Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kabla jua halijazama niseme hili;
Ukitaka kutambua jamii Fulani inajitambua, basi tembelea Maeneo Yafuatayo;
1. Makazi Yao.
Makazi Yao yapo kwenye mpangilio. Kuna miti ya kutosha ya hewa, Bustani na Maua yakupendeza.
Kuna sehemu maalumu za kuhifadhia taka, pia Choo kipo cha kiungwana.
Makazi ya mtu humtambulisha mtu kuwa ni Binadamu au mnyama.
Unakuta jitu limesoma lakini nyumbani kwake hakuna miti ya kivuli, limekata miti Kama lipumbavu. Hopeless!
Umeshindwa kupanda Miti ya matunda basi hata Miti ya kivuli umeshindwa?
2. Nyumba za Ibada.
Nyumba ya Ibada humtambulisha mtu Kama ni mtu kweli au jitu lisilo jielewa.
Nyumba ya Ibada ni sehemu nyeti Kwa watu wenye kujitambua. Ni sehemu ambayo Kwa wanaojitambua wanaamini pale ndio huenda kumuabudu Mungu wao.
Taikon huwaga kuna vijumba mshenzi vya Ibada nikiviona huwa nabaki natingisha kichwa. Nawasikitikia waabuduo na huyo wanayemuabudu.
Mtu anayejitambua hawezi kuabudu kwenye msikiti au Kanisa lisiloeleweka. Hata Biblia inaelezea Jambo Hilo
Yaani kwako kuna vigae alafu unaabudu kwenye nyumba ya vumbi wewe si Mpumbavu tuu usiyejua hata Kwa nini unaishi. Anyway hatupangiani maisha.
3. Makaburini.
Moja ya mambo yanayomtambulisha mtu ni hatma ya makazi ya jamii yake. Makaburini inapohifadhiwa miili ni sehemu nyeti mno Sana Kwa watu wanaojitambua.
Nabii Ibrahimu alilijua hili ndio maana alinunua na kujenga kaburi ambalo yeye, mke wake na Watoto wake wangezikwa hapo.
Pia Simon mkirene aliandaa kaburi lake na familia yake, ndiye aliomba mwili WA Yesu uhifadhiwe katika Kaburi lake. KWa heshima.
Hakunaga taifa au jamii inayojielewa ambayo imeyatelekeza makaburi ya wazazi na mababu waliowaleta Duniani.
Ukitaka kujua mtu Fulani ana Uelewa kiasi gani WA utambuzi, mwambie akupeleke walipozikwa wazazi wake hapo utanielewa vyema.
Makaburi yameota majani hovyohovyo, uchafu na takataka zote zipo kwenye makaburi ya wapendwa wao na hawajali Jambo lolote.
4. Mahali anapofanyia KAZI/Ofisini.
Mtu anayejitambua lazima ofisi iwe Safi na katika mpangilio Mzuri.
Ivutie yeye, wateja wake pamoja wageni watakaomtembelea.
Unakuta jitu ofisi yake chafu, papo vangala vangala, jitu halijielewi alafu linategemea liheshimiwe.
Nani akuheshimu Kwa upumbavu wako.
Fika ofisini, ukiwa nadhifu,. Isafishe, ipange vizuri, kisha piga Dua kukaribisha ulinzi na baraka za siku hiyo kulingana na Mungu unayemuamini. Subiri wateja.
Sio ulete uchafu wako wakipumbavu.
Usafi ni moja ya ishara ya heshima na adabu. Huheshimu mahali unapofanya kazi, unataka kazi yako ibarikiwe.
Watu wengi wanasema Wazungu hawamubudu Mungu, hivi mliwahi ingia ofisi za Wazungu waliowengi? Ofisi zimenyooka, Safi na zinavutia.
Watu wengi tunashindwa kuelewa kuwa Maisha ndio ibada yenyewe. Vile unavyoishi ni ibada. Hata usipomtaja Mungu lakini kile kitendo cha kufuata kanuni za nature moja Kwa moja unafanya ibada.
Unakuta mtu ni Bodaboda, pikipiki chafu, mazingira ya kijiwe machafu, yeye MWENYEWE mchafu ananuka, alafu anataka kazi yake iheshimiwe. Thubutu!!
Mtu asiyejitambua hawezi kuheshimika.
Zipo kazi kama Garage za kushika shika Mafuta yanayochafu nguo lakini ndio maana kuna nguo maalumu za kuvaa, vitu viwe kwenye mpangilio.
Watu tujiheshimu bhana!
Unakuta fundi nguo mazingira yake machafu Hadi unajiuliza anawezaje kufanya kazi mahali Kama pale. Alafu analalamika akiletewa na wateja nguo zinazonuka Mavi.
Sasa Kama ofisi yako imekaa kimavimavi ulitaka uletewe nguo zinazonukia Marashi?
Kuna ofisi ukifika kupeleka nguo ishonwe kiraka au mtengenezo; Kama ni chafu unajiuliza mara mbilimbili. Lazima ukaifue Kwanza ndio uipeleke.
Naomba niishie hapa, wenye mapovu mnakaribishwa. Wakujifunza tumejifunza!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam