Ukitaka kuishi vizuri Dar es Salaam ishi Kigamboni

Vijana wengi Kigamboni wanafanyakazi bandari na wizara za hapo mjini, haizidi nusu saa kufika hapo. Halafu gari kama Passo ni 1,500 tu.
 
Poa Kasie, karibu Kg huku IST,Vanguard na wenzie zinalala nje hamna habari za kuibiwa power window kama huko uzunguni kwenu

Ntakuja vile napenda kula, niandalie jiko la kuchoma/babakyu 😜.

Nna kiwi ya kuchoma choma sea food. Kuanzia pweza ngisi kaa changu kibua kolekole and the team...😋😋😋

Nakuja na kapu langu la sea food toka feri.

Nna P.O. Box huko ila sijarasimisha....

Tukimaliza choma choma tutaenda kupunga upepo, pana vivuli vizuriii usiposinzia basi una upungufu wa usingizi mwilini 😅.
 

Kuna sehemu nyingi karibu na mjini na nyumba bei nafuu.. mfano yombo vituka. Bara bara nzuri lami mpaka mitaani, viwanja vya bata, usalama mzuri, less than 30 minutes to posta. Hakuna foleni popote ukienda town mpaka ufike mataa ya veta napo foleni ndogo.. nyumba za kupanga bei nafuu na mpyaaa nyingii.

Ama chang'ombe pia pako poa sana
 
Karibu sana hio address usiiuze....na zama hizi Dege eco village inamaliziwa tunasogea maeneo hayo kudaka fursa tunaacha wengine wachangamshe vidole kwenye keyboard.
 
Yan mm ndo nafikiria kuhama huku kigamboni nihamie tegeta nyuki maana stress za kuvuka na ma panton haya imenishinda aiseehh. sometimes bora folen kulko ule ujinga wa kuvuka maji
Daraja la kigamboni linaelekea mji gani mbona kuna daraja pamoja na kivuko?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Tuwaombe mamlaka husika wapunguze bei ya kivuko cha daraja, haiwezekani bei iwe sawa na bantoni. Bei ikipungua, wengi tutashawishika kuja kuishi huko
Ngoja hela za watu zirud ndo watapunguza bei
 
Shida ni hayo maji ya chumvi. Ukioga unapauka unatoka na magamba kabisa kama msukule.
Kuna mda fulani nilikaa apartment zile zinazotazamana na chadibwa beach yale maji ya chumvi chumvi yaliniboa sana😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…