PreGE2025 Ukimya wa Mbowe; Je, yupo nyuma ya G55? Kwanini haungi mkono harakati za Lissu na Chadema hivi sasa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Siasa haiko hivyo.Hasa siasa zakiafrika.Endelea kufikiri kwa mihemko hadi utakaposhangazwa.
 
Siasa haiko hivyo.Hasa siasa zakiafrika.Endelea kufikiri kwa mihemko hadi utakaposhangazwa.
 
Chadema hawasusii uchaguzi.

Chadema watazuia uchaguzi.

Kuna tofauti kubwa kati ya kususa na kuzuia.
Nyumbu kama nyinyi mnaweza kuzuia uchaguzi kweli. Labda kama unataka kuvunjwa miguu au kifo kabisa halafu Msaliti Lissu atakimbia kwenda kwa waume zake Ubelgiji anakuacha wewe na familia yako ukiumia.
 
Kwa mbinu gani? Za kujiongelesha humu jf?

Kama kuna kosa kubwa sana watakalo lifanya CCM ni kutumia nguvu kwa watu waliomizwa kwa muda mrefu.

Kuna jambo Watu waliolewa madaraka hawalijui?

Dunia hii sio ya Nchimbi wala Samia wala Lisu wala Mbowe wala matajiri na mafisadi peke yao.

Dunia ni mali ya Mungu na wanadamu wamewekwa tu na wakapewa akili ili waishi kwa haki na kutendeana memo .Jambo usilolitaka usimtendee mwenzako ndio msingi bora wa kuishi Duniani.
Sasa cha ajabu CCM ya Samia wanataka kutendewa mema peke yao na sio wao pia kuwatendea wengine wema na Hali .
Kama Samia anaungangania urais kwa damu na jasho wakati amekaa madarakani miaka 6 ya umakamu na minne ya urais lakini bado anatumia kila hila kuendelea kubakia madarakani ili tu ajinufaishe na watu wake basi ajue wazi kuwa hata wenzake nao wanataka kuongoza nchi hii maana sio mali yake na isitoshe yeye sio mtanganyika .

Kuzuia uchaguzi sio vita wala uhaini maana hakuna mtu anayetaka kumtoa Samia madarakani kwa nguvu wala kwa shinikizo la maandamano .
wale wapumbavu ndani ya Chadema na CCM wanaosema eti ni uhaini ni wajinga kabisa . Lisu anasema pasifanyike uchaguzi kwa sheria hizi ambazo kwa miaka 32 zimewaumiza na kuua watu na kuwabambikizia kesi nyingi sana watu hivyo ni bora uchaguzi usogezwe mbele Samia aendelee kuwa Raisi hata kwa miaka kumi mbele ili Ile nia yake ya kufanya Reform aitekeleze kwa vitendo na uchaguzi ufanyike kwa haki . Hata Samia akishinda kwa haki hakuna atakaye lalamika .Lakini ushindi wa kupiga watu ,kuteka watu ,kuwatisha polisi ili usalama wa taifa na Makada wa CCM waongeze kura halafu wakala akilalamika Msimamizi anawaita polisi kuwa mtoeni huyu nje anafanya fujo kisha polisi wanatekeleza wajibu wao wa kulinda amani maana hawawezi kumuacha mtu aendelee kufanya fujo tu hata kama kuna wizi na kura zinaongozwa .

Kwa hiyo CCM wajihadhari sana .Huu uchaguzi watu wana hasira kubwa na yanayoendelea kuanzia uchaguzi wa mwaka jana kwa hiyo polisi kwa mfano wakaua watu CCM nao watakua hatarini sana nchi itavurugika .

Nimeangalia Polisi mmoja kule Dar es salaam aliyesababisha Bajaji ya mtu ikaungua tena kwa uzembe wa dereva mwenyewe jinsi alivyotaka kupigwa mpaka akakimbia eneo lile kwa kujificha kwenye basi la Magereza lakini bado wananchi walikua na hasira kubwa sana kiasi kwamba kama sio gari la magereza basi angepigwa vibaya tena akiwa hana hata silaha bali anatimiza majukumu yake.

Jamii imeumizwa sana katika chaguzi nyingi . Lisu na heche na Warioba na Kanisa lenye wasomi wengi ,viongozi wengi ,wanafalisafa wengi na waumini wengi duniani kote yaani Kanisa katoliki ambalo kwa miaka mingi limekua likiishauri serkali kwa mifano hai na kwa upendo na tahadhari kubwa ,wote hao wameshauri kuwa pafanyike marekebisho .

Kwa utaratibu uliopo sasa Uchaguzi ni vita maana hali ya maisha ni ngumu sana kwa watu nje ya Siasa na ufisadi. Hakuna mgombea wa CCM atakayetaka kushindwa kwenye nafasi ya ubunge ,udiwani na urais.
Yaani mbunge mshahara mil.18 kwa mwezi halafu akubali kushindwa?
Yaani Samia ameneemesha watu wake na mshahara ambao hata kutajwa hauruhusiwi atakubali kushindwa wakati anaamrisha tu tume imtangaze !
Kule kwenye kata na halmshauri Madiwani wanachotewa mamilioni ya pesa na wakurugenzi kama rushwa ili pesa zipigwe kilaini halafu eti mkurugenzi aache wapinzani washinde na madiwani wa CCM wapoteze fursa .! Kwa sheria hizi haiwezekani kamwe maana wameshaona jinsi walivyoshinda kirahisi kwa kubadili matokeo na kuongeza kura na kuamrisha jeshi la polisi wawapige wanaopinga hujuma hizo maana eti wanafanya fujo kwenye vituo vya kupigia kura .

Utamshindaje ,Nape ,Utamshindaje Waziri anayeweza kumpigia simu mkurugenzi aliyempigania akapata ukurugenzi. Utamshindaje Doto Biteko hata kama ni Mnyarwanda .
Utamshindaje Musukuma kama hata wapa vijana mamilioni ya pesa ukakatwa mapanga mchana kweupe na akahonga polisi unaambiwa umeuawa kwa sababu ya wivu wa mapenzi na sio uchaguzi?

Hivi kweli Mbowe amesahau alivyokosa Kura mpaka kijijini kwake ?
Ama kweli siasa ni biashara kubwa sana kwa wafanya biashara maana wanajua fursa muda wote.

Samia anasema uchaguzi utakua huru na haki lakini anasema ushindi ni lazima . Wanaomzunguka wanasema hata Mungu asipopenda ushindi ni lazima . Lakini Wapumbavu ndani ya Chadema wanasema ni lazima washiriki uchaguzi maana Samia ameruhusu tume huru ambayo haipo kikatiba wala haijafungiwa sheria inayowawajibisha wanaovuruga uchaguzi . Yaani Mkurugenzi anafanya uhuni wa kila namna lakini hachukuliwi hatua bali yule anayesema kuwa kuna hujuma kwenye uchaguzi .

Kuna mchezo hua mara nyingi unafanywa na wapinzani uchwara na wapiga dili . Hasa kwenye vyama vyenye nguvu kama Chadema na ACT.
Anachukua fomu kwa msaada wa CCM halafu anapewa pesa na CCM kwa Kulazimishwa au kwa hiyari yake kisha anajaza fomu kimakosa ili arnguliwe dakika za mwisho halafu mgombea wa CCM abaki na wapinzani dhaifu au abaki peke yake hivyo gharama za kampeni kwake zinapungua .
Huo ndio mchezo wa biashara za wapinzani .
Hata Jimbo la Mwanga kwa Mchome na Hendri Kileo na kule Moshi vijijini hu,Rombo ,Same ,Bumburi , Tanga mjini ,Pangani , Chalinze ,Ilala, Nyamagana, Ilemela ,Srngerema,Iramba ,Singida mjini ,Dodoma mjini ,Nzega , Morogoro mjini ,Gairo ,Kongwa n.k. wapinzani maslahi wamekua wakichukua fomu ili kupandisha bei za kununuliwa . Mara nyingine wanatishwa kuwa wachukue pesa au wasubiri kuenguliwa au hata wakishinda hawata tangazwa .
 
Chini ya kamanda John Mrema wanachadema wote wanaunga mkono maazimio yote yaliyo somwa leo hii tarehe 6/4/2025 na kiongozi wa G55 ndugu John Mrema. Wanachama wote wapo nyuma ya maazinio hayo kwa masilahi ya Chama.
 
Chini ya kamanda John Mrema wanachadema wote wanaunga mkono maazimio yote yaliyo somwa leo hii tarehe 6/4/2025 na kiongozi wa G55 ndugu John Mrema. Wanachama wote wapo nyuma ya maazinio hayo kwa masilahi ya Chama.
Ni muhumi gani huyo anaanzisha chadema ndani ya chadema
 
Chini ya kamanda John Mrema wanachadema wote wanaunga mkono maazimio yote yaliyo somwa leo hii tarehe 6/4/2025 na kiongozi wa G55 ndugu John Mrema. Wanachama wote wapo nyuma ya maazinio hayo kwa masilahi ya Chama.
Uhuni tuu na kuchumia tumbo.
Mrema ni msaliti na HAKIKA HATAFIKA MBALI. Pia wewe ni takataka
 
Wachagaa inaonekana hawajakubali kbs saccos Yao ichukuliwe na lisuu ,
 
Kundi hili lilisama kidete na kumwambia Mwl Nyerere kuwa muungano ni serikali tatu na SI mbili kama ilivyo

Kundi hili lilisheheni watu wenye akili kubwa mno sio Hawa waroho wa madaraka wanotaka hisani ya mama Samia ili kushinda ubunge

Ni dhambi kubwa kina John Mrema Jesca Kishoa na wahuni kama kina Henry Kilewo kujifananisha na kina Mzee Tumtemeke Sanga
Jen.Ulimwengu na wazir mkuu mstaafu John Malecela

Njaa zisitufanye tuharibu brand ya heshima katika historia ya nchi.
 
Wenda ila sidhani , hawa GG 55 ,kwanza hawajui hata maana GG 55 , wale walikua watu wa mfano ,na walilichachafya bunge wakiwa wana ccm sasa hawa wanaharam wapo na jipya lipi chini ya Dunia wapumbavu
 
Mwacheni Mbowe apumzike, simlifanyia figisu mkamuona Lissu wa maana, sasa mtaona cha moto.
 
Mna hela nyingi sana mlizowaibia Watanzania mwaka huu ili kufanya ufedhuli wenu.

Uzuri Watanzania wameshasema wanaenda na Lissu.

Project zenu zote zimefeli na haya mapandikizi yenu mliyoyaweka Chadema.

Wayachukue matakataka yao.

majitu yanayotanguliza matumbo yao huwa ni ya hovyo sana!
 
Mbowe hana tofauti na Lipumba.
 
Wazee wetu nyakati za udogo wetu yapo mazingira ambayo tulikua tunatandikwa viboko dakika chache kabla ya msosi, japo sijui ilikua ni mkakati wa wazee wetu sijui. Baada ya mkong'oto hakuna aliyejali tena chakula. Mwamba amepigwa na chuma kizito kiasi kwamba anahitaji muda wa kutafakari na kuanza maisha mapya. Kibinadamu muachane mzee wa watu apumzike ameifanyia chadema mambo mengi sana. Hivi hamkumbuki mpaka wema sepetu alijiunga chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…