Ukipewa mke kama mama yako mzazi, utafurahi? Au ukipewa mume kama baba yako mzazi, utashukuru?

Ukipewa mke kama mama yako mzazi, utafurahi? Au ukipewa mume kama baba yako mzazi, utashukuru?

Achana nae huyo , Mimi nilishawahi na mpaka hii Leo natamani mke nitakaemuoa awe kitabia , uchapakazi , upendo na uvumilivu kama Mama yangu Mzazi 💯.
Mama zetu 😍 🙌
GIF by UNICEF.gif

Mimi mwenyewe kwa asilimia kubwa sitamani niwe Baba kama Baba yangu Mzazi katika Familia yangu principle zake na mienendo asilimia kubwa sikubali kama ndio miongozo sahihi ya kuishi kifamilia.
Wewe ni mtu wa pili unasema hivi, mimi ni tofauti kidogo, baba yangu ailkua mtu ninayekubaliana naye kwa kila kitu, isipokua kitu kimoja tu, 🍻🍺. Nilishindwa kabisa kuwa kwenye mahusiano na mtu anayetumia pombe!
Nimejifunza makosa kutoka sehemu zote na nimeyachukua yake mazuri tu , na kujivunia uwepo wao
Inapendeza sana mkuu 🫶
 
Mke kama mama yangu ningefurahi mno
Mama yangu ni mtu mwema sana sana sana ana upendo na roho nzuri mno
Ana huruma, Utu na moyo mzuri sana pia ni mpambanaji
Inaonekana ni mtu mzuri sana 😍 heshima kwake 🙌
Ila ningekuwa Manzi then Mume kama Baba yangu hapana kwa kweli Mungu aniepushe nae
Daah wewe pia kama wengine wamesema hivi, ngoja nieendelee kuobserve.
 
Sasa ilikuwaje hakua na mfanano wa tabia unazozipenda kutoka kwa mama yako?
Au uliangalia makebo 😂
Mama yangu ni chaguo la baba yangu ndiyo mpaka nakua sikuwai kushuhudia akimdharau wala kumletea undezi baba amekua akimsapot kila namna ametulea wanae kwa kutokutubagua wala matabaka baina yetu yah namkubali sana mama naye tabia alirithi kutoka kwa mama yake ambaye ni bibi kwangu mpaka uzee wote wapo kwenye ndoa yao na niliona mzee aliwin sana katika ili
 
Kwa hapo mimi sina chaguo maana mama sikumuona na simfahamu hata kwa sura wala haiba yake na upeo wake. Kwa sababu nililelewa na bibi,
Pole sana Elli 😔😔😥
sasa ile mitindo ya uvaaji na mavazi ya wazee ndio nilikua na m force msichana wangu kipindi hiko awe ana vaa hivyo!
Tulisumbuana sana kuhusu uvaaji ule hadi tukaachana.
Haa haaa kama namuona binti wa watu alivyokua ana struggle kuendana na mavazi kama ya bibi.
Kweli wazazi ama walezi wanaacha athari sana kwa mtoto ukubwani na machaguo yake.
Hii ni kweli kabisa 💯
 
Watu hawajaelewa kabisaaa mantiki ya uzi.🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Si unajua ma-great thinkers tena 🚮 🚮 🚮
Kiukweli mzee wangu nilimpenda sana and he was my best friend. Ila mume kama yeye hapana🤣🤣🤣
Mzee alikua na matukio gani tena? so far hakuna mchangiaji hata mmoja ambaye amesifia baba yake 🤔
 
Acha ujinga wako sasa? Maswali gani haya…mamangu alikua chaguo la babangu.
Mimi na babangu tumezaliwa era tofauti, Yes nime-copy vitu vingi kutoka kwake..lakini nope chaguo lake ni chaguo lake.
Nampenda mamangu lakini siwezi kum-date kwanza unapata wapi mawazo kama hayo
jamaa kwani ulishawai kupata jeraha la kichwa labda ?
 
Swali hili linagusa hisia nzito na mtazamo binafsi wa mtu kuhusu malezi, mahusiano, na tabia za wazazi wake.

Jibu lake hutegemea sana aina ya maisha na mifano ambayo mtu ameiona kutoka kwa wazazi wake tangu utotoni.Kundi la kwanza lingefurahi au kushukuru sana ikiwa wazazi wao walikuwa mfano bora wa mapenzi, uaminifu, na uwajibikaji.

Kupata mwenzi mwenye tabia kama za mzazi aliyetunza familia kwa upendo hurejesha mazingira ya amani na utulivu yaliyozoeleka.Kwa upande mwingine, wapo ambao wangasita au kutofurahi kutokana na mapungufu ya kibinadamu ya wazazi wao.
Ikiwa mzazi alikuwa na tabia ngumu kama hasira, ulevi, au kutowajibika, mtoto hawezi kutamani kukumbana na changamoto hizo katika ndoa yake.Mwisho, utofauti wa nyakati na upekee wa mtu binafsi huchangia mtazamo huu, kwani mifumo ya maisha ya zamani inaweza isifanye kazi sasa.
Umeelezea vizuri sana kaka, asante 🙏
Watu wengi wanapendelea kupata wenzi wenye utambulisho wao wa kipekee badala ya nakala kamili ya wazazi wao.
Nickelodeon Point GIF by Paramount+.gif
 
Back
Top Bottom