Ukitaka kujua ofisi unayotaka kufanya kazi, wafanyakazi wana hali gani, wewe tazama parking. Baaasi

Kuna swali huwa najiuliza, parking za shule za serikali mjini zinakua na magari, lakini parking za shule za vijijini huwezi kukuta gari, wajuzi nisaidieni hili
Wengi wa walimu wa mjini wanaotembelea magari wananunuliwa na waume zao ambao ni maafisa wa idara zenye maokoto mengi aidha Serikalini au binafsi
 
Acha ushamba utakufa masikini nausije kupost unanuka umasikini. Warren Buffet anatembea kwa miguu kwenda kwa mishe zake na ni tajiri 1 acha ushamba
 
Mpaka leo unatumia google translator?
 
Mkuu,
Kiswahili chako ni cha kuungaunga sana. Ulikulia nje ya Tanzania?
 
Boss unafeli sana kudhani Gari zuri ndio alama ya Mafanikio. Simshauri Kijana yeyote anayeajiriwa sasa kuanza na gari kabla hajajiwekeza. Nimeajiriwa tu nikajiona hadhi yangu Rav 4. Sitasahau Maisha ya Hasara niliyoishi baada ya hapo. Ashukuriwe Mpenzi aliyenishauri kuuza Gari nihamishie hasira kwenye Ardhi. Ndani ya mwaka alinisaidia kumiliki Mashamba na Nyumba. Nitapanda Daladala mpaka niwe MO au Bakhresa 🤣🤣🤣🤣🤣
 
K
Mzungumzie kahawa na tumbaku mkichoka njooni kwenye zao la pareto.
Pareto ni nyoko.
Ata pareto nayo ina process uzuri wa kahawa nikama godolo la Tanform maana anapanda kijana mpaka mjukuu anavuna sio kama pamba au pareto.Kahawa ukipanda baada ya miaka mitatu ukaanza kuvuna walai mpaka unakufa ata ukienda kuishi marekani au ukakimbia familia ukiwa na miche mia kwenye shamba lako ata mke ata uliza ulienda wapi.
 
Kaka nakusaport 100% ukiwa kijana usikimbilie kujenga kijijini nyumba ya maana kama unafahamu mshahara ni wakuunga, usikope kujenga nyumba ya kuishi kwa sababu haitakusaidia kurejesha mkopo, husinunue gari kama Mshahara unapita NMB kama jamaa fulani anavyosemaga labda uwe unatoka familia ya kishua, unafanya kazi idara ya Misitu, ugavi, Fedha na Afya.
 
Kuna chama cha ushirika kagera KCU 1990. Pale ukienda utakuta magari mawili au matatu parking tena ya milioni kumi, ndani furnitures zimechoka Cpu cijui pentium hipi , photocopy machine wanatumia copy writter Ila wanakula maisha BOT wakasome.
Hapo umeongopa braza
 
Wewe itakuwa Huna familia, Gari kwa sasa sio Luxury tena bali ni basic need, Usalama wa boda Boda ni Mdogo sana Siku Ugongwe ukatike mguu ukajitibu kwa gharama sana
Ukiwa na familia gari ni Muhimu sana
 
Vyama vya ushirika havina mishahara mizuri labda kama wanaiba fedha za wakulima.
Kaka Unapo zungumzia mishahara kama upo wizarani uko usiguse kabisa vitu vinaitwa bodi ya kahawa, bodi ya korosho, bodi ya pamba na bodi ya sukari hzo ni Federation sasa uku kwenye primary society kuna pesa zinatambaa
 
Kaka Unapo zungumzia mishahara kama upo wizarani uko usiguse kabisa vitu vinaitwa bodi ya kahawa, bodi ya korosho, bodi ya pamba na bodi ya sukari hzo ni Federation sasa uku kwenye primary society kuna pesa zinatambaa
Wamasemaga tembea uone.
 
Kumiliki gari Tanzania bado ni shughuli pevu kutokana na kodi. Yaani unalipa 100% ya CIF ni hatari mno. Mtu mwenye gari hapa TZ kajipinda haswa. Wazambia wanamiliki magari makali kutokana na kodi kuwa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…