Ukisikia kujilipua ndo huku. Ml 60 hisa za CRDB bank, liwalo na liwe!

Ukisikia kujilipua ndo huku. Ml 60 hisa za CRDB bank, liwalo na liwe!

Nyumba hazina thamani,kiwanja ndo chenye thamani siku zote. Ndo maana wenye hela wananunua hyo unayo ita nyumba yenye thamani na kuipigq chini na kunyanyua ghorofa. Wekeza kwenye viwanja,ila siyo nyumba ya kupangisha..vinginevyo jenga lodge za biashara
Ukija kwangu unakuja kununua Nyumba yangu mkuu
Hiyo habari ya unafanya nini baada ya kununua hainihusu
 
Mkuu twende sawa kidogo
Twende na hesabu rahisi za makaratasini kama za mamotivesheni spika 😂

Nyumba imegharimu 75M
Kodi kwa mwezi 500,000
Kodi kwa mwaka 6,000,000
Baada ya 10yrs nitakua nimepata 60,000,000 na nyumba yangu ya 75M itakua labda ime double price

Nipe mchanganuo wako kwa 75M baada ya miaka 10 mkuu
Bond,hyo milioni 75 kila mwezi unapata 750,000. Halafu kajisomee kitu kinaitwa compound interest ili uweze kuelewa.
 
Nipe mchanganuo wake basi kwa 75M mkuu

Hapa najifunza pia
Mwaka wa kwanza utakuwa. Utakuwa na
1. 750,000x12 +75M = 84M
2. 840,000x12 +84M = 94M
3. 940,000x12 +94M =105.28M
4. 1,055,000X12 +105.28m =117M
5 . 1,170,000x12 +117 = 131M

Estimation kwenye miaka mitano ya mwisho utakuwa na ongezeko la milioni 70M ukijumlisha na 131 itaingia kwenye 200M
Hiyo hapo ndani ya miaka 5 kwenye return ya 12% per year
 
Mwaka wa kwanza utakuwa. Utakuwa na
1. 750,000x12 +75M = 84M
2. 840,000x12 +84M = 94M
3. 940,000x12 +94M =105.28M
4. 1,055,000X12 +105.28m =117M
5 . 1,170,000x12 +117 = 131M

Hiyo hapo ndani ya miaka 5 kwenye return ya 12% per year
Akasome kuhusu maajabu ya compound interest ama kwa kiswahili huitwa faida jumuishi.
 
Nipe mchanganuo wake basi kwa 75M mkuu

Hapa najifunza pia
Ngoja tukuwekee na picha uelewe vizuri nguvu ya compound interest ama faida jumuishi. Initial capital ni milioni 75 kwa muda wa miaka 10 kwa interest ya 12%
Screenshot_20240911_154650_Compound Interest Calculator.jpg
 
Mfano umepata 100M. Swali la kujiuliza, Kati ya kujenga nyumba ya kupangisha na kununua bonds, kipi bora? Kwangu mimi, likely nitaweka bonds. Maana nyumba ya million Mia moja, utaijenga maeneo ya kawaida sana (not high end plots or locations). Hiyo nyumba itakupa rent ya million kwa mwezi? Highly unlikely! Ila ukinunua bonds zenye returns around 15.49% kwa mwaka, you are guranteed returns ya 15M kila mwaka kwa miaka 20! Na baada ya huo mda unapewa pesa yako. Nadhani pia wengi wetu ni kukosa elimu sahihi ya pesa na uoga wa “kesho itakuwaje”.

Nyumba ya million Mia moja ni nyumba yavkawaida sana na rent zake ndo hizo..unaweza stretch maybe mpaka laki saba. Hapo hujaweka maintenance.

Kwa mtu anayetafuta na asiye taka biashara za kuumiza kichwa, bonds ni better option, kwa mtizamo wangu.
Ishu si nyumba ya million 100 ila ishu ni unaijengea wapi. Kama una kiwanja Ada Estate, Masaki, Oysterbay, Upanga, Mbezi Beach inaweza kuwa investment nzuri ila kwa jengo hilo kulipeleka Kiluvya, Vikindu, Chanika, Chamazi na maeneo ya huko ni hasara tupu.
 
Na ikishuka hata kwa sh 200 ana los ya mil 15 katika hyo mil 60. Ungeweka na hyo point pia
Ila Bond hazinaga hasara 🤣 kwa mtu ambaye fisadi ambaye ameweza kumiliki hata 3 billions anaweza kuishi vizuri sana kwa magawio tu ya Bonds za kila mwisho wa mwaka. Imagine ule 15% ya 3B yani.

Kila mwaka wa hesabu unapofungwa mzigo unaingia wa maana kabisa kitu kama 450M. We umechill tu huna pressure na mtu ni GYM na kula matunda tu. Gari yako moja ya 150M kama Ford au Range Rover unatembelea bila pressure kabisa na mtaji wa biashara ndogo ndogo hukosi.
 
Back
Top Bottom