Mkuu shida sisi wabongo tunawaza mahitaji ya miaka 2-5 au labda 10, hatuwazi mbali zaidi. Hivi unajua Size ya jiji la Dar kwa maana ya eneo ni ndogo sana ukilinganisha na majiji mengine makubwa ambayo yana idadi sawa na Dar, lakini kwenye majiji yenye network nzr ya miundombinu, suala la umbali toka point A kwenda B sy issue. Kuna subways, Kuna mabus ya umma, kuna trams n.k, ni vile tu sisi hatutoweza kuwa na underground trains miaka ya karibuni, lakini kwa ukuaji wa Dar na namna technology inavyoongezeka Pamoja na idadi kubwa ya wakazi inavyoongezeka jijini, basi Dar vitu kama train za kupita juu kama za Japenga au Chicago Illinois na trams havitokwepeka na hv kutakuwa na umeme bwerereee, utaweza toka kibamba mpaka ferry ndani ya 30minutes. Dar inakuwa kwa kasi ya ajabu sana, miaka ya mwishoni mwa 80 na mwanzoni mwa 90 hapo tu tabata Kimanga na tabata shule pande za kushoto ndani kidogo bibi yangu alikuwa na manamba ya mpunga na mikorosho. Leo hii, pametapakaa nyumba kote, miaka hyhy, tukikuwa tukienda vua samaki katika mabwawa hapo mikocheni ofisi za sasa za tanesco.