Ukisikia taarifa za tabia za mwanao kutoka kwa watoto wenzake au majirani zako usipuuze wala usiziamini papo hapo

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Katika malezi ya watoto si kila wakati wote awe mkubwa au mdogo kuna wakati watoto wanafanya mambo wakiwa mbali na wazazi wao na huficha yasijulikane nyumbani.

Ukisikia lawama juu ya mtoto wako au kuwa anatabia ya aina fulani ambayo wewe huijui usikimbilie kumuadhibu/ kumuonya au kumtetea mtoto mbele ya watoa taarifa kuwa mtoto wako hawezi au hajafanya kitendo au hana tabia hiyo bali washukuru watoa taarifa na kisha waahidi kulishughulikia swala hilo.

Usikimbilie kumuonya au kumuadhibu mtoto kwa kuwa hujui ukweli wa jambo hilo kwa kuwa kuna wakati watoto husingiziana au kuhisi na kutoa taarifa ambazo si za kweli ivyo kupekea mtoto kuadhibiwa kimakosa.

Lakini pia usimtetee mtoto au kukataa kuwa mtoto wako hajafanya kwa kuwa watoto huwa wasiri na hufanya vitu vingi kwa siri ivyo ni busara kumuuliza kwa upendo au kufatilia jambo hilo na kujua ukweli kabla ya kuchukua hatua na ikiwa utagundua basi chukua hatua stahiki bila kuathiri saikolojia ya mtoto.

Watoto wanahitaji umakini sana katika kuwafundisha na ili waweze kukua katika maadili mema
 
Katika malezi ya watoto si kila wakati wote awe mkubwa au mdogo kuna wakati watoto wanafanya mambo wakiwa mbali na wazazi wao na huficha yasijulikane nyumbani.

Ukisikia lawama juu ya mtoto wako au kuwa anatabia ya aina fulani ambayo wewe huijui usikimbilie kumuadhibu/
Dah yaani natoka kupokea taarifa kutoka kwa majirani kuhusu mdogo wangu ghafla unaingia ujumbe huu kutoka hapa jamii forum.

Leo ni mara ya tatu napokea taarifa juu ya mdago wangu awapo shuleni yeye ndio huwanunula wanafunzi wenzake hususan mihogo na vitu vingine wanasema hua anaenda na hela 5000 chini ya hapo ni 1000 ilihali mzazi hawezi kumpa hela hiyo.

Ili mtoto huyu asiweze kudhurika ki saikolojia ni kipi cha kufanya ili aache tabia hii ya wizi? maana sasa huu ni wizi wa ndani atavuka mipaka ataibia hadi majirani, binafsi bado sijalichunguza hilo toka kwake.
 
Fimbo zifanye kazi yake
 
Don wa baadae huyo
 
Katika malezi ya watoto si kila wakati wote awe mkubwa au mdogo kuna wakati watoto wanafanya mambo wakiwa mbali na wazazi wao na huficha yasijulikane nyumbani.
Asante sana kwa funzo
 
Back
Top Bottom