Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE

Anaandika Robert Heriel.

Leo sina mengi ya kusema ndugu yenu. Nimefanya uchunguzi Kama mnavyonifahamu. Nikisemacho ni kweli tupu. Wala sisemi haya Kwa maslahi yangu, au ya mtu yeyote Yule. Nazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa.

Na ujumbe huu usomwe na wangu wote. Mnisikie na kuyafuata ninayoyasema, Kwa maana maneno yangu yamepimwa na kuthibitika kuwa hayana madhara kwenu.

Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).

Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.

Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.

Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.

Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.

Tuna Baba wawili, Baba WA kweli, ndiye MUNGU muumba wa mbingu na Nchi. Na yupo Baba wa uongo ndiye Ibilisi.
Ibilisi Kama Baba mpaka Leo anaamini yupo sahihi, licha ya wengi kuona alikosea. Ubaba ndio upo hivyo. Unapaswa uwe na msimamo. Ikiwa Baba unapaswa kuwa na msimamo basi yakubidi kabla yakufanya maamuzi yoyote lazima utumie akili ili ufanye uchaguzi uliosahihi kwako.

Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.

Utamhesabia siku saba za mwanzo, ikiwa hajakutafuta, utamhesabia siku Saba zingine, ikiwa hatajishusha, mhesabie siku saba zingine mpaka zifike siku 28, asipokuja achana naye kabisa wala usihesabu tena siku.

Ikiwa atarudi kabla hata ya mwezi Kuisha utampokea, kisha utampa barua awapelekee wazazi wake, waandikie na Fidia kadiri utakavyoona kulingana na siku alizokaa, na utoe onyo kuwa kama tabia hii itajitokeza wakati mwingine, barua hiyo itahesabika Kama sehemu ya onyo la mwisho, hivyo akirudi basi mtoto wao utampa talaka.
Ikiwa watashindwa kulipa fidia waambie asirudi wakae naye, au wanaweza kumuozesha na barua hiyo itahesabika Kama talaka kwani sababu utakuwa umeziorodhesha.

Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.

Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe mama Mtawala hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.

Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.

Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.

Ikiwa utakiuka na kukaidi maneno haya basi utajikuta katika taabu ambayo hukupaswa uipitie.

Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.

Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.

Mwanamke akienda kwao Kama hamna hata mtoto mmoja mwambie akae huko huko asirudi. Kama mtakuwa na walau mtoto mmoja kuendelea unaweza mfanyia subra Kama nilivyoeleza hapo juu ya siku 28 yaani kabla mwezi mwingine haujaandama awe karudi, Kama hajarudi fukuza. Wala usimsikilize yeyote.

Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.

Usiponisikiliza;
Kila siku utaenda kujidhalilisha ukweni kuomba omba misamaha Kama Juha,
Kujiliza Liza Kama Paka ukweni ati kisa mwanamke asiyejielewa.
Mwanamke akijua kuwa akikimbia kwao utamfuta atakuwa hata kitu kidogo kakimbia kwao, sijui nini kwao,

Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.

Nafahamu kuna watu watanipinga, Hilo sitalijali na ninalitarajia.
Kuna watu watasema kuwa ninadada au nitazaa watoto wakike, Ndio ni kweli; mashemeji zangu na wakwe zangu WA baadaye utaratibu ni huo nilioutoa.

Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.

Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.

Be a Man not like a man.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Mimi walikuja kumchukua walidhani nitamfuata. Kilichofuata ni talaka nikaletewa niliwagomea mpaka BAKWATA. Yaani mke achukuliwe kwa sababu za kijinga halafu niende kumbembeleza nikasema hapa lazima nilinde heshima yangu.
 
Mimi ni mfano hai wa mtu ambaye mwanamke alinikimbia Akaenda kwao, na mimi ndio nilikosea.
Nikamwambia hata kama nimekosa nenda kwa baba yangu kanishtaki ila kwenu siji kwenye kikao.
Can you believe tulikaa mwaka mzima, mpaka akarudi home nikamwomba msamaha nyumbani kwangu na maisha yakaendelea.
Niliitwa na mchungaji, marafiki, mpaka mama mzazi alitaka niende ukweni nikakataa katakata, nakumbuka baba, mama ,na shangazi mkubwa walienda ukweni ila mimi nilikataa katakata, ilifikia hatua mama yangu alikonda nikamuuliza mama mbona unapungua, mama akaniambia ndoa yako inanipa sana mawazo, nikamwambia mama SIWEZI KUMFUATA MWANAMKE, NEVER EVER.
Sasa mama, mama mkwe na mke wangu wanaelewana sana, tatizo mimi ndio nimekataa kumfuata mwanamke aliyekimbia home kwao.
Wazazi wangu na wazazi wa mke wangu wote wanaishi DSM.
Ila hii tabia, mama yangu alisema nimemuaga babu mzaa baba, alikimbiwa na bibi mzaa baba, akarudi nyumbani sababu babu amezaa nje, ila babu aligoma kumfuata na on top of that akaoa mke mwingine.
Mama yangu akasema wewe ukioa mke mwingine nakupa radhi[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mkuu samahani kwa heshima kabisa nikuambie kuwa uliyoandika ni fasihi andishi. Mtu anaitwa Mke ni habari nyingine tofauti kabisa.

