Ukiondoa tabia ya kuwarubuni wabunge wa CHADEMA wahamie CCM, Dkt. Bashiru ni kiongozi makini na mjamaa

Nashukuru KWA kutueleza wapinzan walinunuliwa,ubarikiwe Sana
 
Hilo la kuwapa wapinzani nafas kweny uongoz limetuuma sana uvccm, wakat nia tunayo, uwezo tunao, ari tunayo. Hivi wanatuchukuliaje sisi uvccm lkn?
 
Vipi hapo kaburini ,ULINZI UNAENDELEAJE?MAREHEMU HAJAONESHA DALILI YA KUFUFUKA?
 
Umeshasema ubovu wake halafu tena unamsifia ni kiongozi makini, upo kama wale wabunge wa CCM wanatoa mapungufu mengi mwishowe wanaunga mkono hoja.
Binadamu hakosi kasoro bwashee!
 
Umeshasema ubovu wake halafu tena unamsifia ni kiongozi makini, upo kama wale wabunge wa CCM wanatoa mapungufu mengi mwishowe wanaunga mkono hoja.

Kurubuni wapinzani waunge juhudi sio 'ubovu' kiviiiile.
 
Kinana na Nape walifanya kazi kubwa chama kiliheshimika na siyo huyu mpuuzi anayefanya biashara ya utumwa.
Nilishawahi kusema mtu kama Nyerere, JPM, na hata hawa akina Bashiru dunia ya leo si sehemu salama kwao kuishi. Ni sawa ilivyo bahari huwa si sehemu ya kukaa uchafu na badala yake itautema tu. Sasa hawa wema pia dunia si sehemu salama kwao, naturally itakutema tu. Dunia ni sehemu ya maovu na waovu kustawi, ni mahala ambako mabaya yana nguvu sana na kulindwa na ndo maana wezi wa kuku wanaozea jera na wauza sembe wanatamba mitaani. Uharamia ni mkubwa na ukijifanya kuuzuia utaishia kupotea kwa corona ya kisasa.

Machoni hatupendi ubaya na maovu japo rohoni tunahusudu ktk maovu na waovu, wenye wema kwao mbinguni na duniani ni kwetu sie wazee wa mishemishe
 
Hao wema wako wamelifanya nini cha ajabu? kupoteza watu na kufunga watu ndiyo wema?
 
Ujamaa ni laana
 
CCM hawamtaki kisa eti hakuwa mwanachama kindakindani na hajakulia huko, na alikuwa CUF. Ila jamaa ukimsikiliza anaonekana ni Mzalendo Sana, sema ndo hivo majizi ya CCM hayamtaki
 
Sasa ushasema ana hiyo dosari unadhani atatufaa? Unadhani chama kizima hakuna mtu clean asiye na dosari? We sema unamtetea ili upate ulaji au wewe ni dr Bashiru mwenyewe unajipigia chapuo CCM kama chama taasisi ina watu clean kabisa tatizo hawana connection za vyeo vikubwa maana mfumo baba/mama kanituma umewatawala kinoma.
 
Yaana ccm iww na Mali au vitega uchumi alafu isijue Kama Ina Mali.?

Kwani kwa Sasa bashiru anacheo gani ccm?
 
Kam ni mrubuni basi hafai kuwa kiongozi wa nchi kwa ngazi yoyote.
Akaiongoze familia yake huko.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…