Ukisikia kujilipua ndo huku. Ml 60 hisa za CRDB bank, liwalo na liwe!

Ukisikia kujilipua ndo huku. Ml 60 hisa za CRDB bank, liwalo na liwe!

Kuna uzi unaoelezea hizo UTT ni nini? Tujifunze na sisi kidogo.
Mfuko wa pamoja wa uwekezaji. Unanunua vipande ambavyo vinakuwa sehemu ya uwekezaji wako then UTT wanawekeza sehemu zinazotoa faida nzuri ie Bond, Fixed interest, Hisa etc faida inayopatikana mnagawana kwa idadi ya vipande unavyomiliki
 
Wakuu, Maisha bila kujilipua hayaendi. Kifupi kama unanifuatilia nilijichanga UTT AMIS na kuweza kupata kiasi cha 60ml sasa nimetoa hiyo hela yote na kununua hisa za CRDB. Kifupi, liwalo na liwe nikipata sawa na nikikosa sawa. Mungu jaalia. Nitaleta mrejesho baada ya Mwaka kupitia.
Gawanya nusu CRDB nusu UTT
 
Mkuu unaweza elezea kwa ufupi kuhusu UTT AMIS
 
Mwakani mabenki yatafilisika na kufungwa yaliyomengi!

Recession inakuja! Viashiria vinaonekana!
Matumizi yamezidi mapato au nini mkuu,mbona exports umekuwa sana mkuu, Shabiby alisema bungeni kuwa watu wa umma wakiwezeshwa wanaweza kuwa na expenditure itayo justify circle,na Masoko ya mazao yawe konki ili kila kitu kienda,imagine TANAPA wanakusanya na kila kitu kinaondoka na wadhabuni hawalipiwi,inakuwaje
 
Bank kwa sasa zinaface challenges zifuatazo
1.SACCOS zimekuwa nyingi
2.Kausha damu
3.Wakala wa Pesa za simu
4.Wakala wa mifumo mingine ya Pesa mfano NALA
HAYA MAMBO YA HISA KWA KAMPUNI ZA HAPA BONGO SIO YA KUHISI ULAJI KAMA KWA WENZETU AMBAO WAPO WAZI KWENYE FINANCIAL STATEMENTS ZAO
UTT AMIS ina maana kuliko hizo shares za CRDB
 
Wakuu, Maisha bila kujilipua hayaendi. Kifupi kama unanifuatilia nilijichanga UTT AMIS na kuweza kupata kiasi cha 60ml sasa nimetoa hiyo hela yote na kununua hisa za CRDB. Kifupi, liwalo na liwe nikipata sawa na nikikosa sawa. Mungu jaalia. Nitaleta mrejesho baada ya Mwaka kupitia.
Mwee hizi akili mbovu kweli kweli.
Sasa hapo sii bora ungenipa mie hiyo milion 60 ningekurudishia mil 120 ndani ya miezi 3
 
DOnt put all eggs in one basket.....
Ungeweka Half kwenye Hisa na another half kwenye Bonds.
Kwenye hisa utakiwi kuweka hela ambayo ndio hiyo hiyo unayo tu😆 Kama ndio hiyo hiyo Bora uweke kwenye bond japo kichele , hiss inaweza kupanda gafla au ikashuka ghafla na isifikie Tena hicho kiwango ulichonunulia
 
Back
Top Bottom