Ukiishi kwa ndugu, rafiki, jirani zingatia haya


mkuu inaonekana huwajui vizuli wanawake au wee ni mtoto from familiar bora ..mkuu haya mambo nayo yanahitaji exposure na practical experience .kwa mfano me ni miongoni mwa wahanga wa ayo mapicha picha ya wanawake , yani wako vizuli na smart sana kwenye acting mbele ya mumewe yani utadhani malaika na hapohapo ndugu wa upande wake hapo ni kama paradiso ndogo ila sasa njoo upande wa ndugu wa kiume ni kama wapo afghanistan ..soo broo nmesoma comments zako baadhi ila kuna sehem unapwaya ila sio kosa lako ni kutokana na haujawahi kupitia izi ngwengwe ..kwa sasa me hata wife afiche vipi yani miss treatment ndogo nakuwa nishamsoma apa anazingua basi namwita pembeni tunaelekezana na mambo yanaenda sawa ..ila wapo wanawake wenye tabia kama zetu wanaume yani hawana mda wakumaindi issue za msosi na vitu vidogo ni bigup sana kwao
 
Mkuu kwa hii comment utakua na roho mbaya sana, mchoyo na mkatili.
Mkuu hujawahi kukaa na hawa ng'ombe! Juzi kati hapa wife ameenda kijijini akakuta litoto la sister wangu lipo lipo tu wala halina issue. Akasema aje nalo town labda litaamka, akaliuliza sasa wewe ungependa usomee kitu gani cha kukupa ujuzi (maana shule lilishindwa), likasema nataka nijifunze ufundi ujenzi. Haya njoo nalo mjini, akalipia kila kitu pale VETA, limeenda siku 2 tu likaanza utoro mara leo liende kesho lisiende. Wife sasa akawa mkali akaanza kuliuliza hiki kitu si wewe ndiye ulisema unataka ujifunze? Kuna mtu alikulazimisha? Hapana! Sasa wife akisema hivi wewe unajitambua kweli? Linaona eti analitukana! Halijafungasha kurudi kwao bila kuaga? Ng'ombe zikae huko huko!
 
Mkuu sio ustaarabu kumuita mtoto wa mwenzio litoto,ng'ombe. Je wewe katika makuzi yako hujawahi kukaa kwa ndugu? Au ndugu hawajawahi kaa kwenu?

Kwa jinsi ulivyomuelezea huyo mtoto ni kama wewe,mkeo na watoto wako ni malaika hamjawahi kwaza wengine. Huenda kwa sasa una pesa lakini angalia isikulevye ukakufuru.
 
Ahsante mwanaume. Kuna comments unasoma unasema kuna wanawake wanataabika; kwa waume zao, wao ni wapitaji tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana kheri anayeitwa mke wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo umenibariki sana. Kuna watu kwao mke ni mashine tu ya kutotoleshea watoto. Si wangeishi tu na hao ndugu zao, kama mke hana umuhimu kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona naona yupo makini tuu... Unajua kuna mambo mengine yanakera sana tena sana. Sa hata ingekua wewe hapo ungemuitaje mtu ajitambui hata huyo mtoto wako akizingua huko kwa ndugu ataitwa hivo hivo
 
Mkuu wanaudhi sana. Mimi nimekaa sana kwa watu mpaka nimekuja kuondoka kwenda kazini natokea kwa watu. Sisi enzi zetu tulikuwa tunajituma mpaka hapo unapokaa wanatamani usiondoke! 12 juu ya alama umeshaamka, pigs maki gari ya mzee, umeshaweka chakula cha kuku kwenye banda, umefagia uwanja. Baada ya hapo unaingia bustanini. Saa 4 huna kazi unapiga chai unashuka town! Hapo tupo Kwa Makupa street. Unashuka town mdogo mdogo tu kwa mguu! Sasa hawa wa sasa hivi unakuta wanampakazia my wife wako kwamba ana roho mbaya! Wanaudhi!!
 
Mbona naona yupo makini tuu... Unajua kuna mambo mengine yanakera sana tena sana. Sa hata ingekua wewe hapo ungemuitaje mtu ajitambui hata huyo mtoto wako akizingua huko kwa ndugu ataitwa hivo hivo
Asante mkuu! Wewe umenielewa! Watu wanafikri tuna roho mbaya kumbe sivyo! Kwangu kwenyewe kulishakuwa kama kituo cha kulelea watoto yatima! Ndugu was pande zote wanapenda kuja kukaa kwangu wakati wa likizo zao. Sasa hao wasiojitambua!!
 
Asante mkuu! Wewe umenielewa! Watu wanafikri tuna roho mbaya kumbe sivyo! Kwangu kwenyewe kulishakuwa kama kituo cha kulelea watoto yatima! Ndugu was pande zote wanapenda kuja kukaa kwangu wakati wa likizo zao. Sasa hao wasiojitambua!!
Yaaani ndo shida ya watoto ambao bado hawajajitambua hii, kuna watu wapo makini sana ukiona kafanya jambo ujue yupo correct hakuna kupendelea wala kuonea. Akizingua wa upande wangu nita mtreat sawa na wa upande wa mwenzanguπŸš«πŸš«β›”
 
nikajiuliza Lengo lako haswa Nini?akanijibu SITAKI MAZOEA ndani kwangu...akizoea ataanza kuparamia vitu kwenye friji na ujuaji mwingi hataki!kijana wa watu kapigwa na butwaa maana ndio kafika kutoka Ikonda.
Nimecheka sana mkuu

Dada kulikuwa na ulazima gani kusema katoka Ikonda..
 
kula mara 3 per day kama wenye nyumba

ile tabia ya kwenda kuzurura na kurudi saa 10 unatafta chai na mkate uliobaki ili upunguze njaa achana nayo itakukost.
""Kula mara 3 per day"" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huruma sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…