Nimechunga sana Mbuzi hasa enzi za udogoni(kabla sijaanza primary na kipindi niko primary, huu wakati ndio nimechunga sana pamoja na Ng'ombe, Kondoo, Punda)
Hata sasa nikienda kijijini kusalimia, lazima nichunge kuwasaidia na pia kitu ambacho nakipenda kutokana na kukifanya sana Udogoni.
Kati ya Wanyama wanaofungwa, Mbuzi ndiye anayesumbua wakati wa kuchunga.
Kero kubwa ni ulafi, wanavamia mazao yoyote yaliyopo mbele yao. Pia wana akili ya kukutega/kukuhadaa wewe mchungaji. Wanaweza kujifanya wameshiba na kulala chini huku wakicheu(wakitafuna majani waliyomeza kwa kuyatapika na kuyatafuna tena), ukizibaa kidogo utakuta washaamka na kukimbilia lilipo shamba na kuvamia mazao.
Wakifika lilipo shamba wanaingia ndani zaidi wakale mazao huko ndani, wengine wanajificha huko ndani ili waendelee kula mazao.
Wakivamia shamba la mtama uliokaribia kuiva, wanalaza/dondosha mabua ya mtama na wale punje za mtama.
Ukienda kuwatoa, walio wakorofi wataanza kukimbilia ndani ya shamba huku wakiendelea kula mtama wanaokutana nao mbele.
Muda huo ukiwa unakimbizana na mbuzi kama una ng'ombe nao wanaanza kuvamia shamba, inakuwa mtafaruku.
Hii adha imetukuta sana wachungaji na ilikuwa ni sababu kubwa ya kuchezea stick endapo mwenye shamba akinasa umelisha mazao yake.