Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Tuna matatizo mengi sana lakini kubwa NJ kukosa mipango sahihi,watu sahihi wa kutekeza na jamii kukubaliana kwenda kwa.njia hiyo thus why hatutoi nafasi Kwa watu wenye akili kushika hatamu.

Hii jamii yetu imelelewa vibaya ndio matokeo yake hayo Sasa.
 
Sometimes unajiuliza kuna maana gani ya wewe kua na jumba kubwa la ghorofa mithiri ya ikulu ya chamwino na ukitoka nje tu ya geti lako unakutana na barabara ya vumbu imejaa viraka na mashimo kila kona kisa tu wewe umeamua kubinafsisha hela za mradi?

Hospitali poor
Shule poor


Kila kitu poor, lakini wewe uko na hela umeficha uswis sijui UAE, ina kua na maana gani?

Haya yote ni matokeo ya siasa za kifedhuri za Tanzania. Mfumo wetu haujulikani ni ubepari, ubeberu au umwinyi.
 
Niliona Kwenye tv mayor wa mji Mdogo wa California analia machozi Kwasababu tu nyumba na mali za raia wake anaowaongoza zimewaka moto nikagundua Siri ya mafanikio ya nchi za ngozi nyeupe ni uzalendo !
Sijui uzalendo Huwa unapatikanaje lakini pia kati ya matatizo mengi ya jamii yetu ni ubinafsi , yaani jambo la kunufaisha Umma sio kipaombele kushinda jambo binafsi.
 
Nilienda Mwanza Airport Road yaani Jiji Zima linanuka.shombo ya Samaki πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Eti Kanchi kamechoka😁
Nyiee
Hii Nchi inatia aibu,yaani Halmayzimwshindwa kuajiri kampuni za usafi ili Kusafisha mitaro ,Barabara nk.

Lakini pia ilitakiwa kuweka na sheria kwamba Kila mtu ahakikishe mbele ya nyumba au duka lake kiwanja au mtaro unakuwa safi na hatua Kali zichukuliwe mbona pangekuwa safi ila Kwa kuwa hatuna utaratibu wa kujali na kuthamini ndio maana tunaona Bora liende.
 
Wakati huyo mtu anafanya mipango ya kujenga, anaweka tofali, anachimba msingi, anaanza ujenzi..serikali ya mtaa/kijiji inakuwa wapi?

Hata hivyo, kwa nini kila.mara serikali inasubiri watu waanzishe shughuli za kiuchumi ndipo nayo ijiingize?

Hii nchi nadhani ina ombwe la uongozi, viongozi ni taswira tu ya vile sisi tulivyo, hakuna wa kumlaumu mwenzake coz hata mimi/wewe tukipewa nafasi ya kuongoza tutafanya same same...we're indifferent.
 
Michael Jackson alikuja Dar akawa anajishika pua, tukaona huyu anaringa tu.

Kumbe ike harufu tulikuwa tumeizoea tu.
Nakumbuka niko kituo cha Palm Beach nasubiri chai maharage β€œKabibii” niende home mara huyo Michael Jackson anapita katoa kichwa kwenye open roof amevaa mask yake na bado kaziba mdomo na mkono πŸ˜€
 
Wewe jamaa unazingua kwaiyo kweli mtu akitoka AIRPORT anakutana na vumbi your just wale watu waliotokea familia za kimaskini halafu wakapata ela MWALIMU NYERERE AIRPORT iko vizuri acha ujinga na upuuzi wako
 
Barabara ya kwenda Julius Nyerere airport (kakipande kadogo) sijui ina miaka mingapi haiishi. Na ile ndio reception ya nchi yetu. Wageni wote wakitua tu wanapita hapo. Viongozi wote wa nchi including Rais anapita hapo mara kwa mara. Sijui kile kipande kinashindikana nini?! Kwa kweli tunatia aibu!
 
Hilo suala la jamii watu wengi hawalioni au wanalifumbia macho.

Watu watalaumu viongozi, watalaumu katiba, lakini ni wachache sana watakubali kwamba viongozi wanatoka kwenye jamii na katiba (ambayo hata hii ya sasa mazuri yake mengi hatuyafuati) imeandikwa na watu.
 
Wewe jamaa unazingua kwaiyo kweli mtu akitoka AIRPORT anakutana na vumbi your just wale watu waliotokea familia za kimaskini halafu wakapata ela MWALIMU NYERERE AIRPORT iko vizuri acha ujinga na upuuzi wako
Mkuu,

Kuna tofauti kubwa sana. Kuna jamaa mmoja alirudi kutoka New York akatukuta maskani alikuwa anatuambia hizi habari

Alikuwa anasema akishuka kutoka New York anakutana na jua kali, majumba yamepauka, barabara zenye mashimo kibao, nyuso za watu zenye maumivu makubwa.

Sisi tulikuwa tunaona huyu jamaa anatuletea shobo zake za Marekani tu.

Tulipokua wakubwa na kuanza vyuo Marekani na sisi tukaelewa alikuwa anaongelea nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…