nimeona huko huko Arusha tulikua na ziara kwenye hivyo viwanda lakini idadi ya warangi na wanyaturu ni kubwa kuliko idadi ya wameru na waarusha / wamasai kwenye viwanda vya a to z kule kisongo na unga limited almost maeneo yote ya viwanda, na kuna utamaduni kwamba wahindi hupendelea kuwaajiri hao sababu ya dini zao na hukubali mshahara wowote na sio wasumbufu.

Nimejaribu tu kushare nilichokiona mwenyewe maeneo hayo.
Kuhusu uchapaji kazi kwa Wanyaturu hilo halina shaka afu Sio wasumbufu.
 
Ieleweke ni ngumu sana kufanikiwa kimaisha SIO haiwezekani kufanikiwa:-

- Arusha
- Kilimanjaro
- Tabora
- Simiyu
- Geita
- Kigoma
- Lindi
- Mtwara
- Ruvuma
- Bukoba
- Mara
- zanzibar yote

Hiyo mikoa kama ndio unataka kuanza kutafuta maisha sikushauri uende.
Ongeza na MWANZA nmekaa mwaka wa sita sijaelewa biashara ya huku inaendaje kuna ukora flani ivii ukifungua duka uko jirani na Ngosha basii hauzi kitu
 
Ieleweke ni ngumu sana kufanikiwa kimaisha SIO haiwezekani kufanikiwa:-

- Arusha
- Kilimanjaro
- Tabora
- Simiyu
- Geita
- Kigoma
- Lindi
- Mtwara
- Ruvuma
- Bukoba
- Mara
- zanzibar yote

Hiyo mikoa kama ndio unataka kuanza kutafuta maisha sikushauri uende.
Hujui kuchungulia fursa

Euvuma, kigoma, Lindi, mtwara, na simiyu kuna fursa Tele
Btw, hakuna mkoa wa bukoba
 
Back
Top Bottom