Ukiishi na mwenza unayempenda mnaishi kama Watoto

Kwema Wakuu!

Hakuna kitu kizuri kwenye maisha Kama kuishi na mtu mnayependana, Yaani muda wote raha tuu!

Mnaishi Kama Watoto, mnacheza Kama watoto mkiwa pamoja, hakuna Siri. Hakuna chuki.

Mkigombana hamuwezi kukaa masaa mawili mnajikuta mmesahau kuwa mligombana, mnaendelea kupiga Stori na kucheka.

Mnaheshimiana, bila kuogopana, mnakuwa marafiki wa kweli, zaidi ya ndugu.

Hakuna kuviziana na kunyonyana. Mnapiga Umbeya mpaka unawaishia mnaanza kucheza Games, mkichoka mnaenda kuzurura huku na huko na kigari chenu au kama hamna Gari mnapanda Daladala.

Watu wanaopendana hawawezi kuukimbia Umbeya.

Usije msema Mke au mume WA mtu aliyekwenye mahusiano yenye mapenzi ya dhati mbele ya mmoja wao, Umbeya utamfikia huyo unayemsema.

Mapenzi yananguvu kuliko Mauti wahenga walisema, Ogopa watu wanaopendana Kwa dhati yote hao kuwavuruga haiwezekani.

Mapenzi matamu hasa ukimpata mtu sahihi mnayependana.

Wasalamu
Binti Kimoso
 
Umeizungumzia ndoa yangu mkuu, shukran sana since 2006 hadi Leo na five children naona kama jana tu Alhamdulillah
 
Back
Top Bottom