Kuishi kwa ndugu, mambo ya kufanya
1. Siku zote amka mapema na ufanye shughuli za kimsaada kwenye mji huo, kwa mfano kufagia, kusafisha mabanda ya kuku n.k. wjatever it is, lakini asubuh na mapema ikukute nje.
2. Jitahidi kutoka nje na kuzunguka kitaa ukitafta mishe ndogo ndogo za kukupa vijisenti ili usipauke kisoro
3. Usiwe na mazoea yaliyopitiliza hasahasa Kwa shemeji au wifi yako. Kaa kwa step wacha kiherehere
4. Ukipata chochote huko duniani, kamwe usirudi mikono mitupu, hata ndizi za buku zinaeza sindikiza wali maharagwe hapo ndani. Always provide some input kuwapunguzia mzigo.
5. Kuwa msafi, kuwa msafi kuwa msafi!
6. Fuata sheria zao, kwa mfano kuwahi kurudi, kusali n.k. kama una sheria zako kazipeleke kwenu, hapo ni kwa watu, wacha kisebengo cha kupanga masharti.
7. Hakikisha wale watoto kina "junia" hawakuzoei, wale wana mambo ya kiwaki unaweza mkata kelebu akatema meno. Jiepushe nao
8. Beki 3 ana mbolea iliopitiliza, ukipanda mbegu nakuapia lazma izae matunda. Mkwepe!
9. Kuwa mstaarabu