Ukijifunza kwa waliofanikiwa, hawawezi kukupa njia za mafanikio

Ukijifunza kwa waliofanikiwa, hawawezi kukupa njia za mafanikio

Kabisa mkuu, hawatoi kabisa mnyororo mzima namna walivyo fanikiwa, zaidi zaidi wanatupa maneno ya kutufariji tu..
Wazungu wakonwaz sana. Ndio maana wanaandikanmpaka vitabu..very open. And their "rich to be" hustles are very traceable
 
Usisave pesa zako but wekeza zikuzalishie ila pia wekeza katika kitu sahihi na usiogope risk...huo upuuz wa kusave pesa bila kuwekeza niliachaga unless niwe na emergency fund
Inategemea na kiasi ulicho nacho mkuu, ndo utaweza kuwekeza, ila kama zile za nipate niweke kinywani, ni taab Sana...
 
Mimi takwambia ni kwanini matajiri wengi huwa hawasemi ni kwa njia gani wamepata huo utajiri cha kwanza.

Kwanza kabisa nataka muelewe bongo au Africa ni sehem ambazo miundo mbinu za kufanikiwa ni migumu sana zaidi ya mnavofikiri, kwanza kabisa ukianzia kwenye serikali zetu zilivo na sera mbovu za kiuchumi na maendeleo, pili wananchi wenyewe kuwa na akili ya kimaskini toka mwanzo, kumbukeni Utajiri unaanzia kichwani sio bahati nasibu.

Ndio maana toka makampuni ya kubeti yamekuja imekuwa kama ajila maalum kwa vijana, ila kiuhalisia ukiangalia ughaibuji gambling ni kama ugonjwa ambao mtu akiwa nao wanaona amealibikiwa kabisa. Lakini huku ndio michezo tunayotangaziwa kwenye maredio kila siku na mpaka viongozi wetu wa serikali wanashiliki kihamasisha vijana kujiuhusisha na hii kitu.

Kingine ni kuwa kwa sababu ya miundombinu ya upatikanaji mali umekuwa mgumu na wananchi kukosa uzalendo kila kitu tunachofanya inakuwa ni kwa kubeti, maisha ya sasa ni ya kubeti, Mkulima shambani anabeti mazao, anaweka mbegu kisha anabeti mvua kama itakuja ama la na je ikija itakua inayotosha au itazidi na kuleta mafuliko kwenye mazao. Anabeti kwenye mbegu, kwenye madawa hadi mbolea. Mwaka huu mbegu hii nzuri mwakani imebadilika.

Wafanya biashara wanabeti bidhaa hamna research, wafanya kazi wanabeti kazi leo wapo kesho hana uhakika wa kuepo pale, wanafunzi wanabeti masomo hadi kupata kazi, (sasa kama mtu anasoma kwa nusu ya maisha yake halafu anakuja kumalizia nusu ya maisha yake kwa kufanya kazi tofauti na aliyosomea hiyo si kubeti)

Kwahiyo ukija kujumuisha kila kitu unakuta kijana, mpaka anakuja kuona maisha kuna madudu mengi sana anakuwa amepitia.

Em tupitie haya mambo mawili ambayo mimi naona binafsi ndio hufanya ngozi zetu hizi kutosema mali tulitoa wapi. Kwa ufupu ni kusema wanaona Aibu kusema maana njia zinatia aibu.

1. UCHAWI.
Wabongo wengi (asilimia kubwa na sio wote) Mali zao walipata kwa njia za uganga, ugaguzi na uchawi.

Sasa ndio niwaambie tuu uchawi katika utafutaji siku zote imekuwa ndio nguzo kuu Mtanzania, Uchawi wa aina ya kwanza ni wa namna hii hata kama hutaki wew kitumia huo uchawi kuna hizi jamaa zinaitwa chuma ulete ni za kutosha humu mijini. Ko utalazimika kujichanganya na wewe ama la uwe imara sana kiimani. Ukilima wanakuja kuchezea shamba, ukifungua duka wanakuja kuchezea duka, wanachezea kazi, nasikia wanachezea hadi miili ya watu ko kila sehem hukwepi unawakuta.

