Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Wakati nakua my brother ilikuwa ikifika zamu yake kuwafungulia bandani asubuhi alikuwa analia kinoma jinsi walivyokuwa wanampelekesha. Walikuwa mbuzi 18 tu ila ikifika zamu yako ya kuwafunga kwenye malisho utaimba alelelee
Ukitaka ucheke we kaa Kwa mbali alaf mwangalie mtu anayewafunga mbuzi jinsi wanavyomhenyesha
 
Vipi ukiwachapa viboko kama ng'ombe wanaskia?
Ngombe unaweza mchapa Kwa mbali unatumia Tu mjeredi , mbuzi kumwadhibu inabd umshike au uwe karbu Naye Sana mana yeye ni easy to maneuver ( ananyumbulika Kwa haraka) sio rahs kumwadhibu Kwa fimbo ya mbali
 
Wakiwa watatu wamefungwa kamba shughuli yake sio ya kitoto , wawili wanaweza amua kukaza unavuta wao wanakurudisha nyuma , alaf mmoja wa tatu yeye anakuvuta kuekekea kwenye mazao , ukute hapo na wewe kuna demu kakuvuruga akili , kuua ni kugusa tuu[emoji16]
Ha ha ha....[emoji1787][emoji1787][emoji119]
 
Umenikumbusha kwa babu yangu,kulikuwa na Mbuzi na Ng'ombe. Sema kuna Ng'ombe madume wakati mwingine walikuwa wanasumbua, wakienda machungani wakati mwingine wanang'ang'ania kwa majike ya watu wengine.Ilikuwa ni kazi kuwafuata na kuwarudisha zizini. Balaa ilikuwa ni siku ya kuhasi Ng'ombe madume ili wakauzwe Dar,kuhasi mbuzi madume haikuwa ngumu sana.Tunachukua nyundo tunagonga pumbu 😢.
 
Tuliletewa jike na mwanae kumbe yule mama alikuwa na mimba akazaa dume tukakampa jina Champion, tulikuwa tunacheza naye sana baba akaamua kumuhasi/asi (hapo sijui lipi sahihi) jamaa alivyokuwa akawa na kiburi na dharau sio ya kawaida majani ya jana hali, hataki kufungwa kamba hivyo mama na dada yake wanafungwa yeye yupo pembeni yao na kulikuwa na mti umepinda vizuri kwamba alikuwa anaweza kuupanda hivyo yeye aliupanda akala majani, majani ya jana wakala mama na dada champion. Tusipomuona inabidi tumuite na anaitika kabisa Mee halafu anakuja mbio Kama mtoto anavyoitwa na akija hata Kama kakuudhi inabidi utabasamu lasivyo anakupiga pembe [emoji3][emoji3][emoji3], baadae akawa ukisahau jiko wazi anaingia anakula chakula chochote atakachokikuta ispokuwa nyama na samaki tu. Baadae akawa kero mtaani anaingia nyumbani kwa watu akikuta wanakula na yeye anataka Kula wakimnyima anapindua meza, hawakuchinjwa wote wala kuuzwa maana watoto tulikataa yote, na mwisho mzee aliwagawa baada ya watoto wote kuondoka nyumba, hadi Sasa bado tunamuongelea champion ambaye mdogo wangu aliinama kumfunga kamba kwa hasira jamaa akarudi nyuma Kama hatua saba hivi akaja speed akampiga kichwa mdogo wangu akaanza kuvuja damu puani na mdomoni Mungu NI mwema dogo alipona, visa NI vingi ila niishie hapa maana mmenikumbusha mbali.
Champion aliupiga mwingi[emoji38]
 
Basi labda ndo maana mimi ni mvumilivu,sasa kweli kuwachunga mbuzi ni ngumu sana,Inatakiwa uwe makini ili wasilishe kwa mashamba ya watu ikawa kesi.Pia kila dakika wakitaka kupitiliza mpaka inabidi ukawanyame. Hata mkiwa mnatoka malishoni,inabidi kuwa makini wasiende kulia ama kushoto.
 
Waliwah kumuaibisha mzee mmoja,walikuwa na kamba afu akawashika kwa pamoja ili akawafunge malishoni,sasa ile tabia yao ya mwingine anaenda huku,mwingine mbele mwingine nyuma mzee akawa amekomaa kuwashikilia ili wasimkimbie alijikuta wamemfunga miguu akakosa balance akajipiga chini
Ningeshangaa huu uzi uishe bila kutoa hii habari ya kuangushwa mtu, uzi ungekuwa na mapungufu [emoji3][emoji3][emoji3],
 
Ngombe unaweza mchapa Kwa mbali unatumia Tu mjeredi , mbuzi kumwadhibu inabd umshike au uwe karbu Naye Sana mana yeye ni easy to maneuver ( ananyumbulika Kwa haraka) sio rahs kumwadhibu Kwa fimbo ya mbali
Ha ha ha....kwa hizi comments huyu mnyama pasua kichwa sana[emoji1]
 
Maumivu yakiisha anaendelea na tabia hiyo tena.

Mbuzi wengi wakorofi tulikuwa tunawavunja pembe, maana target kubwa ya kuwapiga ilikuwa ni kichwani.

Unaweza kuta kwenye kundi la mbuzi, wengine pembe zimevunjika ujue hao ni walafi
Ha ha ha.....akil za mbuzi bhana[emoji38]
 
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,

Wana visirani na viburi sijawahi ona ,

Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanba huna la kumfanya

Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga ,

Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt , mchungaji lazima utepete..

Kama Una miadi ya kuonana na demu usiingie kwenye Banda la mbuzi Kwanza mana ni full kunuka kibeberu

wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo mana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania



View attachment 2612382


View attachment 2612275
Kuna braza wangu anao kma mia hv jamaa kaanza kufanana nao kweli yule jamaa ana uvumilivu na upendo wa mbuzi halafu najiuliza kawezaje kuwafuga mjini!?
 
Umenikumbusha kwa babu yangu,kulikuwa na Mbuzi na Ng'ombe. Sema kuna Ng'ombe madume wakati mwingine walikuwa wanasumbua, wakienda machungani wakati mwingine wanang'ang'ania kwa majike ya watu wengine.Ilikuwa ni kazi kuwafuata na kuwarudisha zizini. Balaa ilikuwa ni siku ya kuhasi Ng'ombe madume ili wakauzwe Dar,kuhasi mbuzi madume haikuwa ngumu sana.Tunachukua nyundo tunagonga pumbu 😢.
Imagine na wewe unagonga pumbu la mbuzi 😁
 
Back
Top Bottom