Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Sisi jioni ndo ulikuwa mda wa adhabu kama mchana walileta mambo sio,adhabu zilikuwa ni fimbo na wale wanaokimbia haraka kwenye mashamba tuliwapiga midomo tukisema waache uchoyo,sema ulikuwa utoto
 
Sisi jioni ndo ulikuwa mda wa adhabu kama mchana walileta mambo sio,adhabu zilikuwa ni fimbo na wale wanaokimbia haraka kwenye mashamba tuliwapiga midomo tukisema waache uchoyo,sema ulikuwa utoto
utoto miaka hiyo 🙌🙌🙌🙌😅😅😅😅😅
bibi akikuudhi una deal na mbuzi zake
unawafanya wapige kelele zitakazo muamsha huko alikojipumzikia
unajificha pembeni kumchora unasikia anajiseme nimewapa majani mnalia nn
kumbe washapewa pilipili🤣🤣🤣 ilimradi tafrani
 
visa ninavyo vingi maana tumewachunga sana utotoni na sasa hivi nina mradi wao pia

niseme kwa dhati mbuzi wametusaidia sana kipindi cha barehe . ikatokea siku moja mbuzi wetu kipenzi wa kwa jirani walikuja wageni basi ikabidi achinjwe sasa kabla hajajichwa kijana wa pale akatimka mbio kuja kutupasha habar kuwa mke wetu anachinjwa acha twende tukaanze kulia pale kwenye huo mji tulikuwa wa3 wote tunalia hadi wageni wakasituka wakiuliza sababu tunawaambia chinjeni mwingine ila huyu hapana 😂 😂 😂

hakuchinjwa ila walikuja kujua badae my wetu akauzwa😢😢💔💔
 
Mbuzi ukiwa unamchunga ghafla ianze kunyesha mvua wakimbilie vichakani ukiwatoa humo wewe ni mwanaume utapiga fimbo anajikunyata tu kuzunguka humohumo wakiona umewapiga sana wana hama kichaka yaani mpaka useme imetosha sasa
 
Mlitia mbuzi nyie wajuba💔
 
Mbuzi ukiwafungulia tu, ukimaliza kufunga zizi wanakuwa wapo km 1 mbele unaanza mbio 😀
 
Nishawah kulea kamoja mama yake alikufa
Kila napoenda kako miguun nikienda dukan ananifata nikimuacha nikamfungia analia balaaa
Nikilala anakuja kuniamsha
Nilikuwa namnywesha maziwa na kumuogesha nilimpenda sana alivyojua akachukuliwa
Nao wana hisia mkuu.
 
Ukipata muda nenda jamii ya wafugaji hasa wamasai.. kule bhna mbuzi anaishi kwa protocol ya hali ya juu sijawahi ona, Yani mpaka muda wa kukamuliwa maziwa mbuzi anajua, na ukichelewa ni kelele mfululizo.
Zaidi ya yote wale jamaa wanapenda mifugo yao sana mpaka mbuzi mwenyewe anajua kuwa anapendwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…