Ukipewa mke kama mama yako mzazi, utafurahi? Au ukipewa mume kama baba yako mzazi, utashukuru?

Ukipewa mke kama mama yako mzazi, utafurahi? Au ukipewa mume kama baba yako mzazi, utashukuru?

Mume kama baba yangu?😂
Mzee alikua na matukio gani tena 😂😂
Mzee ephen ataniua kwa matukio yule
Laugh Wow GIF by King of Boys.gif
 
Comprehension inaonekana ni changamoto kwako mkuu

Sawa!
Achana nae huyo , Mimi nilishawahi na mpaka hii Leo natamani mke nitakaemuoa awe kitabia , uchapakazi , upendo na uvumilivu kama Mama yangu Mzazi 💯.

Mimi mwenyewe kwa asilimia kubwa sitamani niwe Baba kama Baba yangu Mzazi katika Familia yangu principle zake na mienendo asilimia kubwa sikubali kama ndio miongozo sahihi ya kuishi kifamilia .

Nimejifunza makosa kutoka sehemu zote na nimeyachukua yake mazuri tu , na kujivunia uwepo wao
 
Mke kama mama yangu ningefurahi mno

Mama yangu ni mtu mwema sana sana sana ana upendo na roho nzuri mno

Ana huruma, Utu na moyo mzuri sana pia ni mpambanaji

Ila ningekuwa Manzi then Mume kama Baba yangu hapana kwa kweli Mungu aniepushe nae
 
Kwa wengi wetu mahusiano ya kwanza kuyaona na kuyaishi ni yale ya wazazi wetu. Je, ukipewa mwenza ambaye anafanana kitabia, kiakili, kiuchumi n.k na mzazi wako utafurahi?
  1. Kama jibu ni ndiyo, kwanini?
  2. Kama jibu ni hapana, ungependa awe tofauti kwa namna gani?
View attachment 3604031

Asante na siku njema!
💖💖💖💖
 
Kwa hapo mimi sina chaguo maana mama sikumuona na simfahamu hata kwa sura wala haiba yake na upeo wake.

Kwa sababu nililelewa na bibi, sasa ile mitindo ya uvaaji na mavazi ya wazee ndio nilikua na m force msichana wangu kipindi hiko awe ana vaa hivyo!
Tulisumbuana sana kuhusu uvaaji ule hadi tukaachana.

Kweli wazazi ama walezi wanaacha athari sana kwa mtoto ukubwani na machaguo yake.
 
Swali hili linagusa hisia nzito na mtazamo binafsi wa mtu kuhusu malezi, mahusiano, na tabia za wazazi wake.

Jibu lake hutegemea sana aina ya maisha na mifano ambayo mtu ameiona kutoka kwa wazazi wake tangu utotoni.Kundi la kwanza lingefurahi au kushukuru sana ikiwa wazazi wao walikuwa mfano bora wa mapenzi, uaminifu, na uwajibikaji.

Kupata mwenzi mwenye tabia kama za mzazi aliyetunza familia kwa upendo hurejesha mazingira ya amani na utulivu yaliyozoeleka.Kwa upande mwingine, wapo ambao wangasita au kutofurahi kutokana na mapungufu ya kibinadamu ya wazazi wao.
Ikiwa mzazi alikuwa na tabia ngumu kama hasira, ulevi, au kutowajibika, mtoto hawezi kutamani kukumbana na changamoto hizo katika ndoa yake.Mwisho, utofauti wa nyakati na upekee wa mtu binafsi huchangia mtazamo huu, kwani mifumo ya maisha ya zamani inaweza isifanye kazi sasa.

Watu wengi wanapendelea kupata wenzi wenye utambulisho wao wa kipekee badala ya nakala kamili ya wazazi wao.
 
Kwa wengi wetu mahusiano ya kwanza kuyaona na kuyaishi ni yale ya wazazi wetu. Je, ukipewa mwenza ambaye anafanana kitabia, kiakili, kiuchumi n.k na mzazi wako utafurahi?
  1. Kama jibu ni ndiyo, kwanini?
  2. Kama jibu ni hapana, ungependa awe tofauti kwa namna gani?
View attachment 3604031

Asante na siku njema!
huwa nataman nipamke mwanamke kama mke wa baba angu ambae ni mama angu.
 
Back
Top Bottom