Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Umenikumbusha miaka fulan nilipokuwa nikienda kijijini kwa babu kusalimia, kuna ng'ombe,mbuzi na panda wa kubebea mizigo.

Nilikua napenda sana kwenda kuchunga, yaani kila atakayekuwa ni zamu yake lazima niende nae, sasa mkiwafungulia kwenda kuchunga inabidi tuwatoe huku tunawakimbiza maana mashamba yapo karibu, yaani ukichunga mbuzi unatakiwa kuwa makini sana ni dk chache wanapotea.

Pale kwa babu kulikua na mbuzi wawili walafi hao ndo huwa wanaanzisha msafara wa kukimbilia shambani, pale tushachinja mbuzi nyingi tu ambazo tulikuwa tunapiga na jiwe kwa bahat mbaya linatua sehem mbaya mbuzi anataka kufa tunachinja

Mbuzi wanauzi sana
 
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,

Wana visirani na viburi sijawahi ona ,

Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanza huna la kumfanya

Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga , wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo mana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania



View attachment 2612382


View attachment 2612275

😀😀😀 na usiombe huyo mbuzi awe na ndevu ni BALAA
 
Mbuzi wasumbufu sana kama unahasira za karibu unaweza kumtwaga jiwe akafa

Mbuzi wakati wa masika sio wasumbufu sana ila wakati wa kiangazi/jua kali wanasumbua sana.
Kwetu kipindi cha masika ndio wasumbufu sana maana wanakuwa kwenye limitation(chini ya ulinzi) machungani na ndipo kipindi penye majani mabichi mazuri ikiwemo mazao.

kipindi cha Kiangazi wanakuwa wanachia maana tunakuwa hatuwalimit, tunawaachia wajichungie kwa kudhurura watakavyo ila ikifika jioni tunaenda kuwapokea(kuwatafuta kwa wale wakorofi kama Mabeberu ambao wanakuwa wanachanganyikana na makundi mengine ya mbuzi), pia mara nyingine huzoea hiyo hali na ikifika jioni wanarudi wenyewe nyumbani.
 
Ao wajinga wanakuaga na kiongoz wao mjinga kuliko wako wao, yani ukiwafungua tu ye anaongoza to njia kwa speed kwenda kula mazao ya watu, dawa yao kamba asa iyo kamba ukute wako wa 3 ndo shughuli inakua ngumu mara wakuvute uku mara uku wakikushinda ujue kesi iyo, mazao ya watu washakula,

Basi nilikua nkiwatuliza kimbelembele na mfunga kamba kwenye lisho alafu namtia fimbo nyingi hadi asira yangu ipoe.... Kuna wakati kimbelembele alikua beberu mkorofi ukimchapa anageuka anaruka anataka akupige, basi nkawa nampa kolabo mwanangu mmoja, nafimbo zetu ndefu mmoja mbele mwingine nyuma akigeuka akupige fimbo akigeuka uku fimbo.....

Ila mikoa mingine noma Mbuzi 50 walipikutika mwezi mmoja, yani mbuzi anapatwa na kichaa, ukimpasua unakuta hadi irizi,

Pia kuna watu noma, waroho ata mbuzi kajifia hadi anaanza kuaribika ila wanakula tu....
Wakiwa watatu wamefungwa kamba shughuli yake sio ya kitoto , wawili wanaweza amua kukaza unavuta wao wanakurudisha nyuma , alaf mmoja wa tatu yeye anakuvuta kuekekea kwenye mazao , ukute hapo na wewe kuna demu kakuvuruga akili , kuua ni kugusa tuu😁
 
Nimewavunja sana hao miguu, mbuzi na ng'ombe nimechunga sana.
Bora ufuge kondoo kuliko hao vicheche.

Wakishazoea kulisha shamba fulani, ukiwa njiani unawaswaga wanatimua mbio hata kama ni umbali wa kilometa 3 mbele. Inabidi ukimbizane nao na lazima utakuta wameshaharibu tu.

Raha ya kufuga hao ni nyama, baba alikuwa akichinja kila wiki mbuzi.

