Hivi akili ya kuwachapa utaipata wapi? wakati wameshakuchanganya unawaza kuwatoa haraka na kukimbia mwenye shamba asikukute maana mtachanganywa wewe na mbuzi wako wote viboko,Vipi ukiwachapa viboko kama ng'ombe wanaskia?
Halafu alikuwa na dharau sana hata kundi la mbuzi wapite karibu yake hajichanganyiChampion aliupiga mwingi[emoji38]
Kulikuwa na kama vyuma pumbu za mbuzi inawekwa katikati.Halafu nyundo inagongwa juu ya chuma cha juu.Imagine na wewe unagonga pumbu la mbuzi 😁
Nduguyo huyo, ndio maana korofi sana kumbe mbuzi wanamtesa😂😂😂😂
Ukatili wa hali ya juu.Kulikuwa na kama vyuma pumbu za mbuzi inawekwa katikati.Halafu nyundo inagongwa juu ya chuma cha juu.
Umemaliza. Hasa Serengeti lager! Haki ya nani 🍻Ukiwa na bia, watamu mno[emoji39]
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku ,
Wana visirani na viburi sijawahi ona ,
Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii , na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani , anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanba huna la kumfanya
Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usku mzima , usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga ,
Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt , mchungaji lazima utepete..
Kama Una miadi ya kuonana na demu usiingie kwenye Banda la mbuzi Kwanza mana ni full kunuka kibeberu
wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo mana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop
, kama unaamini Una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama , vinginevyo unatutania
View attachment 2612382
View attachment 2612275
Pole sana!Nakumbuka vituko vyao vingi sana maana tuliwahi kuwa nao tulipokuwa kijijin wakati huo nikiwa mdogo
Mbuzi ni kama binadamu ambavyo wapo wenye tabia mbali mbali na mbuzi ni hvyo hvyo kuna vimalaya humo kwenye kundi la mbuzi,kuna wezi,kuna wambeya,pia kuna vihele hele
Mbuzi anatakiwa achungwe na watoto maana mtu mzima hzo jogging hutaziweza
Mbuzi vihele hele,nakumbuka tulikuwa na mbuzi wengi lakin ukichelewa kuwapeleka machungani kuna wale mbuzi wachache katika kundi watalia na kupiga kelele ili wazazi wawasikie ili wawaambie muwapeleke machungani
Mbuzi malaya,kuna vile vidume vidogo huwa vinatabia ya kupiga kelele ya kupanda jike usiku kucha na wakati hata vikipewa mbususu haviwezi kuifikia,pia wapo majike ambao wao kila mara utakuwa unawaona wanayapanda madume(ila baada ya kupata elimu niligundua kumbe huwa wanakuwa kwenye heat)
Mbuzi wezi,hawa huwa ni wajanja wajanja sana muda wote hawawazi kula nyasi wanataka kula vya kuiba mashambani,huwa na tabia ya kuwapiga pembe wenzao kama wakiwa karibu na mazao ili wakimbilie kwenye mazao,kipindi hicho nakumbuka tulikuwa tusipofunga vizur mlango wa banda basi usiku wanatoka,tulikuwa tukiwakamata tunawapanda kama farasi,na unapompanda inabid kuwa makin sana maana anakimbia sana na anakuwa na tabia ya kupita karibu na visiki au ukuta ili ujipige pale uumie,
bAada ya kuwajulia wakati wa kwenda kuwachunga ili wasisumbue sana tulikuwa tunaenda na kamba,wale wasumbufu tunawatia kamba
Nakumbuka nilkuwa nikiwapeleka machungani lazima nipoteze mbuzi,inabid niwarudishe nyumban ili nikamsake huyo/hao waliopotea
Katika story za wana jamaa mmoja aliwah niambia kuwa wao walikuwa wanawang'oa meno baadhi ya mbuzi wasumbufu,wakiwapeleka kunywa maji wanaanza kumshika mmoja mmoja wanamgonga na jiwe mpaka jino linatoka au wanamkamata wanamzamisha kichwa kwenye maji kwa muda ndo wanamtoa,hao waliokuwa wanatolewa meno itamchukua siku hata tatu atakuwa ametulia sana na hali majani sana kama siku zingine
TUlikuwa tusipowapatia maji ya kutosha,ile jioni wakati wa kuwarudisha walikuwa wakifika nyumban wanakuwa na fujo balaa watalazimisha mpaka waingie ndani,na wataangusha viti na kumwaga maji
Mbuzi sina hamu nao,nimechapwa sana enzi hzo kwasababu ya hawa wapuuzi pamoja na kwamba mimi nilikuwa mtoto mpole sana
wAlinifanya hata nisipate muda wa kucheza mpira hadi leo nikiambiwa nipige mpira naanguka tu mwenyewe
Hivi Zanzibar huwa mnafuga nini kingine ukiacha majini?Jf ilivyo. Utashangaa watu wote sasa humu mnachunga mbuzi. Hata waliozaliwa hospitali wilaya ilala CBD nao utakuta wanachunga mbuzi, Tiririkeni.
Mkuu sikusingizii, una maneno makali na kuna wakati una majibu ya kikatili sana.Mkuu Mimi sio mkorofi
vingine huwa vina dharau kupisha mtu njia 😂😂Ha haaaa, huenda wanawaza unawaletea maji au kitu flani mwenye nao amewazoeza kuwapa mda fulan