Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Wasalamu!
Humu ndani kunakuwaga na mijadala ya hapa na pale.
Ipo mijadala inayogusa hisia za watu Moja Kwa Moja na kuamsha mihemko ya hasira zinazopelekea matusi na kutoa Lugha chafu na Kali.
Mijadala mtambuka kama ya Kijinsia, kidini, Mila na desturi n..k. ni baadhi ya midajala inayoleta fujo nyingi humu ndani.
Sisi Waandishi ambao wengi wetu kabla ya kuandika tunajua response ya Wasomaji itakavyokuwa tunajibanza kwenye kifuto cha kalamu ya mkaa, tukisubiri Kupata matokeo ambayo hatukuyadhania. Kwetu hii fantasy katika kuandika. Yaani msomaji kuonyesha response ambayo mwandishi au Mtunzi hakuitarajia Kabisa. Fantasy hii ndio hutupa uwezo Waandishi wakujua mambo mengi kuhusu watu wengine.
Tukirudi kwenye Hoja,
Wanawake wengi ukisema Ukweli wowote ule juu Yao. Asilimia kubwa wataona unachuki na wanawake. Hii ipo Dunia nzima.
Wanawake wenyewe Jambo hilo wanalijua fika ndio maana wao wenyewe hushindwa kuambiana Ukweli wakiwa wao kwa wao na hiyo kuwafanya wawe wananafikiana ili kuendeleza mahusiano yao.
Zipo sababu nyingi zinazowafanya wanawake kuwa hivyo walivyo, Sababu kubwa ni KUENDESHA NA MIHEMKO kwani wao ni emotional entity.
Sababu ya pili inatokana na sababu ya kwanza kuwa wao wanapenda upendeleo, kupendwa.
Njia rahisi ya kuonyesha unampenda mwanamke sio kumwambia ukweli kwa Sababu kwao upendo huitafsiri kama kitu kizuri ambacho ni kitamu. Ilhali ukweli sio mtamu ingawaje unaweza kuwa Mzuri.
Ukweli hauhitaji ubunifu ili utokee.
Mwanamke hata akivunja maadili Fulani labda amevaa nguo fupi, au anamienendo isiyofaa, au matendo Mabaya. Hatataka umwambie ukweli.
Ukweli anaoupenda mwanamke ni kumsapoti kwa Jambo Baya analolifanya au alilolifanya.
Mfano.
Inajulikana wazi kuwa kuzaa kabla ya ndoa sio maadili. Ni dalili ya uzinifu, Umalaya,
Sasa namna ya kuutaja ukweli huo kwa mwanamke ni kuusema UKWELI kwa namna ya kumsapoti.
Kama hivi; Ni Bora wewe unafanya Umalaya ukiwa bado hujaolewa kuliko walioolewa na bado wanafanya Umalaya.
Kuliko ungesema, wewe unafanya Umalaya. Malaya ni malaya tuu awe kaolewa au hajaolewa.
Mfano #2
Mwanamke amezalishwa (single mother) katelekezwa.
Utamwambia ukweli hivi; Kuzaa kabla ya ndoa ni vibaya lakini ni Bora wewe haukutoa Mimba.
Hapo hautakuwa na ugomvi na mwanamke.
Ingawaje kosa liko la kuzaa kinyume na maadili.
Katika scenario hizo utagundua kuwa Wanawake hutafuta mtu mwingine WA kupewa lawama zaidi kuliko wao.
Huku wao kwa sehemu kubwa wakijiondoa kwenye makosa.
Wanawake haijalishi wewe ni Jinsia gani, iwe mwanaume au mwanamke lakini kama utamwambia ukweli pasipo kumpa Lawama mtu mwingine na kutompa sapoti huyo mwanamke, lazima akuone unachuki naye.
KWA UPANDE WA WANAUME!
