Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Sijawahi kutamani kuishi huko,ila ni kuzuri kwa sasa hivi ukilinganisha na miaka ya nyuma.Ukitaka kuinjoy maisha ya kule uwe na ka usafiri kako na hela ya mafuta isiwe ya mawazo.Kuna hali flani hivi ya hewa tofauti na sehemu nyingi sana za Dar...
 
Mkuu mkadiriajimajenzi uliishi survey kwa miaka.minne na sasa unapata utelezi kuishi kigamboni toka 2015. Unaongea kama unazungumzia nafsi yangu,, maana na mimi niliishi survey pia nikahamia kigamboni ingawa nako nilihama na sasa niko mkoani Iringa.
Mkuu watu watakuoinga ingawa ukweli ndio huo, kigamboni inafunguka na inaendelea kufunguka, suala la malipo ya kuvuka darajani ni la muda na wimbi lake la upepo wa kisiasa linakuja pengine 2025 itakuwa mwisho, kwani ujio wa daraja la tanzanite unaondoa maana ya msingi kwanini kulipia juvuka kigamboni
 
Pameshangaa shangaa tu utasema mkoa wa wapi sijui!plus hayo makero ya vivuko na daraja nilijuta kupanga huko...
Ila kweli uko sahihi, maana ukizoweya sana Maisha ya Manzese,lazima Kigamboni utaiona Kama Mkoa, maana kuna greenish kwenye maeneo yake, wakati Manzese sizani Kama mti hata mmoja!!!
 
Ivi huwa kuna hospitali kubwa kule? Just in case kuna emergency ya ugonjwa usiku
Kwani hospitals kubwa Dar ziko ngapi? Si Muhimbili na Mlongazila tu? Kuna hospitali ya wilaya tu kama Mwananyamala/Temeke/Ilala. Hakuna kitu kama Aga Khan.
 
Kwani Kona bar alikua anawapata Bure?
 
SIPAPENDI KIGAMBONI.
Unatufokea?!! Sister du huwezi kukaa huko. Hakuna Kidimbwi,Samaki samaki. Wapangaji wengi wa Kigamboni ni wafanyakazi wa makampuni za mafuta,bandari,serikali kabla ya kuhamia Dodoma na wanafuzi wa IFM,TIA,Mwl Nyerere.
 
Kweli aisee.Kila Ukitaka kwenda kwako unaanza kupata mawazo.Napitia darajani au Kwny kivuko.?
 
Unatufokea?!! Sister du huwezi kukaa huko. Hakuna Kidimbwi,Samaki samaki. Wapangaji wengi wa Kigamboni ni wafanyakazi wa makampuni za mafuta na wanafuzi wa IFM,TIA,Mwl Nyerere.
Wewe ni mfanyakazi wa kampuni ya mafuta au mwanafunzi wa IFM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…