Nb: ukitaka kuwa mfugaji wa hutu "tushenzi" basi uwe na eneo kubwa vinginevyo kila siku utaitwa kwa mwenyekiti au mtendaji kujibu mashitaka ya kuharibu mazao ya watu.😂😂😂
Kama kuna shamba wamelizoea ukiwafungulia tuu ni mwendo wa Usain bolt , kila sku utakuwa unakimbia relay😁
 
Mbuzi wanachangamsha watoto nyumbani [emoji16]
Tuliletewa jike na mwanae kumbe yule mama alikuwa na mimba akazaa dume tukakampa jina Champion, tulikuwa tunacheza naye sana baba akaamua kumuhasi/asi (hapo sijui lipi sahihi) jamaa alivyokuwa akawa na kiburi na dharau sio ya kawaida majani ya jana hali, hataki kufungwa kamba hivyo mama na dada yake wanafungwa yeye yupo pembeni yao na kulikuwa na mti umepinda vizuri kwamba alikuwa anaweza kuupanda hivyo yeye aliupanda akala majani, majani ya jana wakala mama na dada champion. Tusipomuona inabidi tumuite na anaitika kabisa Mee halafu anakuja mbio Kama mtoto anavyoitwa na akija hata Kama kakuudhi inabidi utabasamu lasivyo anakupiga pembe [emoji3][emoji3][emoji3], baadae akawa ukisahau jiko wazi anaingia anakula chakula chochote atakachokikuta ispokuwa nyama na samaki tu. Baadae akawa kero mtaani anaingia nyumbani kwa watu akikuta wanakula na yeye anataka Kula wakimnyima anapindua meza, hawakuchinjwa wote wala kuuzwa maana watoto tulikataa yote, na mwisho mzee aliwagawa baada ya watoto wote kuondoka nyumba, hadi Sasa bado tunamuongelea champion ambaye mdogo wangu aliinama kumfunga kamba kwa hasira jamaa akarudi nyuma Kama hatua saba hivi akaja speed akampiga kichwa mdogo wangu akaanza kuvuja damu puani na mdomoni Mungu NI mwema dogo alipona, visa NI vingi ila niishie hapa maana mmenikumbusha mbali.
 
Samahani:
Hivi ushawahi funga KONDOO?

Ushawahi wakuta ule ukiburi wao waki inamisha vichwa chini?

Kati ya mbuzi na Kondoo, basi kondoo ni mchafu zaidi, ni anakiburi zaidi alafu kiburi cha kimya kimya.

Alafu akili zao wanazijua wenyewe wakiamua jambo lao.

Nawashangaa sana wanakubaligi kuitwa MAKONDOO kanisani.
Kondoo nawafuga ni wapumbavu sana, wanapenda kukaa kimakundi, mmoja asipoona wenzie atalia na masauti yao mabaya.

Ni wabishi pale unapo wavuta wana kiburi hatari, ila ukishamjua kiongozi wa kundi basi hawana shida kuwa fuga.
 
Nikiwa mdogo, kuna kundi la vimbuzi saba nilikuwa nachunga. Kuna beberu mmoja alikuwa msumbufu sana hasa akiona majike. Huyu yeye machungani muda mwingi nilikuwa namfunga.

Siku moja jioni natoka kuchunga, amenisumbua njia nzima. Mara anatoka kundini anakwenda kulisha mazao ya watu. Namkimbiza nashika kamba namvuta anaresist na mamiguu yake yote manne, limenyanyua shingo limetoa ulimi kama linakara roho, nalichapa linatoka nduki linakwenda hovyo tuu kusiko julikana.

Alichokuja kuniudhi kabisa, nilikutana na dogo mwenzangu nae anatoka kuchunga mbuzi wa kwao. Tunafahamiana. Lile beberu acha lianze kuonesho umwamba kwa wale majike wa kundi la yule dogo. Linampanda huyu, linaacha linaenda kwa yule na yale makelele ya mabeberu yakiwa yanataka mbususu.

Nikijaribu kuliswaga lirudi kundini linakimbia hovyo. Yule dogo nae akaanza kunicheka. Nilipandisha hasira aisee. Nikatimua mbia kumfuata yule beberu. Akanyanyua miguu ya mbele tupigane sasa. Nikasimama. Nikaishika kamba nikaanza kumvuta anaresist huku mi namsogelea. Nilivomfikia nikamshika pembe nikampiga kichwa. Ile head to head yani. Hadi nikahisi kizunguzungu. Nikamuona nae ameanza kuruka ruka hovyo huku anatikisa kichwa. Alivyotulia akanyoosha njia hadi nyumbani. Yule beberu hakuwahi kunisumbua tena hadi alivyouzwa.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,

Wana visirani na viburi sijawahi ona ,

Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanza huna la kumfanya

Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga ,
Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt , mchungaji lazima utepete..
wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo mana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania



View attachment 2612382


View attachment 2612275
Ndo mana mitume karibia wengi walikua wakifuga mbuzi kabla ya kupewa utume ili waweze kuvumilia maudhi ya binadamu katika kulingania Dini
 
Kwetu kipindi cha masika ndio wasumbufu sana maana wanakuwa kwenye limitation(chini ya ulinzi) machungani na ndipo kipindi penye majani mabichi mazuri ikiwemo mazao.

