Ukifikiria kiundani hili la kununua maji ya kunywa ni ulimbukeni na ushamba

🀣🀣🀣
 
Aibu sana hii.

Inakuwaje mtu hadi anakuwa Profesa ila anashindwa kujua tu kuwa watu wana mahitaji tofauti ya nutrients na kiwango cha mazoezi?

Haya mbona ni mambo ya kushangaza sana!
 
Kama ni mtoto wa karne hii sawa, ila kama ni wale wa zamani haiwezekani...kwanza asilimia kubwa tumekulia vijijini, huduma za maji ni kutoka mitoni, visimani, mabwawani, ziwani, baharini...na maisha yalikuwa yanakwenda safi...ugonjwa ni kichocho tu. Mtu aliyekulia haya maisha asijifanye hapa mjini yeye hawezi kuishi bila maji ya Lita moja kwenye chupaπŸ˜›
 
Mkubwa kuna vitu vya ndani ya nyumba yako, Wewe ndiyo mkuu wa utawala nyumbani mwako, ni kuamua unachoona kinafaa.
 
Me nimeanza kununua maji toka nin miaka 17 mpk sas naanza kuzeeka na sitaacha kununua maji nibaki t na ushamba wng
Kwanz maji ya bomba nikinywa t napata kizungunzugu cha gafla πŸ˜€
 
Aibu sana hii.

Inakuwaje mtu hadi anakuwa Profesa ila anashindwa kujua tu kuwa watu wana mahitaji tofauti ya nutrients na kiwango cha mazoezi?

Haya mbona ni mambo ya kushangaza sana!
Haya matatizo mengine ya kiutamaduni hayamalizwi na usomi wa darasani.

Utamaduni mtu aliokua nao una nguvu sana kuzidi usomi wa darasani alioupata ukubwani.

Ndiyo maana mpaka leo wenye ma degree ni wengi lakini wasomi halisi ni wachache sana.

Kwa sababu usomi, zaidi ya madegree, ni utamaduni.
 
Usomi, zaidi ya madegree ni utamaduni?

Ni utamaduni kivipi mkuu?
 
Unakunywa Maji ya Bomba huo ni ushamba kunywa maji ya kisima mbona Yako poa kabisa
 
Usomi, zaidi ya madegree ni utamaduni?

Ni utamaduni kivipi mkuu?
Utamaduni wa kuwa mdadisi, utamaduni wa kukosa woga, utamaduni wa kuwa mkweli, utamaduni wa kujua mipaka ya ujuzi wako, utamaduni wa kuheshimu michakato na mantiki ya kutafuta ukweli na si kuheshimu vyeo na majina.

Sasa ukilelewa katika utamaduni unaosema mkubwa hakosei tangu ukiwa mtoto, hata unapofundishwa darasani mwalimu akikosea inakuwa vigumu kum challenge na kumsahihisha.

Unapata wasomi waliokariri mambo bila kuyatafakari kwa kina na wao wakipata u Profesa wanaona ni zamu yao ya kukaririsha wengine.

Ndiyo hivi tunakaririshwa kwamba mahitaji ya kila mtu ya maji au chakula ni lazima yawe sawa.

Bila ya kujua kwamba kuna watu inawezekana wanatakiwa wanywe maji yenye pH level fulani tu, au yasiyo nankemikali fulani, au wale chakula kisicho na vitu fulani, au chenye vitu fulani, kwa kulingana na vipimo vya miili yao.

Ukiwa challenge hao ma Profesa Janabi wetu, unaonekana huna adabu.
 
Thank you.
 
Ungefanya utafiti wa hayo maji ya Dawasco katika maeneo yote wanayoyahudumia, mimi ninaishi eneo ambalo hatuwezi kutumia koki za chuma kutokana na maji kuwa na chumvi nyingi sana, pia hauwezi kufulia nguo nyeusi kwani zikikauka chumvi inaonekana, si rahisi kunywa maji haya ya visima vya Dawasco.
 
Maji katika mazingira ya sasa yanachafuliwa kwa njia nyingi, sio lazima uone madhara moja kwa moja kama kuumwa tumbo n.k. kuna kemikali zinazoingia kwenye maji ambayo madhara yake yanaweza kuja kuonekana baadae. Unahitaji kuwa na elimu ya haya mambo kabla ujajiona mjanja na kuita wengine washamba.
 
Kwani utamaduni wa kuchemsha maji umepotelea wapi siku hizi?

Yaani kuna yale maji unaweka kwenye sufuria unachemsha,yanapoa unaweka kwenye friji unakunywa.

MImi kwa kifupi sipendelei maji ya chupa sababu mengine ni feki na yanawekwa kemikali kizembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…