Ninae bro wangu mmoja namkubali sana jamaa Yuko real mbaya alaf Hana maneno mengi Yani.
Sasa wife wake alizingua yani mke ndo alikua chanzo Cha maneno siku hiyo kaenda kazini mke akaamua kumtumia jamaa sms kumwambia kuwa anataka kuondoka arudi kwao kwahyo amwambie sehem atakayo acha ufungo wa nyumba ili yeye aende kwao.
Mwamba akamuelekeza mwanamke sehem ya kuacha funguo, kweli bana jamaa jion karud nyumban kwake hakumkuta mke jamaa akavunga akatulia kimya, kesho yake akapiga simu kwao na mke kuuliza kama ameshafika, mama mkwe akaanza kumuwakia jamaa bila kuuliza chanzo, alafu mama mkwe akamwambia jamaa kuwa haya mambo hayawezi kumalizwa kwenye simu hivyo basi aende ukweni ndo watayaongea hivihivi haliishi na mke hawez kurud kwa jamaa.
Jamaa alicho jibu ni kuwa, Mimi sijamfukuza na chanzo Cha ugomvi ni mtoto wako mwenyewe, kwahiyo Mimi sina muda wa kuja huko kwaajili ya hili jambo, hivyo ni maamuzi yenu tu kuendelea kubaki nae Mimi kilicho nifanya nipige simu ni kutaka kujua tu kama kweli amefika nyumban kwakua umenithibitishia uko nae basi Mimi sina tatzo nipo na amani kwakua hamtaniliza chochote kwakua tayar mpo na mtoto wenu.
Siku zikaenda walivyoona jamaa Yuko kimya wao wenyewe wakampigia simu kumuomba msamaha mke akarudi nyumban mwenyewe na Hadi leo wanamuheshimu jamaa ile mbaya na adabu imeboreshwa kwa hali ya juu, ila mwamba angeenda kutembelea magoti ukweni Hadi leo ingekua migogoro haiishii.