Ukiondoa tabia ya kuwarubuni wabunge wa CHADEMA wahamie CCM, Dkt. Bashiru ni kiongozi makini na mjamaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
 
sio kisiasa ameshiriki kuiba kur na kupunguza upendo wa watanzania kwa chama kazi ya kulinda mali za chama sio ya kisiasa ni ya kihasibu,CCM ni chama cha kisiasa .kauliyko sawa na kusema.ukiondoa tabia ya umalaya na ushirikina mke wangu ni mpishi mzuri sana.
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Ina maana karudisha mali za chama ili pesa ziwanunue hao wabunge wa upinzani?
 
Umeshasema ubovu wake halafu tena unamsifia ni kiongozi makini, upo kama wale wabunge wa CCM wanatoa mapungufu mengi mwishowe wanaunga mkono hoja.
 
Tz tumepoteza dira, hatuendi tulikotamani na tunaongozwa na wasioona faida ktk kujitegemea kwetu kama nchi huru. Wanadhani kuwategemea weupe na kuwatetemekea ndo kutatupa maendeleo na kujitegemea.

Mwl. Nyerere aliandika ktk development&freedom akimaanisha hivi vitu haviachani. Hauwezi ukajiita umeendelea na wakati huna Uhuru wa ndani ya nchi yenu.

Leo wenye mawazo ya kujitegemea wanauwawa na imekuja siasa kali ya kuwaondoa ili kutawaliwa kurudi mezani. Wanawaaminisha eti wanaweza kuwasaidia kuendelea na kusahau kuwa Uhuru kamwe hawatakaa wawape

Kwa sasa ni rahisi mgonjwa wa ukimwi akaishi +50 na akafikisha 100 kuliko kiongozi anayesimamia nchi yake na kujitegemea kuishi japo kwa miaka 10.

Nilishawahi kusema mtu kama Nyerere, JPM, na hata hawa akina Bashiru dunia ya leo si sehemu salama kwao kuishi. Ni sawa ilivyo bahari huwa si sehemu ya kukaa uchafu na badala yake itautema tu. Sasa hawa wema pia dunia si sehemu salama kwao, naturally itakutema tu. Dunia ni sehemu ya maovu na waovu kustawi, ni mahala ambako mabaya yana nguvu sana na kulindwa na ndo maana wezi wa kuku wanaozea jera na wauza sembe wanatamba mitaani. Uharamia ni mkubwa na ukijifanya kuuzuia utaishia kupotea kwa corona ya kisasa.

Machoni hatupendi ubaya na maovu japo rohoni tunahusudu ktk maovu na waovu, wenye wema kwao mbinguni na duniani ni kwetu sie wazee wa mishemishe
 
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Kiukweli chini ya uongozi wa katibu mkuu Dkt. Bashiru, CCM imepata mafanikio makubwa sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Sasa mali za chama zinajulikana bayana na miradi yote ya CCM inajulikana tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa watangulizi wake kuanzia Dkt. Gama hadi kanali Kinana.

Tatizo moja la uongozi wa Bashiru ni ule utaratibu wa kuwarubuni wapinzani na kuja kuwapa vyeo serikalini wakati UVCCM kuna hazina ya kutosha ya wasomi.

Itoshe tu kusema Dr Bashiru bado anafaa kuongoza CCM labda kama vyombo vimemmulika pahala.

Kazi Iendelee!
Wabunge wa chadema waliamua kuondoka sababu walichoshwa natabia za kijinga za kupinga kilakitu.
Waliona dhamira ya kweli ya shujaawetu Hayati Magu wakaamua wenyewe kuunga juhudi mkono bila kushawishiwa na mtu yoyote.
Mkuu, matendo na styl ya uongozi wa Magu ni kichaatu ndio ataweza kupinga kila alichokuwa anafanya.

Tulihitaji rais aina ya Magu ili kurudisha nchi kwenye mstari.
 
katika mambo mama samia kanichefua ni kumpa ubunge huyu mfungwa wa kunyongwa .
 
Kuwanunua wapinzani wako siyo siasa,
mwanasiasa mzuri anawavuta wapinzani wake kwa ujenzi wa hoja na kuisimamia vema serikali.
Uongozi wa Bashiru Ali umebomoa misingi ya umoja wa kitaifa, Bashiru hakuwahi kutamka lolote wakati serikali ya chama chake ilipokuwa inaendesha siasa za kuteka, kutesa na kuua watanzania kwa sababu za kisiasa.
 
Back
Top Bottom