Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

Tupe mbinu mkuu
Mbinu ni kuweka akiba na kuwekeza, lakini haya yote hayawezekani kama hauna nidhamu ya pesa.

Yahitaji ujinyime kweli kweli hata kwa muda ukiwa unaijenga future yako vinginevyo umri utasogea bila mafanikio yeyote.

Kuna kipindi nilikuwa niliingia mkenge ila nashukuru nilishtuka mapema sana vinginevyo ingekuwa maumivu. Marafiki/kampani zinachangia sana kwenye hili, kuna watu ukiambatana nao spending inakuwa kubwa mno, usiposhtuka inakula kwako.
 
Lakini mwingine alipata 50k siku hiyo hamnywi maji, ni fujo za hatari. Mtu wa aina hiyo hata umpatie pesa kiasi Gani, atatapanya tu.
Hivi hii huwa ni hali ya kawaida au kuna namna? Huyu jamaa yangu akishaishiwa anatia huruma sana na kujiapiza hatorudia kutumia pesa vibaya ila akipata pesa kidogo anarudi kule kule, huwa namuonea sana huruma hasa kwa future yake kama ataendelea kuwa hivyo. Hawezi kukaa na hela kabisa.

Kamari iliwahi kunitesa sana nilikuwa siwezi kukaa na hela ila nikafanikiwa kutoka huko nnaweza kuwa na laki kwenye simu na ikakaa hata mwezi mzima sijaigusa jambo ambalo lilikuwa ni mtihani mgumu sana kwangu.
 
Dawa ya hii ni kuwa na mkopo ukiwa Na mkopo kamwe hutatumia pesa ovyo
Uko sahihi.
Mwaka 2014 mdogo angu alipata ajira ya ualimu serikalin. Hana majukum hana starehe na mbaya zaid hana mipango 😂😂 pesa yake haikai ameishiwa na hakuna cha maana kafanya.ukiuliza vipi, hana anachojua. Nikawaza huyu dawa yake inachemka. Nikampa kama miez 6 namu observe. Mwaka 2015 nikamshawishi achukue mkopo bank, kama mil 5, kwakua ananiheshim na kuniamini akakubali, nikamtafutia eneo hapo hapo kibaha, nje kidogo but ni karibu tu na mjini na kazi kwake, akapata eka 3/4 eka kwa milion 2. Nyingine nikanunua tofali 1500. nikamtafuta mshkaji wangu architech aka design raman .Tafuta fundi wakaanza kuweka foundation.
Njkamwambia dogo hapa sasa utajua pa kupelekea pesa kabla hujaanza kuwa na majukum serious. Hii nyumba iishe kama hujaanza kuwa na family.

Alisha maliza mkopo alisha maliza nyumba and she got kids now. Ila akili zilimkaa sawa.. marejesho plus ku push ujemz taratibu.. kuna time alikua ananilaumu sana but now kasahau hayo yote
 
Which mkenge?
Marafiki/kampani, kuchagua marafiki unaoendana nao hasa tabia ni muhimu mno. Kuna jamaa tulikuwa washkaji sana chuo, baada ya chuo tukakutana kitaa. Yule mwamba hela anatumia na anazo, ila nikaja kushtuka mbona nikiwa na jamaa natoboka sana matumizi yanakuwa makubwa sana? Nikaona huu upepo siuwezi nikamuepuka acha nijikune napofikia nisifosi mambo.
 
Hapo unakuta hakuna hata cha maana alichofanya zaidi ya kuhonga wanawake, kwa sababu hakuna kingine kikubwa kinachomaliza pesa ya mwanaume wa kiafrika haraka kama hicho, nilichogundua vijana wengi pesa wanapata ila wanafanyia mambo ya kijinga halafu wanalialia mishahara au faida haitoshi
Kuna ka raha fulani tunapata tukihonga
Hatutaki kukakosa hako ka raha...😁
 
Back
Top Bottom