Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Kuna sehemu nyingi karibu na mjini na nyumba bei nafuu.. mfano yombo vituka. Bara bara nzuri lami mpaka mitaani, viwanja vya bata, usalama mzuri, less than 30 minutes to posta. Hakuna foleni popote ukienda town mpaka ufike mataa ya veta napo foleni ndogo.. nyumba za kupanga bei nafuu na mpyaaa nyingii.

Ama chang'ombe pia pako poa sana
chang'ombe ipi mkuu.
 
Ni kwamba hayo maeneo yote Kuna viwanja vya kupima na baadhi vya squatter, nakushauri chukua cha kupima. Kuna makampuni mengi sana yapo huku wanahusika na uuzaji wa viwanja ( wana bei na wana top up kwa original price na commission wanakata) lakini pia Kuna madalali na wenyewe wanatop up na watataka commission hawa unaweza wasomesha na wakakuelewa muhimu upate muaminifu.

Kuna viwanja vipo kwa neighborhood nzr mno vya kupima bei changamshi kdg ila it's worth the price na Kuna viwanja vipo na location matata sana, kiasi unaliona jiji la Dar haswa posta kwa juu hv. Kama ukifanikiwa ukashusha ka ghorofa kako kisha balcony ya master inakuwa na view ya city, inakuwa amazing. Bei inategemea na square mita. Maeneo mazuri ni hayo niliyokutajia hapo juu, kwamba Gezaulole, Kuna Avic town mji mmja wa kishua sana, mikwambe na Kibada.

Kuhusu accessibility, kwasasa kigamboni inajengwa sana, miundo mbinu imeboreshwa na inaendelea kuboreshwa, gari zipo za kumwaga japo si za kufanya kazi mpaka usiku wa manane, life la huku ni la kibepari fln hv, ambapo unaenjoy zaidi ukiwa na usafiri binafsi kama ilivyo miji mingi ya states [emoji2][emoji2]. Huduma za afya zipo za kutosha, agha Khan wana Polyclinic yao pale Shangwe, shule kwa ajili wa watoto zinafumuka kwa kasi ya rocket, ingawa Kuna shule maarufu kama Malaika, HBS, Joyland, Excel etc. Kingine nini, maji? DAWASCO wako katika mpango kama siyo wapo katika utekelezeji wa kuchimba kisima kitakacho kuwa kina samabaza maji kwa wilaya nzima ya Kigamboni, kumbuka maji yatakuwa treated na ya siyo ya chumvi.

Kuhusu usalama, ni kama ilivyo sehemu zingine zozote za makazi mapya, lkn coverall usalama upo wa kutosha. Uzuri wa kigamboni kwangu ni uwepo wa space, yaani hakuna foleni wala mbanano lakin pia ni sehemu ambayo unaweza kaa ukatuliza akili, lakini trust me kama wewe ni mtu wa kupenda fast life kama ya Sinza au kino kigamboni utapachukia sana. Binafsi napenda maisha matulivu, sababu nimwzaliwa na kukulia katika wilaya yenye mchaka mchaka jijini, kigamboni pana nifaa sana, pana life fln hv la ki suburban kama umenaglia series moja unaitwa "Desperate house wives" au " If Loving you is wrong". Mwisho, Kigamboni Kuna sehemu za kula starehe kwa maana ya Bar, ila ni kistaarabu zaidi, zipo za kutosha sana kuanzia silver shark, shamba bar, na zingine nyingi sana.

Kwa kumalizia kama shughuli zako ni mjini kati, basi utapapenda Kigamboni, sababu fasta tu upo town, achana na hao wanaosema pantoni zinazingua, Yes Kuna muda inatokea hvy, lakn si mara zote. Ukiishi kigamboni mara zote utakuwa unaenda kinyume na foleni za mjini
NIMEONA NIWEKE HAPA KWA FAIDA YA WOTE, OTHERWISE una issue ya ndani sana, karibu PM.
.
Mie nataka kilichopimwa pia naogopa madalali Sana Bora kampuni inayojulikana, asante kwa maelezo mazuri
 
Ni wazi wachangiaji wengi wanapasikia tu Kigamboni kama kawaida ya wabongo mpe heading mengine atajazia.
Ila mimi maeneo kama hayo ya kigamboni ndio nayapenda,maisha ya uswahili yalishanishinda.

Sema nini serikali ingekufanya kuwe jiji jipya la kitalii kama vile Eco tlantic ya Lagos kungenoga sana
 
Mie nataka kilichopimwa pia naogopa madalali Sana Bora kampuni inayojulikana, asante kwa maelezo mazuri
Vilivyopimwa pia vipo, ukiwa tayari nijuze ufike manispaa uangalie wapi patakufaa au waweza pata vile viwanja vya makampuni
 
Dea si mtafute hata Lodge au hotel, au mtakua na mda mwingi San wa kuishi?
Ndo home halafu Kuna watu wana tabia ya kupenda kipya kila kitu, akibadili life style anabadili vingi vinavyomzunguka, makazi, usafiri nk
 
Tatizo la huko ni wezi. Kuna wizi sana wa kuvamia usiku huko Kigamboni. Wenye pesa zao wanalazimika kuweka electric fence na makamera.
 
Back
Top Bottom