Ukikamatwa na Afisa wa LATRA barabarani, tulia kama unanyolewa. Sheria imewapa nguvu sana

Ukikamatwa na Afisa wa LATRA barabarani, tulia kama unanyolewa. Sheria imewapa nguvu sana

Hapo kwenye hawahongeki ndo nimechoka kabisa.
Rushwa Iko kwenye DNA ya mbongo mkuu na hii sio kulaumu viongozi maana ni tatizo linaanzia kwenye familia zetu.
Kiufupi kuibadilisha hii nchi inahitaji kazi ya ziada vinginevyo labda huijui hii nchi vzr
Upo sahihi. Naomba ushuhuda wako, ulishampa au ulisikia mtu kaombwa Rushwa na mfanyakazi wa LATRA? Tujadiliane kwa fact sio hisia.
 
Asante kwa masahihisho but hoja ipo pale pale hayaongwi mamlaka wanaongwa watendaji ambao ni watu na tabia za watu zinajulikana.
Nahisi wewe kazi ya urefa au ujaji huowezi sababu utahukumu kwa hisia

Swali ni dogo, ulishaombwa Rushwa na huyo mfanyakazi wa LATRA au ulishasikia mfakazi wa LATRA kapokea Rushwa?
 
Nahisi wewe kazi ya urefa au ujaji huowezi sababu utahukumu kwa hisia

Swali ni dogo, ulishaombwa Rushwa na huyo mfanyakazi wa LATRA au ulishasikia mfakazi wa LATRA kapokea Rushwa?
Boss, kusema kuwa "Hawaongeki" na ushahidi ikawa ni kutokusikia wakihongwa ndo hisia zenyewe.

Kama ushahidi wa kutohongeka ni kutokusikia basi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hawaongeki, sababu sijawahi sikia wakipokea rushwa.

Ni mechanism gani inatumika na LATRA kuwabana wahusika wakatae dau la hongo watakalopewa regadless ya amount?
 
Wakiwa na shida na Hera lazima watachukua tu hwa watu hawakosagi kosa😀😀
 
Kama ingekuwa kweli unavyosema basi usafiri ungekuwa umeboreshwa sana, daladala zingeacha kujipangia nauli, zingeacha kukatisha ruti, magari ya mikoani yangeacha kutoza nauli isiyo halali mfano nauli ya Moshi na Arusha kwenda au kurudi Dar zinalingana wakati umbali ni tofauti, ukipandia morogoro au kushukia morogoro kwenda au kutoka mikoani unalipa sawa na nauli ya Dar
 
Wakiwa na shida na Hera lazima watachukua tu hwa watu hawakosagi kosa😀😀
Upo sahihi. Lakini hadi sasa taasisi zinazolaumiwa kwa Rushwa, LATRA haimo. Wanaoongoza kwa rushwa ni Polisi.. Latra wanafanya kazi kama Polisi lakini ni Wasafi. Nini siri? Mchujo wao wanaufanyaje? Au mishahara yao mikubwa?
 
LATRA sio Jeshi. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ni Mamlaka ya Serikali ambayo imejizatiti kusimamia sekta ya usafiri wa ardhini, hasa usafirishaji wa mizigo na abiria (mabasi ya mjini, mabasi ya njia ndefu, magari ya mizigo, teksi, pikipiki za magurudumu mawili na pikipiki za magurudumu matatu), usafiri wa Reli na usafiri wa Waya.. Mara nyingi wanaongozana na Polisi.. Ila wao sijawahi kuona wakiwa na bunduki.
Mbona wanafanya kazi kama polisi
 
Hakuna kitu hapo, wamejitengenezea kamradi ka kula rushwa na polisi
Kuna mizani wako na polisi, kuna TRA wako na polisi, kuna hifadhi ya misitu wako na polisi, na hao nyongeza
Si muda mrefu kutakuwa na TBS nao wanakamata magari yasio na viwango
Hapo kuna uhamiaji nao wanasimamishiwa magari na polisi.
 
Back
Top Bottom