kipindi cha Kiangazi wanakuwa wanachia maana tunakuwa hatuwalimit, tunawaachia wajichungie kwa kudhurura watakavyo ila ikifika jioni tunaenda kuwapokea(kuwatafuta kwa wale wakorofi kama Mabeberu ambao wanakuwa wanachanganyikana na makundi mengine ya mbuzi), pia mara nyingine huzoea hiyo hali na ikifika jioni wanarudi wenyewe nyumbani.
Huku kwetu kipindi cha kiangazi wanasumbua sana maana kuna migunga/accasia
 
Sisi uchagani tunafuga kwa kuwafungia ndani. Kuna kichanja cha nje na cha ndani. Sasa way back 2003 au 2004 kama sijasahau kuna mbuzi mmoja yeye haridhiki yani. Hata apewe majani vipi ataruka tu kwenda kujilia huko. Sasa akaruka zizi si akajiumiza kifuani. Aisee kesho yake mzee ananiita eti kwa nini mbuzi ameruka akajiumiza ulikua wapi? Nilipewa kipondo cha haja mpaka nikatoka vidonda miguuni. Ilibeba muda mimi kunsamehe mzee. Yani alitaka nisiende shule nichunge mbuzi wake au niwe nawakagua aisee?. Ilibibeba kumjua Yesu kujifunza kusamehe. Yani sijamsahau yule mbuzi moaka leo.
 
Wafugaji mje huku mtupe visa vya visirani vya mbuzi wa kienyeji
Nakumbuka vituko vyao vingi sana maana tuliwahi kuwa nao tulipokuwa kijijin wakati huo nikiwa mdogo

Mbuzi ni kama binadamu ambavyo wapo wenye tabia mbali mbali na mbuzi ni hvyo hvyo kuna vimalaya humo kwenye kundi la mbuzi,kuna wezi,kuna wambeya,pia kuna vihele hele

Mbuzi anatakiwa achungwe na watoto maana mtu mzima hzo jogging hutaziweza

Mbuzi vihele hele,nakumbuka tulikuwa na mbuzi wengi lakin ukichelewa kuwapeleka machungani kuna wale mbuzi wachache katika kundi watalia na kupiga kelele ili wazazi wawasikie ili wawaambie muwapeleke machungani

Mbuzi malaya,kuna vile vidume vidogo huwa vinatabia ya kupiga kelele ya kupanda jike usiku kucha na wakati hata vikipewa mbususu haviwezi kuifikia,pia wapo majike ambao wao kila mara utakuwa unawaona wanayapanda madume(ila baada ya kupata elimu niligundua kumbe huwa wanakuwa kwenye heat)

Mbuzi wezi,hawa huwa ni wajanja wajanja sana muda wote hawawazi kula nyasi wanataka kula vya kuiba mashambani,huwa na tabia ya kuwapiga pembe wenzao kama wakiwa karibu na mazao ili wakimbilie kwenye mazao,kipindi hicho nakumbuka tulikuwa tusipofunga vizur mlango wa banda basi usiku wanatoka,tulikuwa tukiwakamata tunawapanda kama farasi,na unapompanda inabid kuwa makin sana maana anakimbia sana na anakuwa na tabia ya kupita karibu na visiki au ukuta ili ujipige pale uumie,
bAada ya kuwajulia wakati wa kwenda kuwachunga ili wasisumbue sana tulikuwa tunaenda na kamba,wale wasumbufu tunawatia kamba
Nakumbuka nilkuwa nikiwapeleka machungani lazima nipoteze mbuzi,inabid niwarudishe nyumban ili nikamsake huyo/hao waliopotea

Katika story za wana jamaa mmoja aliwah niambia kuwa wao walikuwa wanawang'oa meno baadhi ya mbuzi wasumbufu,wakiwapeleka kunywa maji wanaanza kumshika mmoja mmoja wanamgonga na jiwe mpaka jino linatoka au wanamkamata wanamzamisha kichwa kwenye maji kwa muda ndo wanamtoa,hao waliokuwa wanatolewa meno itamchukua siku hata tatu atakuwa ametulia sana na hali majani sana kama siku zingine

TUlikuwa tusipowapatia maji ya kutosha,ile jioni wakati wa kuwarudisha walikuwa wakifika nyumban wanakuwa na fujo balaa watalazimisha mpaka waingie ndani,na wataangusha viti na kumwaga maji

Mbuzi sina hamu nao,nimechapwa sana enzi hzo kwasababu ya hawa wapuuzi pamoja na kwamba mimi nilikuwa mtoto mpole sana

wAlinifanya hata nisipate muda wa kucheza mpira hadi leo nikiambiwa nipige mpira naanguka tu mwenyewe
 
Back
Top Bottom