Yaani acha tu.
Unamkuta mwanaume amekukuta unafanya kazi bank, mshahara wako mzuri tu. Anakuonesha mapenzi ya kweli unasema mwanaume si ndo huyu. Hajawahi kugusia kwamba nikikuoa utaacha kazi, hakupangii marafiki wala nini na amekukuta unaishi vizuri na ndugu zako na rafiki zako. Umezoea unajinunulia nguo zako na vitu kama hivyo.
Sasa subiri akuoe. Anaanza. Mi sipendi pale unapofanyia kazi, sasa unamuuliza kwanini kipindi tupo kwenye uchumba hukuwahi kusema kwamba hupendi ofisi yangu na hutamani nifanye kazi hapa ili nijue kama ntaweza kuishi
Na wewe au la. !! Kwanini usubiri unioe ndo uniachishe kazi. Unakuta mtu anakwambia mi staki hiki staki kile na kipindi cha uchumba hakuwahi kusema hivyo vyote.
Kakukuta una gari, una viwanja anataka na yeye majina yake
Yawepo kwenye hivyo viwanja. Hivi huwa shida ni nini? Af wanaume wa hivyi
Wanaenda kutangaza mwanamke msomi mjeuri. Sasa kwanini usingeenda kuoa wa darasa la saba? Mimi
Nna familia nasaidia vitu vidogo umenikuta nawahudumia na hata mia yako sijawahi kukuomba. Unanioa unaanza kunipangia na hata nikiacha kazi unaanza manyanyaso ukiomba hela yaani utaulizwa ya nini. Hadi uje na
Proposal kama unaomba funds UN. Aisee wanaume kwani wanawake huwa wanaomba sana muwaoe? Mbona mnawatreat kama they are desperate in getting married? Umemkuta mtu ana mfumo wake na unajijua we ni mtemi muache tafuta kingedere chako ukipelekeshe