Ukifikiria kiundani hili la kununua maji ya kunywa ni ulimbukeni na ushamba

Sasa chief watu wote tukigoma kunywa maji ya chupa huko viwandani walipoajiriwa ndugu zetu itakuwaje? Vipi kuhusu serikali kukosa kodi? Ili uchumi wa nchi ukue kunatakiwa kuwe na miradi mingi itayotumika kusustain uchumi wa nchi na kutoa ajira umenipata?
 
Maji ya Chupa raha yake unakunywa kwa amani sana hivyo unakunywa mengi.
Yale maji yetu yaliotukuza kuna wakat mpaka uyachunguze uyatafakari sana unless kama yanaandaliwa vyema kabla ya matumizi.
 
chemsha maji weka kwa friji safi
Heri ununue MAJI kuliko Kuchemsha Maji.

Unapochemsha maji unaondoa madini mengi yanayofanya Maji kuwa HAI.

MAJI HAI ni yale Pure water ambayo hayajachemshwa.

USichemshe Maji badala yake Tumia FILTER zipo zinauzwa kuchuja MAJI.

Utapata MAJI SALAMA yasio na kemikali za viwandani na yenye Ubora wake ambao Mungu aliyaleta kwa ajili yetu.

USICHEMSHE MAJI...
 
Ukija kuomba maji kwangu nakwambia usinywe maji, kunywa bia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Wabongo wengi kama mtoa mada ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kuhusu vitu wasivyovifahamu.

Unaweza kukuta mtu kasoma mpaka kawa Profesa Janabi halafu anatoa ushauri wa jumlajumla tu kwa watu wote kwa mambo yanayotakiwa kuwa very individualized.
 
Wewe siyo mimi siwezi kukuiga weye. Acha niwe mshamba hayakuhusu mambo ya wengine
 
Hapa kwangu tangu ninunue water dispenser imekua tabu! Natamani hata niipasue! Nimegombana na wife ila haelewi.

Imagine kwa mwezi nanunua machupa yale ya lita 18 sio chini ya manne (45,000) halafu bili ya maji yote tunayotumia kuogea, kufua, kudeki, kuoshea vyombo, kupikia n.k. ni 27,000 😐
 
Inategemea na ugeni na mazoea ya sehem husika!

Kuna visima huku kwetu ukinywa maji hutoboi full amoeba!!

Tunakinga ya mvua kibao!
 
Kwa wakazi wa Dar ni sahihi kabisa kununua maji ya dukani Kam masafi,uhai,afya n.k maana mabomba ya dawasa yamepita kwenye mitalo na yanavuja na baadhi ya sehemu wanatiririsha kemikali za viwandani.Maji ya dawasa Kwa kunywa siyo salama lakini kama kipato chako ni kidogo endelea kutumia lakini ujue gharama itakuja kwenye kujitibu magonjwa. Mimi mwanzo nilijifanya nunda kunywa maji ya dawasa Kila siku Hadi nilipougua tumbo nikaachana nayo.
 
Naona unataka kupangia watu maisha,
Umasikini usikufanye utake watu kuishi kwenye matakwa yako
 
Dah aisee, Kila mtu mkuu ana maamuzi yake juu ya hela zake na namna yakuishi aina ya maisha ayapendayo.

Siku Moja nilikuwa mahala watu wanakunywa ndani ya ile bucket yao kulikuwa na vinywaji ambavyo kwa hesabu ya haraka ni kama 2mil hivi, huku mimi niko na kinywaji cha 1000 na mfukoni nina change ya 9k.
Nilijisemea tu ya watu hayanihusu, acha niangalia yanayonihusu.

ndani ya viunga ya Basra-Iraq.
 
Hivi ushamba ni kutaka mtazamo wako na mipaka yako ichukuliwe kama sheria za ustaarabu kwa watu wote au ushamba ni kudhani uhalisia wako ndio uhalisia wa watu wengine pasipo kuangalia utofauti wenu wa kimaisha na kimakuzi?.

Sijawahi kuelewa
 
Nilikuwa kijijini Butiama naona watoto wanachota maji katika dimbwi.
Ndio imejaa maji yenye udongo mwing sana.
Nokawauliza" haya maji ya nini?"
Wakasema,haya maji ya kunywa.
Nikawauliza,"Mtakunywa maji haya !?"
Wakasema,"By the time we drink it,the water will be clean"
Yaani haya maji yanawekwa ( ndani ya chungu) for 24 hours au 48 hours,au I don't know for how long ili yatulie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…