Tumia pesa ikuzoee Mnyampaa.
Pesa Ina kanuni na taratibu zake, haijalishi una Elimu Gani ukizifuata, haitakuangusha.
Kama hauna mipango na malengo, utafanya chochote unachomudu Kwa pesa uliyonayo Kwa wakati huo.
Mwisho wa siku, pesa hua haitoshi, ni wewe kuamua ukipata, ifanye vitu gani vya muhimu.
Kuna mtu akiwa na 1M haujui, akiwa na 10k haujui, Yuko vilevile. Lakini mwingine alipata 50k siku hiyo hamnywi maji, ni fujo za hatari. Mtu wa aina hiyo hata umpatie pesa kiasi Gani, atatapanya tu.
Kutafuta na kupata pesa ni jambo Moja, kuitunza ikaongezeka ni kitu kingine kabisa na sio Kila mtu anaweza.