Hamjambo Wote!
Mwanaume were ndiye Mfalme, ndiye Rais, ndiye Mtawala wa Familia yako.
Chochote kitakachotokea kwenye Familia yako wewe ndio mtu wa Kwanza kuwa responsible, na lawama zote zipo Kwako.
Mkeo kutokuwa na adabu, shida ni wewe.
Mkeo kuvaa mavazi ya hovyo, shida ni wewe.
Watoto kutokuwa na Adabu, shida ni were.
Familia kukosa chakula, mavazi, na maisha mazuri, shida ni wewe!
Ni kwamba hujui kutawala, kuna sehemu umeboronga, umefeli, umeshindwa.
Moja ya sababu ya wanaume wengi Kufa Mapema ni pamoja na Kushindwa kutawala himaya yake.
Unakuwa under stress. Umefeli! Mwanaume aliyefeli!
Mfalme aliyeshindwa kutawala miliki yake.
Mungu amekupa Nguvu kuliko mkeo.
Mungu amekupa Akili kuliko Mkeo.
Mungu akakupa utisho kuliko Mkeo.
Yaani mkeo alichokuzidi ni uzuri na urembo tuu ili akufurahishe.
Alafu Leo ushindwe kutawala.
Ukitaka kujua mwenye Makosa ni wewe.
Kwanza, wewe ndiye unatafuta na kuchagua msaidizi wa kukusaidia katika utawala wako.
Hivyo kukosea kuchagua ni dalili ya Kwanza kuwa haukuwa Makini, na hukumwomba Mungu.
Sawa, umeshakosea kuchagua, lakini kushindwa kufanya maamuzi ya kumtengua msaidizi wako utafute mwingine atakayefit ni kiashiria kuwa wewe sio tuu haupo makini Bali pia huna sifa za Watawala, wafalme, Rais.
Kwenye himaya, mfalme ukishaona msaidizi wako hafuati maelekezo yako hutakiwi kufikiri fikiri chakufanya unapiga chini.
Sasa mwanaume mzima kutwa kulalamika oooh! Wanawake wanatesa, wanatesa wanaume wapumbavu.
Yaani msaidizi amsumbue Rais au Mfalme. Kweli?
Sheria ni Moja kwenye utawala.
Lazima msaidizi amtii mtawala. Kama hataki tengua. Tafuta mwingine.
Mwanamke anakupangia ratiba za kukupa mchezo. Ulivyo lijinga na dhaifu unabung'aa bung'aa kama kondoo. Hivi unaelewa maana ya Mwanaume, Mume, Baba. Unaelewa hayo maneno na role zake?
Au mwanamke unayemlisha, unayemuongoza, unayemtawala ati anakupangia pangia vitu kijingajinga, au anakujibu kunyakunya. Kweli?
Huo ni ushoga.
Ukishakuwa mtawala lazima order zako zifuatwe kwa vyovyote iwe kwa diplomasia au kimabavu.
Kama unaona mabavu yatakutia matatizoni tengua, tafuta msichana mwingine mdogo, mbichi kabisa, wamejaa. Kuliko kuwa mwanaume dhaifu.
Mkeo lazima aongee kwa adabu mbele yako. Hiyo hakuna demokrasia.
Iwe umepatia au umekosea. Lazima awe na adabu.
Hakuna kughafilika, sijui amekasirika sijui mihemko, hakuna cha mihemko kwenye utawala.
Ukihemka unawajibishwa!
Ati wanawake hawana adabu. Wanawake wapi! Sijawahi kuona hao wanawake.
Ila nimeona wanaume waoga, wasiojiamini, wasiojua nafasi zao.
Wanaume wanaobembeleza ndoa na mahusiano kama wanawake.
Ati mwanaume anamwambia mkewe arudi nyumbani baada ya mkewe kuondoka kwao tena kwa makosa yake mwenyewe. Mke kakosea na bado anakutisha anaondoka. Kweli?
Jinsi unavyoona serikali inavyoendeshwa ndivyo hivyohivyo tawala za kifamilia zipo hivyo.
Ukimuendekeza mkeo au wanawake watakupanda kichwani.
Ukishindwa kumtawala mkeo hata watoto wako hutowaweza.
Acha nipumzike!
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam