Saad30
JF-Expert Member
- May 26, 2020
- 2,737
- 5,464
Ulivyoandika na nilivyousoma huu uzi asee kweli hawa viumbe wanatesa...Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,
Wana visirani na viburi sijawahi ona ,
Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanza huna la kumfanya
Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga ,
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania
View attachment 2612275
Wakiamua kula mahindi yako sasa uliyoyaanika yapigwe na jua...afu unatoka shambani njaa kali 😂😂😂😂 asee utasema walikuwa wanakusubiri ndio wale mahindi yako.