Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Katika malezi ya watoto si kila wakati wote awe mkubwa au mdogo kuna wakati watoto wanafanya mambo wakiwa mbali na wazazi wao na huficha yasijulikane nyumbani.
Ukisikia lawama juu ya mtoto wako au kuwa anatabia ya aina fulani ambayo wewe huijui usikimbilie kumuadhibu/ kumuonya au kumtetea mtoto mbele ya watoa taarifa kuwa mtoto wako hawezi au hajafanya kitendo au hana tabia hiyo bali washukuru watoa taarifa na kisha waahidi kulishughulikia swala hilo.
Usikimbilie kumuonya au kumuadhibu mtoto kwa kuwa hujui ukweli wa jambo hilo kwa kuwa kuna wakati watoto husingiziana au kuhisi na kutoa taarifa ambazo si za kweli ivyo kupekea mtoto kuadhibiwa kimakosa.
Lakini pia usimtetee mtoto au kukataa kuwa mtoto wako hajafanya kwa kuwa watoto huwa wasiri na hufanya vitu vingi kwa siri ivyo ni busara kumuuliza kwa upendo au kufatilia jambo hilo na kujua ukweli kabla ya kuchukua hatua na ikiwa utagundua basi chukua hatua stahiki bila kuathiri saikolojia ya mtoto.
Watoto wanahitaji umakini sana katika kuwafundisha na ili waweze kukua katika maadili mema