Tz tumepoteza dira, hatuendi tulikotamani na tunaongozwa na wasioona faida ktk kujitegemea kwetu kama nchi huru. Wanadhani kuwategemea weupe na kuwatetemekea ndo kutatupa maendeleo na kujitegemea.
Mwl. Nyerere aliandika ktk development&freedom akimaanisha hivi vitu haviachani. Hauwezi ukajiita umeendelea na wakati huna Uhuru wa ndani ya nchi yenu.
Leo wenye mawazo ya kujitegemea wanauwawa na imekuja siasa kali ya kuwaondoa ili kutawaliwa kurudi mezani. Wanawaaminisha eti wanaweza kuwasaidia kuendelea na kusahau kuwa Uhuru kamwe hawatakaa wawape
Kwa sasa ni rahisi mgonjwa wa ukimwi akaishi +50 na akafikisha 100 kuliko kiongozi anayesimamia nchi yake na kujitegemea kuishi japo kwa miaka 10.
Nilishawahi kusema mtu kama Nyerere, JPM, na hata hawa akina Bashiru dunia ya leo si sehemu salama kwao kuishi. Ni sawa ilivyo bahari huwa si sehemu ya kukaa uchafu na badala yake itautema tu. Sasa hawa wema pia dunia si sehemu salama kwao, naturally itakutema tu. Dunia ni sehemu ya maovu na waovu kustawi, ni mahala ambako mabaya yana nguvu sana na kulindwa na ndo maana wezi wa kuku wanaozea jera na wauza sembe wanatamba mitaani. Uharamia ni mkubwa na ukijifanya kuuzuia utaishia kupotea kwa corona ya kisasa.
Machoni hatupendi ubaya na maovu japo rohoni tunahusudu ktk maovu na waovu, wenye wema kwao mbinguni na duniani ni kwetu sie wazee wa mishemishe