Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,
Wana visirani na viburi sijawahi ona ,
Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanba huna la kumfanya
Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga ,
Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt , mchungaji lazima utepete..
Kama Una miadi ya kuonana na demu usiingie kwenye Banda la mbuzi Kwanza mana ni full kunuka kibeberu
wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo mana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania
View attachment 2612382
View attachment 2612275