Watanzania wengi hawawezi kuizungumzia Marekani vizuri kwa sababu wana uvivu wa kiutamaduni na Marekani haitaki uvivu hata kuizungumzia tu.
Marekani ni nchi yenye mambo mengi sana huwezi kuitendea haki kwa kuizungumzia kizembezembe kama hivi.
Picha linaanza hakuna Marekani moja, kuna majimbo 50 yapo tofauti, yana sheria tofauti, chumi yofauti, tamaduni tofauti. Unaambiwa jimbo hili hakuna kodi ya mavazi, kuna kodi ya mapato, jimbo hili hakuna kodi ya mapato, kuna kodi ya mavazi. Hata kuchagua pa kuishi tu ni mahesabu.
Na hata ndani ya majimbo kuna counties tofauti, na katika counties kuna miji tofauti, na hata katika mji mmoja unakuta kwa mfano kuna districts tofauti zina shule zenye sheria tofauti.
Kuna mambo ya rural urban divide, kuna republican democrats divide, kuna coastal and interior divide, kuna liberal conservative divide, kuna all kinds of regional divide north vs south kuna watu wamegawanyika utafikiri bado wanapigana The Civil War. Kuna racial divide weusi weupe na wote katikati yao. Kuna walio na elimu na wasio na elimu. Kuna white collar America na blue collar America.
Hiyo USD $1200 New York City hupati hata chumba kimoja, huko Kansas na Texas vijijini au hata pembeni ya miji mikubwa unaweza kupata nyumba nzima.
Kwa hivyo ukija na generalizations zako za "Marekani hivi" naona mpaka hapo huijui Marekani.