Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Katika sehemu za Watu Wanaojielewa Duniani Mhimili wa Mahakama ndo Kimbilio la Haki kwa Wananchi Wote
Mhimili wa Mahakama ndo Chombo cha kuhakikisha Mamlaka ya Dola (Executive) na Bunge hayakinzani na Sheria pamoja na Haki.
Mhimili wa Mahakama ndo chombo kinachopaswa kuhakikisha mamlaka ya Watawala hayatumiwi ndivyo sivyo.
Ushahidi wa Unyeti huo wa Mhimili wa Mahakama tunauona sasa ambavyo Majaji wa Mahakama za Marekani wanamfundisha Rais Donald Trump namna ya kuheshimu Sheria, Haki na Mipaka yake.
Ushahidi wa Unyeti wa Mhimili wa Mahakama tunauona namna Mahakama ilivyohakikisha Rais wa Korea Kusini anaondolewa madarakani kwa kukiuka Katiba.
Wakati tukiona hayo kwenye mataifa yaliyo mbele kiuchumi huku kwetu hali ni tofauti. Huku kwetu Majaji ni watu wa kujipendekeza kwa Watawala. Wasiojua hata unyeti wa mamlaka yao.
Huku kwetu tunaona kwaya ya Mahakama ikiimba kwenye uzinduzi wa Majengo yao huku wakiinua mabango ya Rais. Watumishi wa Mahakama wanaimba nyimbo za kumsifia Rais alafu alafu majaji wanaaamka na kucheza kuwaunga mkono pamoja na kuwapa fedha.
Kusema kweli Tanzania tupambanie sana Katiba Mpya maana hii Katiba imefanya tuwe na watu wajinga na wapumbavu sana nchini.
Lord Denning
Ukonga.