Hujawasoma vizuri shabiki wa mpira.
Kuna Shabiki,
Kuna mshangiliaji,
Kuna shabiki mshangiliaji.
Shabiki- Huyu unaweza usijue yeye yupo upande gani. Goli likifungwa ametulia tu, akifungwa yeye ametulia tu. Mechi ikiisha anarudi nyumbani anatulia.
Mshangiliaji- Huyu unaweza ukamuuliza hata center forward wao hamjui. Wakati mwingine kama ni mechi za usiku, anasubiria kabisa muda wa mechi ufike. Mechi ikianza anaangalia kidogo anasinzia. Akisikia kelele anaamka kushangilia. Wakati mwingine mechi inaweza kuisha akaanza kukuuliza wametokaje, ile hali naye yumo ukumbini. (Wafuata mkumbo)
Shabiki mshangiliaji- Hawa ndio wanasumbuaga kwenye ukumbi. Kelele mwanzo mwisho. Wanaroho ndogo. Kujinyonga kwao ni kawaida.
Wanaridhika na matokeo hata kama goli ni la mkono wakati timu yake imecheza hovyo.
Wanasifu kila ujinga wa timu.