Saikolojia ya wanaume iko tofauti kidogo katika kuambiwa Ukweli
Wanaume kwa asilimia kubwa hawana tatizo lolote wakiambiwa ukweli na wanaume Wenzao.
Ili mradi uwe ukweli
Kwanza kusema ukweli ndio uanaume wenyewe huo.
Wanaume hawasengenyani. Ikitokea wanasengenyana ndio Istihali Umbea inazaliwa.
Mwanamke hawezi kuitwa Mmbea kwa Sababu wao kisaikolojia hawawezi kuambiana UKWELI. Wao kusengenyana ni Jambo la asili. Huwezi mzuia mwanamke asiwe Mmbea.
Hivyo mwanamke Umbea sio sifa mbaya Bali ni ASILI.
Ila kwa mwanaume Umbea ni sifa mbaya kwani ni kinyume cha ASILI.
Mwanaume lazima uwe na uwezo wa kuwa na ujasiri WA kum-face mtu na kumwambia ABCD na black ni black ni white ni white. Bila kuogopa.
Kwa mwanamke sio Lazima ingawaje wapo wanawake wenye baadhi ya hizo hulka za kiume. Wapo!
Mwanaume hapendi kuambiwa UKWELI na Mwanamke.
Ikitokea mwanamke akaanza kuwa Mkweli hiyo ni kiashiria kuwa ni Jasiri, sio mwoga. Na hiyo Moja Kwa Moja wanaume huitafsiri kama ujeuri na Ujuaji.
Kiasili mwanaume hapendi kuonewa huruma, kupendelewa kwani sifa hizo huwa kwa Watu dhaifu na wasio na uanaume ndani Yao.
Ukimwambia mwanamke unamhurumia atafurahia Sana na unaweza kugusa hisia zake. Ni sehemu ya kumdekeza. Kujali. Lakini kumwambia Mwanaume unamhurumia ni kumwambia yeye ni dhaifu asiye na Nguvu zozote.
Kumwambia Mwanaume unampendelea ni kumaanisha umemwambia Hana sifa Wala vigezo stahiki na hiyo humshusha heshima ya ule uanaume wake.
Mwanaume anapenda Heshima. Na heshima ni ishara ya nguvu na Mamlaka.
Sio ajabu watu wenye Mamlaka na nguvu ikiwemo serikali hawapendi wananchi wasema UKWELI kwa sababu huwaona kama wajuaji na wasio na Nidhamu(wasioheshimu Dola)
Mwanamke akimwambia ukweli mwanaume itampasa ajishushe Kwanza na kuchagua chakusema,
Mfano:
Mwanaume kuwa na wanawake wengi wameumbwa hivyo. Ingawaje ni Jambo Baya kwani linaumiza hisia za wenza wao.
Tofauti ni ukweli huu;
Wanaume ni kama mbwa, wanatabia mbaya ya kupandapanda wanawake wengi.
Sentensi zote ni sahihi na Kweli lakini Moja imeonyesha Staha, Hofu, na kuumauma maneno.
Wakati sentensi ya pili ikiwa Kali isiyo na hofu yoyote wala Staha.
Mfano mwingine!
Wanaume ni wababe na makatili Sana.
Hiyo ipo very direct Sana.
Mwanamke akisema hivi ataonekana mkorofi na jeuri ingawaje kwa sehemu kubwa unaweza kuwa ukweli kwa sababu ubabe unaendana na ukatili.
Chakufanya;
1. Jamii ifundishwe kuusema UKWELI wote Bila kujali Nani anafanya
2. Jamii na watu wafundishwe kukubali matokeo ya matendo Yao ili wajifunze na wengine Wapate Somo.
3. Watu wafundishwe kuupokea ukweli hata kama ni mchungu na wabadilike.
Kwa sababu Njia pekee ya kubadilika mi kusema ukweli na kuukubali na kuamua kubadilika.
Kukataa watu kusema UKWELI ni kujaribu kukataa mabadiliko.
Kuzuia watu wasijifunze.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam