#COVID19 Ukimya wa Serikali dhidi ya chokochoko za Askofu Gwajima, Je imempuuza? Inamuogopa? Anainamlia timing?

Serikali inamwogopa Gwajiboy... simple.

Angekuwa Mwananchi wa kawaida akichochea watu wasichanjwe muda huu angekuwa ndani ya shimo la tewa.
 
Ngoja nikueleze kitu bwana mkubwa, hakuna mwanadamu asiye na haya...halafu hivi vitu vinafanyika public sio mafichoni ushawishi wa gwajima ni mkubwa isitoshe sio mtu wa hovyo ( Ameelimka) na anajua kuitumia elimu yake ipasavyo, anajua kujenga hoja...naweza kusema wanajipanga namna nzuri ya kumwingia bila kuharibu image ya kisiasa isitoshe gwajima yupo upande wao (CCM) kwa hiyo kama watachanga karata zao vibaya watajikuta wanapoteze imani kubwa kwa wananchi ogopa sana binadanu aina ya gwajima anaweza kukusumbua kuliko gaidi. Wako wachache sana, kiufupi jamaa kawazidi maarifa, BBB serikali wakitumia nguvu tu...wameumia[emoji4]
 
Kwani hii ndio chanjo ya kwanza Tanzania? Kwa nafasi yake kama mbunge je hiyo ndio ilikuwa njia sahihi ya kuwasilisha hoja yake?
Tatizo sio chanjo ya ngapi, chanjo zinataratibu zake na zinafahamika hii inatutia wasiwasi kwanza ipo kwenye majaribio, mosi imechukua muda mfupi mno km uitengeneza...lanazima kuwepo na taharuki
 
Mliokuwa mnamsifia kipindi cha Makonda,leo mnamwita mwongo, so kwa hiyo inawezekana hata kipindi cha Makonda alikuwa anasema uongo.

Manake mlimsifia na kumpamba kipindi cha Makonda, leo mnamponda wakati ametumia style ile ile aliyo itumia kwa Makonda. Ila si shangai baadhi ya wabongo, wanapenda kusikiliza na kusifia ujinga na Gwaji anapita mule mule, japokuwa ikitoa hizo personal attacks kwa waziri, still kwenye chanjo bado ana hoja.
 
Anayepotosha NI Waziri na Naibu wake, Ukijaribu kutizama msimamo wa waziri huyu huyu na naibu wake miezi mitano iliyopita ndio kile kile anachokiongea Gwajima kwa sasa (Na aliongea hivyo tangu awali), Kilichotakiwa ni waziri ama naibu waziri wajibu hoja ama maswali yanayokinzana na msimamo wao wa sasa. Wao ndio walituambia mambo ya Chanjo na Dna & rna. Walichokosea ni ku attack personality badala ya kujibu hoja na kutoa elimu.

Naibu waziri alisema chanjo hizi zinaenda kugusa Sijui DNA & RNA pasipo kujua madhara yake, atuambie sasa ni kipi kimebadilika hadi tuziamini tena.
 
Mshana jr kule bungeni nani anayeweza kuwatetea watu wasiotaka kuchanjwa?
Kama ni Spika Tuambie
Kwani msimamo wa Gwajima ulikuwa upi kabla na baada ya kupata Ubunge.
Tumia uganga wako kutubashiria Madhara ya Chanjo kwa miaka ijayo. Wewe unaweza kujuwa tatizo la mtu kabla hata hajafika kwako.
Jibu hoja za Gwajima. JJ wametengeneza busta hakuna majaribio yeyote yaliyofanyika heti inasaidia kupambana na kirusi cha Delt.

Naona kama una support upande wa Serikali .
America wameshndwa Corona na Taliban ni bora Mchina aliyefanikiwa kudhibiti Corona
 
Huyu ni Mshana kweli au kuna mtu ame-hack ID yake?
 
Wewe mbona unampeleka mtoto wako akachanjwe anapozaliwa zaidi ya chanjo 3.. umewahi uliza side effects za hizo chanjo? Na kwanini hujauliza mpaka leo? Au wewe ni miongoni mwa misukule wa Gwajima!?
Kwa sababu hizo chanjo zilishafanyiwa majaribio za muda mfupi, muda wa kati, na muda mrefu
 
Ni kukosa hoja, serikali haina hoja za kumjibu Askofu Gwajima, ndio maana wapo kimya. Tukiwauliza side effects za hiyo chanjo baada ya miaka mi5 ni zipi kwa atakaechomwa na kwa watoto atakaowazaa wanabaki kutoa macho kama panya aliyebanwa na mlango.
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€. Jamaa alihoji hata contents tu za hiyo chanjo macho yanawatoka ndio itakuwa madhara yake?. Kwenye hili la chanjo wamekurupuka.
 
Swali....Je nikichanja nitaambukizwa au sitaambukizwa?
Jibu......utaambukizwa

Swali... kwa nini nichanjwe?
Jibu....wewe sio askofu mwenye karama.

Mshana"....you are exposing yourself, stop it. Chanjo ni ya hiyari.
 
Mkuu mshana hata huyo waziri naye anamajibu ya hovyo tu ndiomaana awali bandiko langu nikakwambia unafeli unapo weka sides, kama mtu alikua kwenye cabinet ya kwanza na sasa amebadilika alitakiwa aseme waziwazi aliamini nini na sasa kwanini amebadilika badala yake anahangaika kuatack personalities, nimesema woote hawako sawa na unaposhadadia kuwa the whole cabinen imebadilisha mwelekeo jiulize ni kwanini? na kwanini sasa wana msimamo mwingine? jamani watanzania sio wajinga wana akili zao mjue. Suala la uasikofu sijui nini halina tija hapa ishu ni mambo anayouliza hayana mashiko? mtu leo unatwambia chanjo ni sumu keshokutwa wewe huyohuyo unabadilika kisa umehamia kwenye nyumba ya mmiliki mwingine unasema haina shida, utaeleweka kweli? Reasoning ya watanzania ni kubwa msifikiri hawajui kitu
 
Swali....Je nikichanja nitaambukizwa au sitaambukizwa?
Jibu......utaambukizwa

Swali... kwa nini nichanjwe?
Jibu....wewe sio askofu mwenye karama.

Mshana"....you are exposing yourself, stop it. Chanjo ni ya hiyari.
Chanjo sio hiari chanjo ni lazima..uhiari wake unakuja na vigezo na masharti
 
Gwajima yupo sahihi kwa upande wake labda uamue kumpinga kwa hoja zingine ameamua ashikilie msimamo wake.
Dorothy amezingua sana huwez kuwa na ndimi mbili eti unabadilika na mazingira.
Kumwamini Gwajiboy ni sawa na kumwamini kayafa aka Jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…