Ukienda kutafuta maisha kwenye mikoa hii ni ngumu sana kutoboa

Nakubishia kwenye muingiliano wa watu.hakuna mkoa wenye muingiliano mkubwa wa watu tz kama Kagera.mkoa huu ndo unaongoza Kwa wahamiaji Kwa sababu ya giografia yake ndo maana ukimwi ulipitia huko na tishio la ebola wanaanzaga na Kagera Kwanza maana kwa muingiliano wa watu kutoka mataifa mbalimbali ni kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sawa mkuu, Bukoba nyama kilo ni 5,000/= niambie mji unaponunua nyama sh 3,000/=

Bukoba maharage ni sh 1,800 kwa kilo niambie mji unaponunua maharage sh 1,000/=

Bukoba mchele ni 1,600 niambie wewe mji unaponunua kwa sh 1,000/= kama sio mashambani kwenyewe.
Ujue pia kwa Bukoba ndizi ni za bei ya kuokota ukilinganisha na miji mingine.

Bukoba boda boda hata kwa mia tano anakupeleka unapotaka kwenda!


Na kwa taarifa yako tu mkuu mimi sijaona mji ambao samaki wanauzwa bei ya kutupwa. Samaki wa 2,000 hapa Bukoba kwa Kigoma ni samaki wa 10,000/= na kwa Dar ni samaki wa 8,000-10,000/=

Kuhusu vyumba vya kupanga ndo sawa na kuokota. Kwa wenzangu tuliozoea vyumba vya Dar ukija Bukoba unacheka tu. Maana vyumba huku vinaanzia 15,000 na kuendela. Na chumba cha 30,000/= ni kikubwa sana na cha standard nzuri sana.


Unasema "hiyo vanilla unadhani kulima ni kazi rahisi" hii inanionesha kumbe wewe hauangalii fursa unataka vya bwelele. Unataka kazi rahisi ndo utoboe eeh!? Hii ndo aina ya vijana tulio nao!

Hata kama nguo zinanunuliwa Katoro hakuna shida. Hata zingenunuliwa Mwanza hakuna shida. Cha msingi ni zikishaletwa soko lipo??

Alafu sijasema Bukoba kuna mzunguko mkubwa sana wa biashara, ninachosema unaweza kuwa eneo lenye mzunguko mkubwa wa biashara na matumizi yakawa makubwa ukaishia kupata faida na kula tu. kwa Bukoba hela sio rahisi sana kupatikana ila ukichungulia fursa ukazitumia uwezekano wa kutoka ni mkubwa sana kwa kuwa matumizi yake yapo chini sana.

Tatizo tunapenda kufanya yale yale ambayo wenzetu wanayafanya katika maeneo mengine na sisi tuyafanye popote tunapotaka kutafuta riziki. Huwezi kuona mwenzio anapiga biashara ya mtumba inamtoa Dar na wewe ukataka kufanya biashara hiyo Lindi bila kuanza kuanhalia kwa Lindi ni biashara gani inaenda zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kuwa SMART ni muhimu lakini maelezo yako hapo chini naona yameegamia kwenye SWOC analysis.
 
Hujanielewa nazungumzia muingiliano wa watu kutokana na shughuri za kiuchumi, kama ilivyo mikoa mingine ya mipakani!! Sasa unapakana na burundi, Rwanda, kule kuna nini? Kidogo hiyo mtukula nayo ni ya miaka ile. Nenda mipaka inayopakana na kenya, au tunduma ndio utanielewa ninachozungumzia hapa na sio wahamiaji!!!
 
Maisha ni popote.. Changamoto za kwenye hiyo mikoa ndio fursa zenyewe...

Umeitaja Simiyu? Unaijua Simiyu lakini? Umeshawahi fika pale makao makuu ya mkoa, Bariadi?
Waambie bhana mie niko ruvuma hali ngumu kweli ila sio malambo bariadi maana fursa ni nyingi sana kuuza maji tu kwa siku unapata hela kibao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya arusha wakora wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wengi vijijini kabla ya ujio wa pikipiki walijishughulisha na kahawa......kulima kulangua nk

Kagera kugumu acheni sifa zisizo na mantiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wengi vijijini kabla ya ujio wa pikipiki walijishughulisha na kahawa......kulima kulangua nk

Kagera kugumu acheni sifa zisizo na mantiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani hukuelewa mada ya mtoa post. Hata mimi kwa wakazi napaona ni pagumu kama wewe.

Ninachozungumzia ni fursa na uwezo wa kutoboa mtu ukiamua kwenda kufanya maisha!

Hivi kapeace kweli unaweza kutoka huko ulipo au mwenzako akaja Bukoba kufanya biashara ya kahawa??

Anyways kama wewe unaichukulia kama sifa sawa. Lakini sisi wengine tulitoka Dar na tukaacha kazi zetu na elimu zetu tukaja Bukoba kuchangamkia fursa baada ya kufanya research vizuri na tunaona mambo yanaenda. Hakuna maana ya kuandika hapa kuwafurahisha watu kisa sifa wakati unakufa kwa njaa. Trust me Bukoba ni palaini mno ukifanya research ukagundua nini hasa cha kufanya.

Siku ukija Bukoba niPm tuonane nikupe live experience

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…