Uchawi mwingine ni ule wa mara Safisha nyota, mali Waganga wa kupata mali, mara Free masoni, mara nyota, sasa ni ukweli na ipo wazi sasa hivi humu mijini kuna watu mali zao ni za ndagu, unakuta mtu ana nyumba 50 za kupangisha ila anaendesha baiskeri, mara anatembea pekuu, mara njia ni kwa mparange tuu, mara chumba kimoja ndani ya nyumba haingii mtu, mambo kibao.

EM NAMBIE HUYO NDO UNAMUULIZA UMEPATAJE UTAJIRI UNAFIKIRI ATAKWAMBIAJE?

2. WIZI
Mara ya kwanza nishaelezea jinsi miundombinu ilivokuwa mibovu. Sasa kwa wengine waliobaki unabaki ni kuiba tuu, sasa hapa ndo tunaanzia serikalini mpaka huko uswahilini, kila mtu ni mwizi siku hizi, hupati mali bila kuiba. Kila mtu akipata mali utasikia kuna sehem alipiga serikali au mtu fulani, njia ya alali ya kupata hela bongo ni ngumu wadau. Mimi asilimia kubwa ya watu ninaowafaham vijana wamepiga hela najua walikuwa wanafanya kazi sehem fulani wakaiba hela huko ndo hizi wanazo mtaani.

SASA NIAMBIE UNATAKA KUOMBA NAMNA HUYO MTU ALIVOPATA UTAJIRI UNATAKA AKUPE NJIA ZA KUIBA AMA?
Ujumbe mzuri mkuu, wote tunajua hela ni haramu, sasa kama ulipata hasa kwa kichwani 😄😄, Unaonaje na sisi utupe direction ya kufika hapo. Kwenye wizi hapo achana napo labda iwe ndani ya CCM.
 
Wazungu wakonwaz sana. Ndio maana wanaandikanmpaka vitabu..very open. And their "rich to be" hustles are very traceable
Naam, mzungu akifanikiwa lazima aweke documentary yake, namna alivyo toboa maisha. Tuje Africa sasa..
 
Naam, mzungu akifanikiwa lazima aweke documentary yake, namna alivyo toboa maisha. Tuje Africa sasa..
Utasikia "aahh namshukuru Mungu, amenisaidia" imeisha hiyooo

Sema na sisi weusi tatizo husda sana ndio maan watu wanapenda kuwa wasiri.

Ukishajua mtu wapi aliweka mizizi yake ya kutobolea life, badala ujifunze ,mbongo anaenda kukuharibia , shida huamzia hapo watu kuwa wachoyo wa kutoa ramani maana hamkawii kuwawangia
 
Utasikia "aahh namshukuru Mungu, amenisaidia" imeisha hiyooo

Sema na sisi weusi tatizo husda sana ndio maan watu wanapenda kuwa wasiri.

Ukishajua mtu wapi aliweka mizizi yake ya kutobolea life, badala ujifunze ,mbongo anaenda kukuharibia , shida huamzia hapo watu kuwa wachoyo wa kutoa ramani maana hamkawii kuwawangia
Tatizo hasa hapa kwenye husda, mtu amekupa njia ili utoboe lakini unakuwa mtu wa kwanza kuweka hadharani siri na kumharibia maisha yake, Kweli hii ni Moja ya changamoto sisi rangi nyeusi tuliyo nayo
 
Tatizo hasa hapa kwenye husda, mtu amekupa njia ili utoboe lakini unakuwa mtu wa kwanza kuweka hadharani siri na kumharibia maisha yake, Kweli hii ni Moja ya changamoto sisi rangi nyeusi tuliyo nayo
Ndio maana yake. Una act kama una feli vile kumbe ndo unatoboa 😂😂
 
Ndio maana yake. Una act kama una feli vile kumbe ndo unatoboa 😂😂
Hii comment wasione wale walio toboa maisha kwa njia ya panya. Watazidi kuwa na sura ya mbuzi zaidi. Ili kuepusha kushawishiwa na wapelelezi. 😄😄
 
Huyo anajua malengo yake na anachokifanya. Mwenyewe nmejiwekea utaratibu wa kusave 75% ya kila kiasi nikipatacho kwa ajili ya kukua kiuchumi. Kuna vitu najinyima sana lakini fresh ni kwa faida ya future yangu.
Ukitaka kupata 100 ni lazima uanze na 1.
Moja ya kanuni ya Hela ni Spend money save too,usisahau kuenjoy maana muda haupo kukusubiri
 
Back
Top Bottom