Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Mbuzi kwa dharau wanaweza kulia bandani bila sababu ukienda kutizama nini kinaendelea eti na wao wanakutizama design kama wewe fala umekuja eeh ukipiga hatua kadhaa wanaliamsha dude tena basi kukutesa tu..
 
Samahani:
Hivi ushawahi funga KONDOO?

Ushawahi wakuta ule ukiburi wao waki inamisha vichwa chini?

Kati ya mbuzi na Kondoo, basi kondoo ni mchafu zaidi, ni anakiburi zaidi alafu kiburi cha kimya kimya.

Alafu akili zao wanazijua wenyewe wakiamua jambo lao.

Nawashangaa sana wanakubaligi kuitwa MAKONDOO kanisani.
bora kondoo mara mia n wastaarabu sana...ila wakianza pigana kaa mbali
 
Hongereni
Mwezi uliopita nilijitia kiherehere kununua ng’ombe wa kienyeji, alitaka kunipa kesi ya mauaji baada ya kumpiga jirani

Nimeishia kumchinja siku ya Eid,
Sitaki tena mnyama Mwenye miguu minne kwangu
Sasa jirani yako analeta umbea kwenye nyumba za watu ng’ombe afanyeje

Ng’ombe ukiona amekupiga kuna mambo mawili

Unapiga umbea sana kumhusu

Unamuangalia demu wake kimatamanio😁😁😁

Hilo la umbea anaweza kukufikiriapo akakupa karipio tu

Ila hilo jingine zea iz no wei aut
Lazima akutaitishe tu😂
 
Sasa jirani yako analeta umbea kwenye nyumba za watu ng’ombe afanyeje

Ng’ombe ukiona amekupiga kuna mambo mawili

Unapiga umbea sana kumhusu

Unamuangalia demu wake kimatamanio😁😁😁

Hilo la umbea anaweza kukufikiriapo akakupa karipio tu

Ila hilo jingine zea iz no wei aut
Lazima akutaitishe tu😂
🤣🤣🤣 alitaka kunisababishia kesi
 
Mbuzi anaweza akawa anatafuna kitu hicho kitu ni kama vile hakiishi hapo yupo bandani ambapo hamna majani lakini unamuona anatafuna kitu kama.mtu anavyotafuna bigijii
 
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku.

Wana visirani na viburi sijawahi ona.

Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani, anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanba huna la kumfanya.

Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usiku mzima. usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga.

Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt, mchungaji lazima utepete.

Kama Una miadi ya kuonana na demu usiingie kwenye Banda la mbuzi Kwanza maana ni full kunuka kibeberu.

Wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo maana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop, kama unaamini una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama, vinginevyo unatutania.

View attachment 2612382


View attachment 2612275


View attachment 2612810

View attachment 2688995
Unafugia wapi ndugu.
 
Hahaaaaa, mzee wangu alikuwa anafuga. Ile nimemaliza form six, nikawa nawafungilia nawapeleka sehemu. Kuna mmoja huwaga anasumbua. Hata mzee huwa anamsumbua sana.

Siku 1 nawafungulia kanitoroka huku ameniburuza mkono ukutani kwani nilikuwa namfunga kamba. Nikachubuka na kutoka damu mkononi. Nikawa namfuata nimrudishe, akakimbia kama Kilomita 3 huku namfukuza. Akawa anakula vitu vya watu huku anakimbia

Hahaaaaa, nilipomshika huko mbali, nilimpiga hadi wapita njia wakaja mtetea. Kule kijijini wengi hawanijui ila kwa kuwa nimefanana na mzee na wanajua mbuzi za mzee. Wakawa wanamwambia mzee, yule mtoto wako mmoja mwanajeshi America sana mbuzi. Yaani nilimtandika mateke, magumi, vichwa, nilimpiga roba, vipepsi, makofi hadi kumng'ata masikio.
😅😂😂😂😂😂 ukifuga mbuzi unakuwa kichaaa et unamng’ata masikio una matatizo ya akili
 
Mbuzi ni viumbe wazuri ila wasumbufu .
Nafuga mbuzi ila ni mgeni kwenye haya mambo wiki mbili mbuzi wangu wanne wamefariki kisa kilikuwa hivi .

Ninaye kijana anawafuga ila jioni anawaleta kwangu hivyo alfajiri anawafuata pia , sasa siku hiyo wamerudishwa jioni nilisahau kufunga stoo ya mahindi .

Usiku wakaingia hao wanne wakala mahindi kwa kiasi walichopenda .

Asubuhi naamka nakuta hao wanne wanataabika kwa kupumua kwa shida na pia matumbo yao yamevimba sana .

Basi nikaamua niulize kwa watu kuwa hiki ni nini wakasema hao wamekula mahindi makavu na hapo wasinywe maji wakinywa maji watakufa , hivyo wanadai niwalishe magadi ili watoe gesi tumboni nikajisemea wacha niwape hayo magadi ila mpaka inafika mchana mbuzi wanapumua kwa shida na ni kama wanataka kufa .

Nikiwaza kumpiga bwana mifugo naogopa maana siku mbili nyuma tuligombana kisa pombe huko bar maana mimi niliwahi kufika hapo bar nikakuta kuna uhaba wa bia kulikuwa na bia tisa tu kwenye ile bar na hapa kijijini inatokeaga bar zote hazina bia hivyo ni mpaka ushuke mjini .

Hivyo nikamwambia muhudumu aziache kwenye friji na pia nikalipia nikawa nachukua moja moja nafurahia maisha alipokuja bwana mifugo naye anaforce apewe tatu wanamwambia zimenunuliwa haelewi anaforce ikabidi niingie front kumwambia nakuzingua sio mda hivyo tuliza tamaa zako .

Akapoa sana ila kwa vile ananiogopa na kuniheshimu , sasa nakuja kupata story mtaani ananikandia naringa sana .

Hivyo hata kumpigia sikuweza nikawa najua hatoweza kuwasaidia mbuzi wangu .
Basi saa saba ndiyo muda watoto wangu mbuzi walianza kupukutika , alianza mwanangu Celine , akaja mtoto wangu Cloude , akafuata Chriss na mwisho binti yangu mdogo Chyna alifariki saa kumi na moja jioni .

Ilikuwa siku ya huzuni sana kwangu na nyumba ilikuwa kubwa sana , niliwazika pembezoni na nyumba yangu nikiwa na ndugu zao wakubwa sita ila pia mbwa wangu kipenzi Chizika alikuwepo na alishuhudia mazishi yale mwanzo mwisho , pamoja na rafiki yangu na msiri wangu paka bwana Cherish naye aliona kila kitu .

Ni hivyo ndugu kuhusu usumbufu sijui lolote nawaona ni wazuri tu kikubwa wawe na kamba na pia uwe na sehemu maalumu ya kufugia japo sikatai kuwa ni viumbe wenye resistance sana wakiamua .

Endeleeni kupumzika nawakumbuka sana Celine , Cloude , Chyna na Chriss njia ni yetu sote .
 
Mwingine huyu hapa kajifunga mguu makusudi ili kufupisha kamba yake
20240319_153517.jpg
 
Back
Top Bottom