Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Mkuu kila kitu kina gharama zake, hivi umewahi waza mtu anaeishi madale na kufanya kazi poata anapoteza mafuta ya gari kiasi gani kwa mwezi kwenye foleni? Kigamboni hata ukiwa na usafiri na shughuli zako nyingi ni katikati ya jiji, basi huna haja ya kuvuka na gari, kuna parking unalipia 1000-1500 mpaka jioni. Lakini pia Kuna Daraja la nyerere unaweza tumia. Yes ofcourse Kuna changamoto zake hususani katika vivuko kutokana na foleni na changamotoya barabara kwa upande wa darajani, lakini kwasasa Kuna upanuzi wa barabara unaendelea bandarini, ukikamilika mambo yatakuwa bambam.
Practicallity ya mtu kukaa madale ni ishu kama anafanya kazi posta
 
Acha fix wewe. Mimi kuna siku nakaa huko Juliana,samaki samaki Hadi saa Saba nane na ninarudi Kigamboni usiku sina mlinzi geti nafungua mwenyewe. Niliishi miaka mitatu bila geti
Huyo jamaa labda anaongelea wale vibaka wa pale ferry waliokuwa wanawatarget wanachuo na kuwakwapulia lap top. Mimi nimeishi kigamboni Kibada tangu 2011 kiukweli crime rate ipo chini ukilinganisha na maeneo mengine kama tegeta, mbezi luis, mbagala na kwingineko. Bata Kigamboni ni hadi asubuhi na hamna uhalifu, sema tu ni kweli hamna viwanja vikali sana kama huko Masaki, Obey, Mlimani City,Sinza na kwingineko. Ila kwa foleni hatuna stress hizo kabisa hivi karibuni wametuwekea taa na bado naona kama hazina umuhimu sana kwa sasa.
 
Nilikuwa nasubiri nione mwisho ila TAYARII BIASHARA IMESHAANZA HUMU na wameanza kuja inbobo 😁!
 
Hiyo kwa mpalange unaona uzuri sasa, tuulize sisi ambao tumekaa na kusoma huko kuanzia primary , hiyo barabara kabla ya kujengwa ilishapoteza maisha ya watu hapo shule Dovya na pale kwa mama kibonge,
Kipindi hicho pale Azaboi ukikaa huko unaonekana unakaa mkoani [emoji28][emoji28],
Kwa mpalange lilikua eneo la michezo , kuwinda na kula korosho,
Maisha yanaenda kasi sana
Hivi mtu kama huyo unamchukulia serious? Huko Kwa mpalange ingekuwa sehemu ya maana hawa NSSF na NHC si wangeenda kuwekeza huko? Au Aviv Town si wangeenda kuwekeza huko?
 
Dondwe mnaendeleaje huko nina kaeneo huko pia nasikia na umeme umeshaletwa huko swahiba,ni dondoo zaidi kiongozi..!/hofu yangu nasikia huko ni wachawi hawana mfano naomba ukweli ndugu kama hutajali....with lots of thanks.
Mkuu

Mie nimehamia Januari mwaka huu mpaka sasa hakuna aliyeniloga.

Ni kweli REA walishaleta umeme. Hivyo mambo ni poa.
 
Tuwaombe mamlaka husika wapunguze bei ya kivuko cha daraja, haiwezekani bei iwe sawa na bantoni. Bei ikipungua, wengi tutashawishika kuja kuishi huko
Na kwanini tulipe? Kama NSSF washarudisha hela yao serikali ilichukue daraja tuwe tunapita bure kama madaraja mengine hapa nchini.
 
Wapemba wengi wapo Kigamboni ya zamani kuanzia feri hadi kisiwani, miji mipya kama Gezaulole,Kibada,Mikwambe etc sio wengi. Huko waliwahi Wasukuma.
Mkuu kutoka feri mpaka kibada sheli ni km ngapi?
 
Hv kwa mji wa dar ni maeneo gan yaliyo salama kuishi?/ Ambayo hayana vibaka vibaka na wezi? Ukiachilia mbali oSterbay,Upanga,Mbezi,Masaki, na mitaa ya kishua kama hyo. Nazungumzia mitaa ya watu wa kipato cha kati tuh!
 
Shida kweli kweli na ma gharama yani ina maana wewe kuvuka itakulazimu upoteze 90-100K per months kwenda na kurudi kwako! Huu ujinga ndio unanifanya Kigamboni sitaki hata kupasikia
siyo lazima uvuke na kivuko, kuna barabara ya kijichi ns unaweza kuzunguka kongowe
 
Sheli ipi? Kuna oilcom pale junction mji mwema then mji mwema to Kibada kuna sheli kama tatu hivi. Ferry mpaka mji mwema ni kama km 5-6
Duuh..sijakariri hiki kituo cha mafuta but hapo pia kuna junction kushoto barabara la vumbi nyingine ya lami inaendelea
 
Back
Top Bottom