Mwanaume atakayefuata wazo lako kuna mambo matatu yatampata:
1. Sonona
2. Aibu
3. Kudharaulika hata akifariki

Kweli kuishi na mke kunahitaji akili na busara, ila sio ubabe. Nitakuonesha jambo lakujifunza.

Tuseme mfano Magu ni baba sisi ni watoto na Samia ndio alikuwa mama yetu. Kwa mambo yalivyo sasa hali ya familia na historia ya baba yetu ipoje?

Hii dhana yako ndio ile ile ya marehemu baba yetu Magu. Na ukweli mchungu hii dhana haifai kuongozea familia.

Utashangaa wale wanaowacheka na kuwaita wanaume wenzio dhaifu ndoa na familia zao zinateketea alafu wale wanaoitwa dhaifu ndoa na familia zao zinastawi.

Ni hayo tu Mkuu.
Umeongea pumba bro,,, msome vzr tena mleta uzi
 
Kukusaidia Wanawake wanapenda kukaa na wanaume aliowaongelea mleta uzi,

angalia ndoa zinazopelekwa kifilipino nyingi zimevunjika
 
Nilioa ka mwalimu siku moja kakanizingua nikakuta kamejifanyia mgao wa vitu vya ndani kakaenda kupanga! Sjawahi kukatafuta jopo tupo eneo moja kanaomba msamaha.
Unatumia bia gani mkuu, pita hapo grocery ushushie afu nipe namba ya wakala aliyepo karibu
 
MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE

Anaandika Robert Heriel.

Leo sina mengi ya kusema ndugu yenu. Nimefanya uchunguzi Kama mnavyonifahamu. Nikisemacho ni kweli tupu. Wala sisemi haya Kwa maslahi yangu, au ya mtu yeyote Yule. Nazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa.

Na ujumbe huu usomwe na wangu wote. Mnisikie na kuyafuata ninayoyasema, Kwa maana maneno yangu yamepimwa na kuthibitika kuwa hayana madhara kwenu.

Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).

Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.

Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.

Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.

Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.

Tuna Baba wawili, Baba WA kweli, ndiye MUNGU muumba wa mbingu na Nchi. Na yupo Baba wa uongo ndiye Ibilisi.
Ibilisi Kama Baba mpaka Leo anaamini yupo sahihi, licha ya wengi kuona alikosea. Ubaba ndio upo hivyo. Unapaswa uwe na msimamo. Ikiwa Baba unapaswa kuwa na msimamo basi yakubidi kabla yakufanya maamuzi yoyote lazima utumie akili ili ufanye uchaguzi uliosahihi kwako.

Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.

Utamhesabia siku saba za mwanzo, ikiwa hajakutafuta, utamhesabia siku Saba zingine, ikiwa hatajishusha, mhesabie siku saba zingine mpaka zifike siku 28, asipokuja achana naye kabisa wala usihesabu tena siku.

Ikiwa atarudi kabla hata ya mwezi Kuisha utampokea, kisha utampa barua awapelekee wazazi wake, waandikie na Fidia kadiri utakavyoona kulingana na siku alizokaa, na utoe onyo kuwa kama tabia hii itajitokeza wakati mwingine, barua hiyo itahesabika Kama sehemu ya onyo la mwisho, hivyo akirudi basi mtoto wao utampa talaka.
Ikiwa watashindwa kulipa fidia waambie asirudi wakae naye, au wanaweza kumuozesha na barua hiyo itahesabika Kama talaka kwani sababu utakuwa umeziorodhesha.

Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.

Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe mama Mtawala hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.

Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.

Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.

Ikiwa utakiuka na kukaidi maneno haya basi utajikuta katika taabu ambayo hukupaswa uipitie.

Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.

Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.

Mwanamke akienda kwao Kama hamna hata mtoto mmoja mwambie akae huko huko asirudi. Kama mtakuwa na walau mtoto mmoja kuendelea unaweza mfanyia subra Kama nilivyoeleza hapo juu ya siku 28 yaani kabla mwezi mwingine haujaandama awe karudi, Kama hajarudi fukuza. Wala usimsikilize yeyote.

Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.

Usiponisikiliza;
Kila siku utaenda kujidhalilisha ukweni kuomba omba misamaha Kama Juha,
Kujiliza Liza Kama Paka ukweni ati kisa mwanamke asiyejielewa.
Mwanamke akijua kuwa akikimbia kwao utamfuta atakuwa hata kitu kidogo kakimbia kwao, sijui nini kwao,

Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.

Nafahamu kuna watu watanipinga, Hilo sitalijali na ninalitarajia.
Kuna watu watasema kuwa ninadada au nitazaa watoto wakike, Ndio ni kweli; mashemeji zangu na wakwe zangu WA baadaye utaratibu ni huo nilioutoa.

Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.

Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.

Be a Man not like a man.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam

Kwa statement Hii andiko lako ni la kipumbavu kabisa!

“ndiyo maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini”
 
Kila kitu ni ‘timing’ kuna muda wa kusimamia nafasi yako kama mwanaume na pia ku balance nafasi ya mwenzio/mkeo

Ukijifanya ubabe muda wote hautakaa na mwanamke nakuambia, unatakiwa kujua mipaka ya power yako na kiwango cha kutumia

Pia jua familia sio zote zinakubali mtoto wao akigombana na mwenzake arudi kwao sema tu inakuwa hakuna jinsi ya kumfukuza na hasa wakijua kosa ni la mtoto wao na unaweza kuta una watetezi kutoka huko huko familia ya mkeo maana wanamjua mtu wao labda tu na wewe uwe kimeo hasa

Nipo kwenye ndoa karibia miongo 2 , mleta uzi naomba pia uzoefu wako una miaka mingapi ktk ndoa? Labda tuanzie hapo kwanza
Ndoa haina uzoefu mkuu,[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mimi ni mfano hai wa mtu ambaye mwanamke alinikimbia Akaenda kwao, na mimi ndio nilikosea.
Nikamwambia hata kama nimekosa nenda kwa baba yangu kanishtaki ila kwenu siji kwenye kikao.
Can you believe tulikaa mwaka mzima, mpaka akarudi home nikamwomba msamaha nyumbani kwangu na maisha yakaendelea.
Niliitwa na mchungaji, marafiki, mpaka mama mzazi alitaka niende ukweni nikakataa katakata, nakumbuka baba, mama ,na shangazi mkubwa walienda ukweni ila mimi nilikataa katakata, ilifikia hatua mama yangu alikonda nikamuuliza mama mbona unapungua, mama akaniambia ndoa yako inanipa sana mawazo, nikamwambia mama SIWEZI KUMFUATA MWANAMKE, NEVER EVER.
Sasa mama, mama mkwe na mke wangu wanaelewana sana, tatizo mimi ndio nimekataa kumfuata mwanamke aliyekimbia home kwao.
Wazazi wangu na wazazi wa mke wangu wote wanaishi DSM.
Ila hii tabia, mama yangu alisema nimemuaga babu mzaa baba, alikimbiwa na bibi mzaa baba, akarudi nyumbani sababu babu amezaa nje, ila babu aligoma kumfuata na on top of that akaoa mke mwingine.
Mama yangu akasema wewe ukioa mke mwingine nakupa radhi[emoji1][emoji1][emoji1]
Mkuu mwaka mzima si alikua anachakatwa huko aisee .
Anakuletea ngoma kizembe kabisa.
 
Wosia wangu Kwa wanaume wote, akili za kuambiwa changanya na zako.
Ukizima data, ukitoka kijiweni unakuwa wapi? Sasa endekeza ushauri Kama huu halafu ujikute unazeeka mpweke, wenzio wanapiga magoti mafichoni wanazeeka na wake zao.
Umwamba huu ni kwa hisani ya kitoko vodka, baada ya kuzima data ndio watajua hawajui....
 
Yan wife uliendelea kupiga ? Alikua akisikia nyege lazima akutafute? Hahah kama Ni hvo ulitisha mkuu
Ndugu zake wakiongozwa na mashangazi zake ndio walikomaa hakuna kutoka mpaka nimfuate. Mimi nikakataa.
Achana na wamama wa kichaga, ila wale wachaga wahatanisahau.
Ila huwezi amini tukaja tukawa marafiki kiasi kwangu kwenye sherehe zao wananiweka kwenye kamati
 
Inakupasa kutumia akili kubwa ili uweze kuelewa ana maanisha nini,
Ukikulupuka utabadiri sana wanawake
 
Back
Top Bottom