Ukiona namna Majaji wanavyomnyoosha Trump Marekani alafu ukiwaangalia Majaji wetu wanavyowalamba miguu CCM unasema tu tupate Katiba Mpya

Ukiona namna Majaji wanavyomnyoosha Trump Marekani alafu ukiwaangalia Majaji wetu wanavyowalamba miguu CCM unasema tu tupate Katiba Mpya

Ni kitu Cha ajabu eti muhimili mwingine Tena wenye kiongozi wake kama jaji mkuu, unakuwa una hafla ya uzinduzi wa mahakama badala jaji mkuu ndiyo awe mgeni rasmi eti wanaenda kumtafuta kiongozi wa muhimili mwingine ndo aje kuzindua tukio lao, Sasa hapo unategemea huu muhimili wa mahakama utaweza kusimamia na kuonya pale muhimili mwingine unapokengeuka?
Hapo rules agaisnt bias haiwezi kutekelezeka, mbwa lazima amtii anayempa chakula.
 
Hapo rules agaisnt bias haiwezi kutekelezeka, mbwa lazima amtii anayempa chakula.
Kwaya ya Mahakama inabeba picha ya Samia na kuinyanyua juu kama Wanachama wa CCM alafu kesho mtegemee kupata haki Mahakamani dhidi ya CCM eti.

Hii nchi ni ya kufanyiwa complete overhaul kabisa.
 
Huwezi kuona upuuzi wa namna hii kwenye nchi za Watu wanaojielewa na kujitambua.

Kwenye hafla ya uzinduzi tu wa Majengo yao Kwaya ya Mahakama inaimba mapambio ya Kumsifu Samia kama kwaya ya TOT ya CCM.

Kweli nchi hii ilishajifia. Wakishindwa kina Lissu kuikomboa hakuna budi Jeshi lihamasishwe kuipindua tu tuanze upya.
Loh!
 
Katika sehemu za Watu Wanaojielewa Duniani Mhimili wa Mahakama ndo Kimbilio la Haki kwa Wananchi Wote

Mhimili wa Mahakama ndo Chombo cha kuhakikisha Mamlaka ya Dola (Executive) na Bunge hayakinzani na Sheria pamoja na Haki.

Mhimili wa Mahakama ndo chombo kinachopaswa kuhakikisha mamlaka ya Watawala hayatumiwi ndivyo sivyo.

Ushahidi wa Unyeti huo wa Mhimili wa Mahakama tunauona sasa ambavyo Majaji wa Mahakama za Marekani wanamfundisha Rais Donald Trump namna ya kuheshimu Sheria, Haki na Mipaka yake.

Ushahidi wa Unyeti wa Mhimili wa Mahakama tunauona namna Mahakama ilivyohakikisha Rais wa Korea Kusini anaondolewa madarakani kwa kukiuka Katiba.

Wakati tukiona hayo kwenye mataifa yaliyo mbele kiuchumi huku kwetu hali ni tofauti. Huku kwetu Majaji ni watu wa kujipendekeza kwa Watawala. Wasiojua hata unyeti wa mamlaka yao.

Huku kwetu tunaona kwaya ya Mahakama ikiimba kwenye uzinduzi wa Majengo yao huku wakiinua mabango ya Rais. Watumishi wa Mahakama wanaimba nyimbo za kumsifia Rais alafu alafu majaji wanaaamka na kucheza kuwaunga mkono pamoja na kuwapa fedha.

Kusema kweli Tanzania tupambane sana Katiba Mpya maana hii Katiba imefanya tuwe na watu wajinga na wapumbavu sana nchini.

Lord Denning
Ukonga.

View attachment 3293968View attachment 3293969
Kule kwa wanzenu mfumo ndio unatawala nchi sio kule kwa kusadikika kila ingizo na ngoma yake.
 
Back
Top Bottom