Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Ukitaka mwisho wako wa Kutembea kutokana na Vibaka na Majambazi kuwa wengi na Kula Kwako Bata ( Kustarehe ) kuwe ni Saa 12 Jioni, basi kaishi Kigamboni.
Afande khamisi kawamaliza sana mkuu kapiga shaba mno majambazi
 
Mimi nimekaa sehemu mbalimbali dar,but kigamboni is the best place hakuna foleni, nyumba zimekaa kwa nafasi Hali nzuri ya hewa n.k nimepanga but next month naanza ujenzi kwenye kiwanja changu kisarawe 2 mwasonga
 
Kigamboni hakuna tofauti na Mbagala, hakuna tofauti na Temeke, hakuna tofauti na Yombo, hakuna tofauti na kiwalani, hakuna tofauti na kongowe.
maeneo hayo yote yanafanana sana
kwa sababu kwa asilimia kubwa yanakaliwa na wakaazi wa mikoa ya kusini.
 
Kinacho nikera Kigamboni ni kuwa kushoto sana na maeneo yote ya Dar.. yani mfano umepata safari ya mkoani inayokubidi ukapande basi Mbezi stand hapo utalazimika kukimbia kimbia asubuhi kama kichaa kuliwahi hilo basi.

Pili kigamboni mambo ya kuvuka maji unalipia, kuvuka daraja unalipia huu ukoloni ni wa kipuuzi sana kwa watu wa kigamboni , sijui watu wa huko wamelikosea nini hili taifa? yani kutoka kwake asubuhi akatafte hela ni lazma atoe hela kuvuka, bado wakati wa kurudi kukitafuta kitanda kuegesha mbavu mtu alipie kwenda kwake,, maana ake ukiwa na gari basi elfu 90 hadi 120 kwa mwezi za kuvukia ni lazima uwe nazo.... stupid
 
Bei ya kiwanja shingapi
 
"kula utumbo wa samaki"[emoji849][emoji849][emoji849][emoji15][emoji15][emoji15]


[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hupajui vizuri kigamboni labda kama uliishia hapo kwa wapemba mwanzoni mwanzoni uswahilini
Wamarekani walitaka kuichukuwa kigamboni yote waipige mabomu wajenge mji wa kisasa, sijui hii project ilikwamia wapi.
 
Kigamboni hakuna tofauti na Mbagala, hakuna tofauti na Temeke, hakuna tofauti na Yombo, hakuna tofauti na kiwalani, hakuna tofauti na kongowe.
maeneo hayo yote yanafanana sana
kwa sababu kwa asilimia kubwa yanakaliwa na wakaazi wa mikoa ya kusini.
Umeshafika Kibada? kama ungefika Kibada huwezi kuropoka haya.

Kibada kuna mashindano ya kujenga nyumba za ghorofa ukiwa na nyumba ya chini utatamani kuuza uhame.
 
Kigamboni ukishuka Panton tu unakutana na maeneo skwata ta kufa mtu.

Eneo Kama kigamboni ingebidi iwe Kama Masaki au ostabay ila kwasababu sisi watanzania hatuwezi kupanga Basi ni balaa tupu.
Mikwambe na Chekechea ni sehemu nzuri sana. Tuna wakaribisha, viwanja hakuna chini ya nusu ekari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…